Ahadi Za Mwana Ccm

kinepi_nepi

JF-Expert Member
Aug 16, 2007
869
235
Ahadi za mwana ccm
Rushwa sio adui wa haki nitatoa rushwa na nitapokea rushwa.
Kazi sio msingi wa maendeleo kwani wafanyakazi wengi ni masikini . Ufisadi na wizi wa mali za uma ndio msingi mkuu wa maendeleo.
Nitalinda na kutetea mafisadi wote kwa nguvu zangu zote.
Nitasema uongo daima , na fitina ndio msingi wa maisha.
Hakuna usawa na wananchi ila na mafisadi.
Chuki na ulaghai ndio misingi mikuu ya chama.
Mwongo ataenziwa na msema kweli ni adui wa chama.
Binadamu wote sio sawa mpaka awe fisadi na mwizi wa mali ya uuma.
Kazi ya raisi ni kulinda hizi ahadi kwa nguvu zake zote
 
Nakumbuka Shule ya Msingi nilikuwa naimba haya karibia kila wiki... I mean nilikuwa naimba kinyume cha haya. Serikali ya Tanzania ya Sasa inazidi kunithibitishia ya kwamba xmy childhood was a Big Joke na kwa sasa nazipata kwa ufasaha bila chenga!!!
 
Ahadi za mwana ccm
Rushwa sio adui wa haki nitatoa rushwa na nitapokea rushwa.
Kazi sio msingi wa maendeleo kwani wafanyakazi wengi ni masikini . Ufisadi na wizi wa mali za uma ndio msingi mkuu wa maendeleo.
Nitalinda na kutetea mafisadi wote kwa nguvu zangu zote.
Nitasema uongo daima , na fitina ndio msingi wa maisha.
Hakuna usawa na wananchi ila na mafisadi.
Chuki na ulaghai ndio misingi mikuu ya chama.
Mwongo ataenziwa na msema kweli ni adui wa chama.
Binadamu wote sio sawa mpaka awe fisadi na mwizi wa mali ya uuma.
Kazi ya raisi ni kulinda hizi ahadi kwa nguvu zake zote

Hizo ni ahadi za Mwana Kinepi..
 
Ina maana wamefanya maerekebisho juzi katika NEC? maana za zamani zilikuwa kinyume chake.
 
Jamani mmepat ridhaa kwa maandishi? Mnajadili kanuni za usalama wa nchi? jamani kuweni makini - MP Nyoosha
 
Ahadi za mwana ccm
Rushwa sio adui wa haki nitatoa rushwa na nitapokea rushwa.
Kazi sio msingi wa maendeleo kwani wafanyakazi wengi ni masikini . Ufisadi na wizi wa mali za uma ndio msingi mkuu wa maendeleo.
Nitalinda na kutetea mafisadi wote kwa nguvu zangu zote.
Nitasema uongo daima , na fitina ndio msingi wa maisha.
Hakuna usawa na wananchi ila na mafisadi.
Chuki na ulaghai ndio misingi mikuu ya chama.
Mwongo ataenziwa na msema kweli ni adui wa chama.
Binadamu wote sio sawa mpaka awe fisadi na mwizi wa mali ya uuma.
Kazi ya raisi ni kulinda hizi ahadi kwa nguvu zake zote

Hii kali mkuu kinepi,

Hii ndio kazi ya Makamba iliyobakia.
 
AHADI ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI

(1) Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja
(2) Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote
(3) Nitajitolea nafsi yangu kuondosha umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma.
(4) Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa.
(5) Cheo ni dhamana, sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.
(6) Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote.
(7) Nitashirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yetu.
(8) Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.
(9) Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na raia mwema wa Tanzania na Afrika.
 
Hizi zilishapitwa na wakati, mtafute kikwete au Rostam au Lowasa au Membe kama anakumbuka hata moja. Azimio la Mkapa lilizibadilisha azimio la kikwete inazitekeleza hizi ahadi mpya. Kilegee chama cha mafisadi na kifilie mbali.
 
Mkuu Kinepinepi,

Heshima mbele mkuu, hizi unazoleta ni siasa za kitoto sio watu wazima kama tunavyojulikana na taifa, mimi ni mwanachama wa CCM na sikumbuki hizi ahadi zako kuwepo kwenye chama changu, sio Chadema wote akili zao ni kama Wangwe,

so is CCM sio sisi wanachama wote ni mafisadi, tuna viongozi wachache ambao siku zao zinakaribia kufika mwisho, tafadhali jaribu kuheshimu hilo ili na wewe uheshimiwe japo kidogo.

Ahsante Mkuu
 
Heshima kwako mh.
Mimi nalia na chama kilichopo madarakani na kama wewe ni mmoja wao pole kama hujaziona hizo ahadi kwenye chama kwa maandishi basi matendo yanaeleza zaidi ya maandishi.
Sioni siku hiyo ikifika wala haitafika. kwani msururu wa urithi na ukiritimba bado ni mrefu. Unamaanisha kunasiku nitaona utawala wa sheria ndani ya chama. je wanachama wako wapi sasa na zama za akina mkapa. Je si wote wanateseka kwa ulaghai wa serikali ya CCM? kuwa CCM au kutokua CCM haimaanishi kitu kwa sasa. Hizo nilizo andika ndizo nguzo za CCM na ndilo azimio jipya la chama. Sio utoto huo ndio utu uzima kwani mimi na kizazi kijacho tumeshaathirika. Na hakuna wa kumfunga paka kengele ndani ya CCM kwani paka mwenyewe ni mbishi halafu mbabe, wafunga kengele woga na hawana nguvu.
 
Hapana mkuu bado nitakujibu kistaarabu kuwa hizo sio nguzo za CCM, ila ni nguzo za baadhi ya viongozi wachache, kwa sababu kama hizo ndizo nguzo CCm haikujiweka mdarakani, sisi wote wananchi tumewachagua tena for the past 45 years, sasa labda hizi unazozisema ni nguzo ambazo sisi wananchi wote tuliowachagua tunazikubali ndio maana tuliwachagua,

naona unajaribu kukimbia kivuli chako mwenyewe na maneno ya urithi off course ndio urithi tulioachiwa na Mwalimu, yaani hii CCM, na tuliowachagua CCM fopr the last 45 years ni nani mkuu kama sio mimi na wewe?
 
Mheshimiwa hakuna kivuli hapa wala sijikimbii. Mimi ninasema ukweli. Naomba nikukumbushe kuwa mpaka sasa tanzania tupo kizazi cha nne kiutawala. urithi mwalimu aliouacha hautumiki tena kwa sasa wanatumia urithi wa mwinyi na mkapa Halafu kikwete anauenzi urithi wa hawa mabwana wawili. Na kama hilo ni kweli niambie umerithi nini toka kwa mkapa na mwinyi kama wenyeviti na wakuu wa nchi. mwinyi rejea Ndolanga na loliondo, dhahabu nk.
Mkapa unajua mwenyewe. Bingwa msanii unaona mwenyewe anavyocheza rafu JK
Sasa ni ahadi gani kwa sasa zinaenziwa. Kumbuka Walimzika nyerere kabla hajafa na urithi wake kule Zanzibar, kwa azimio la Zanzibar.

Ufisadi ni msingi wa maisha na rushwa ndio nguzo ya CCM. kama unaona huu ni utoto subiria ukubwa.Hizi ndizo ahadi za mwana CCM. Inauma sana kwani sio wote wanaotengeneza ahadi kwani hata zile za mwanaTANU-CCM sio wote walishiriki ila wengi tuliziimba.

Kuwabadilisha wanaosimamia hizi ahadi sioni. kazi kubwa. Damu ya masikini inaweza kutupeleka kwenye uhuru wa kweli. Uhuru wa kiuchumi na kubadili ahadi za kiimla.
 
Mkuu unayosema yote ni sawa, lakini kubali kuwa nguzo za ccm ni zetu wote wananchi tunaowachagua for the last 45 years, zingekuwa sio nguzo zetu pia tusingewachagua, mbona hutaki hili mkuu na ni very simple thing,

maneno yako yote ni kweli tupu, ila unakwepa only one thing kuwa hizo nguzo ni zetu wote ccm na sisi wananchi tunaowachagua, tena for the last 45 years, au?
 
Mheshimiwa Field
Unayoyasema ni kweli, kwamba tatizo ni kwa wananchi kuendelea kuchagua viongozi wabovu. Ila mimi ninachojaribu kufanya ni kuwaonyesha wananchi kuwa misingi iliyokuwa imejengwa na kanuni za CCM imebadilika kivitendo. hivyo zama za ahadi za kale za mwanaCCM hazipo tena, sasa ni ahadi mpya ambapo nataka wanaCCM wazijue ili waamue kunyoa au kusuka. Sote tuliimbishwa na naamini kila mtanzania mwenye miaka zaidi ya 30 wengi wao waliimba ahadi zile lakini wengi hawajui kuwa zile ahadi zimefutika na hakuna anaye zisimamia wala kuzitenda. Ahadi za sasa za mwana CCM ni hizo za Kifisadi. Tuendelee kuwaelimisha wananchi wajue somo limebadilika. Wajue ukweli.Waweze kutoa maamuzi au kuhoji kulikoni???????????????
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom