lolypop
JF-Expert Member
- Jul 29, 2015
- 2,430
- 1,681
Habari zenu wadau,
Leo ninapenda kuzungumza kuhusu kupeana ahadi wakati tunapokuwa kwenye mahusiano. Utasikia ooh! baby nitakuoa, mwingine utamsikia akisema wewe ni mwanaume/ mwanamke wa maisha yangu sitakuacha.
Jamani kama huna mpango wa kuishi au kufunga ndoa na mpenzi uliyenaye usimpe ahadi kama hizo hapo juu.
Naomba kuwashirikisha ushuhuda uliotokea siku ya jana kanisani. Jana nilipokuwa kanisani mchungaji aliruhusu watu kutoa shuhuda na shukrani mbalimbali juu ya mambo Mungu aliyowatendea. Ndipo akasimama kaka mmoja anaitwa John (sio jina lake) na mke wake.
Wakasema wanamshukuru sana Mungu kwa wema aliowatendea mana walitafuta mtoto kwa muda wa miaka mitano bila mafanikio ila mwezi huu mke wake anaujauzito wa mwezi mmoja.
Akaendelea kusema; siku moja alichoka kwenda hospital kwa ajili ya tatizo la kutopata mtoto akaamua kwenda kwa mchungaji kumshikisha tatizo linalomsumbua, Mchungaji akamuuliza kabla ya huyu uliyemuoa ulikuwa na nani? Akajibu sijakuelewa mchungaji.
Mchungaji akarudia, nakuuliza hivi kabla ya kumuoa huyu mke uliyenaye ulikuwa kwenye uhusiano na mwanamke gani? John akajibu kuna dada nilikuwa naye anaitwa Monicca. Basi mchungaji akamwambia rudi ukamuombe msamaha Monicca. John akarudi nyumbani kwake akiwa na mawazo wapi atampata Monicca mana mara ya mwisho waliachana Monicca akiwa anafanya kazi Morogoro ila nyumbani kwao ni Mwanza.
Baada ya week moja akaamua kufunga safari kwenda Morogoro ofisi aliyokuwa anafanya kazi Monicca, cha ajabu alipofika akaambiwa amehamishwa kikazi yupo Mwanza. Akajipanga upya kwa safari ya Mwanza, Mungu akamsaidia akampata Monnicca.
Anasema siku alipokutana na Monicca, bibie huyo alilia sana akimlaumu kwa nini alimwacha wakati alimpa ahadi ATAMUOA. Anasema alijiheshimu na kumuheshimu John kama mume amtarajiwa lakini haikuwa hivyo, aliwakataa wanaume wengi kwa ajili yake.
John akajikaza, kwa upole akamwambia najua mama ndo maana nimekuja kuomba msamaha wako maana kwa huzuni niliyokupa imepelekea mpaka familia yangu imekosa furaha. Tuachana kwa zaidi ya miaka mitano sasa nimeoa lakini sijapata mtoto nisamehe mama.
Monicca akajibu; nimesamehe John, nenda na uwe na amani. Basi John akarudi kumweleza mchungaji ya kwamba nimeonana na Monicca na amenisamehe. alipofika kwa mchungaji akamwambia mwite mkeo tufanye maombi ya pamoja. Maombi yakafanyika na Mungu akatenda miujiza.
USHAURI WANGU KWA VIJANA:- Usimpe ahadi mpenzi wako ya kumuoa au kuolewa naye kama huna mpango nayeye.
USHAURI WANGU KWA MASHEIKH, WACHUNGAJI, MAPADRE NA WALE WOTE WANAOHUSIKA NA UFUNGAJI WA NDOA:- Kabla ya kufungisha ndoa ifanyike dua au maombi maalum ya kumtenga bwana harusi/bibi harusi mtarajiwa na nafsi za wanawake/wanaume aliowahi kukutana nao kimwili. Ndipo hawa watu wawili wasimame wao kama wao waingie kwenye agano la ndoa. Hii itasaidia kuwaepusha vijana na baadhi ya matatizo ya ndoa kama kutopata watoto, na ndoa zisizodumu. Mana ndoa za wakati huu zinavunjika sana
NB:- Yule wangu tulieachana miaka ile tulishaombana msamaha.
Siku njema