Ahadi za mahusiano: Usitoe ahadi kama hutamuoa/kuolewa nae

Penzi jipya linakuwaga tamu kuliko kitu chochote. Yani hapo unaweza ukatoa ahadi ambazo hata zingine hazipo.
 
Habari zenu wadau,

USHAURI WANGU KWA VIJANA:- Usimpe ahadi mpenzi wako ya kumuoa au kuolewa naye kama huna mpango nayeye.

USHAURI WANGU KWA MASHEIKH, WACHUNGAJI, MAPADRE NA WALE WOTE WANAOHUSIKA NA UFUNGAJI WA NDOA:- Kabla ya kufungisha ndoa ifanyike dua au maombi maalum ya kumtenga bwana harusi/bibi harusi mtarajiwa na nafsi za wanawake/wanaume aliowahi kukutana nao kimwili. Ndipo hawa watu wawili wasimame wao kama wao waingie kwenye agano la ndoa. Hii itasaidia kuwaepusha vijana na baadhi ya matatizo ya ndoa kama kutopata watoto, na ndoa zisizodumu. Mana ndoa za wakati huu zinavunjika sana

NB:- Yule wangu tulieachana miaka ile tulishaombana msamaha.
Kweli mkuu.
 
Wale wenye list ndefu ya wadada sasa ikiwapata hii balaa watasafiri kuzunguka dunia nzima kutafuta misamaha 7-8-10 bora usiweke ahadi we kula papuchi faidi kisha tambaa. no strings attached
 
Ameeen,ni kweli kabisa usimpe mtu ahadi ambayo hutaitekeleza,siyo tu sisi kwa sisi Hata kwa Mungu usitoe nadhiri ambayo hutaitekeleza,pia Hata kwa wazazi,waswahili wanasema Ahadi ni deni, hii itaendelea kukugharimu maisha yako yote deni hii itaendelea kuwepo kama hutofanya matengenezo,Asante kwa kushare nasi ushuhuda huu ,barikiwa
 
Hakuna kitu kinauma kama mwanaume kucheza na hisia za mwanamke.

Mwenyewe unajimaliza kwa viapo vyote kwa kuamini maneno ya mwanaume anayekuaminisha visivyo.

Anachokitamka mdomoni sicho anachokiamini moyoni mwake na mwanamke anamuamini mwanaume na kumpa moyo wake wote huku akikataa wanaume wengine wenye nia ya dhati kwake.

Na pale anapokuja kugundua kuwa aliyekuwa naye ni mbwa mwitu katika ngozi ya kondoo ndipo anapoishia kujuta na kulaani yeyote aliyemfikisha hapo.

Na Mungu naye si Mjomba lazima ule matunda ya matendo yako.
Na machozi ya mtu hugeuka laana wakati mwingine
 
hizi hadithi za kutunga huwa zinaangalia upande mmoja yaani kuonesha mateso kwa aliyetenda kosa tu hawakumbukagi huyu mkosaji akiadhibiwa kuna watu wataadhibiwa indirectly sasa kama mke wa john laana ilimkumba ya nini,au mungu huyo aliyetoa laana ni mungu wa mabua ila Mungu wa kweli hatoagi adhabu kwa wasiohusika
sikiliza mkuu hiyo ni shuhuda ya kweli, alafu mke wa john hakuazibiwa yeye maana kama angepata mwanaume mwingine angezaa bila tatizo. Mwenye mateso ni john na ninan angeweza kuzaa na mke wa mtu? ilibidi john ahangaike kuupata ukweli na tatizo lipo upande wake
 
Shida mabint nao wanapenda kuuliza, eti babie una mpango gan na mim! vidume ndio vinaanza maelezo!
Hapa sasa inabidi tubadilike usimpe ahadi ya kuja kumuoa mwambie suala la ndoa ni mipango ya Mungu
 
Ila huyo mchungaji na mke wa John wana mioyo ya pekee, wanaume wenyewe wa siku hizi anasafiri pekeyake kumuomba msamaha ex?? Aaaah lazima wangekumbushia kwanza then kuombana msamaha baadae
 
Wasichana wenyewe ndiyo husababisha hayo yote yatokee.

Unakuta anauliza utanioa? Usipotoa jibu linaloendana na lake lazima utaachwa.

Hivyo kuepuka kuachwa ghafla inabidi ukubali uendelee kufaidi tunda.
 
sikiliza mkuu hiyo ni shuhuda ya kweli, alafu mke wa john hakuazibiwa yeye maana kama angepata mwanaume mwingine angezaa bila tatizo. Mwenye mateso ni john na ninan angeweza kuzaa na mke wa mtu? ilibidi john ahangaike kuupata ukweli na tatizo lipo upande wake



mmmmh haya sawa,japo kishingo upande
 
Mfano mmevishana Pete ya uchumba na MTU mbele ya kanisa mkaombewa na kuwekeana nadhiri kwamba sitakua acha na ikitokea nipate matatizo.na mahari ikatolewa ikatokea misunderstanding kidogo jamaa akakuacha kuna haja ya kumtafuta umuombe msamaha?
 
Mfano mmevishana Pete ya uchumba na MTU mbele ya kanisa mkaombewa na kuwekeana nadhiri kwamba sitakua acha na ikitokea nipate matatizo.na mahari ikatolewa ikatokea misunderstanding kidogo jamaa akakuacha kuna haja ya kumtafuta umuombe msamaha?
Kwa kuwa pete ni agano inabidi kuvunja ilo agano kila mtu awe huru kupata mwenzi mwingine. Bila utaoa/ kuolewa ila ndoa itakuwa na changamoto sana
 
afi sana nani kweli ...somo kama hili nilikuwa namegewa namheshmiwa mmoja pili after ibada.....kuna spirit zipo counseling inahitajika...kutenganisha rohoza kingono za wanaume na wanawake wa nyuma...maana utaoa au kuolewaila umefungwana vitu vyazamani
Ni kweli kabisa mkuu
 
Back
Top Bottom