Ahadi za mahusiano: Usitoe ahadi kama hutamuoa/kuolewa nae

lolypop

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2015
Messages
1,621
Points
2,000

lolypop

JF-Expert Member
Joined Jul 29, 2015
1,621 2,000
Habari zenu wadau,

Leo ninapenda kuzungumza kuhusu kupeana ahadi wakati tunapokuwa kwenye mahusiano. Utasikia ooh! baby nitakuoa, mwingine utamsikia akisema wewe ni mwanaume/ mwanamke wa maisha yangu sitakuacha.

Jamani kama huna mpango wa kuishi au kufunga ndoa na mpenzi uliyenaye usimpe ahadi kama hizo hapo juu.

Naomba kuwashirikisha ushuhuda uliotokea siku ya jana kanisani. Jana nilipokuwa kanisani mchungaji aliruhusu watu kutoa shuhuda na shukrani mbalimbali juu ya mambo Mungu aliyowatendea. Ndipo akasimama kaka mmoja anaitwa John (sio jina lake) na mke wake.

Wakasema wanamshukuru sana Mungu kwa wema aliowatendea mana walitafuta mtoto kwa muda wa miaka mitano bila mafanikio ila mwezi huu mke wake anaujauzito wa mwezi mmoja.

Akaendelea kusema; siku moja alichoka kwenda hospital kwa ajili ya tatizo la kutopata mtoto akaamua kwenda kwa mchungaji kumshikisha tatizo linalomsumbua, Mchungaji akamuuliza kabla ya huyu uliyemuoa ulikuwa na nani? Akajibu sijakuelewa mchungaji.

Mchungaji akarudia, nakuuliza hivi kabla ya kumuoa huyu mke uliyenaye ulikuwa kwenye uhusiano na mwanamke gani? John akajibu kuna dada nilikuwa naye anaitwa Monicca. Basi mchungaji akamwambia rudi ukamuombe msamaha Monicca. John akarudi nyumbani kwake akiwa na mawazo wapi atampata Monicca mana mara ya mwisho waliachana Monicca akiwa anafanya kazi Morogoro ila nyumbani kwao ni Mwanza.

Baada ya week moja akaamua kufunga safari kwenda Morogoro ofisi aliyokuwa anafanya kazi Monicca, cha ajabu alipofika akaambiwa amehamishwa kikazi yupo Mwanza. Akajipanga upya kwa safari ya Mwanza, Mungu akamsaidia akampata Monnicca.

Anasema siku alipokutana na Monicca, bibie huyo alilia sana akimlaumu kwa nini alimwacha wakati alimpa ahadi ATAMUOA. Anasema alijiheshimu na kumuheshimu John kama mume amtarajiwa lakini haikuwa hivyo, aliwakataa wanaume wengi kwa ajili yake.

John akajikaza, kwa upole akamwambia najua mama ndo maana nimekuja kuomba msamaha wako maana kwa huzuni niliyokupa imepelekea mpaka familia yangu imekosa furaha. Tuachana kwa zaidi ya miaka mitano sasa nimeoa lakini sijapata mtoto nisamehe mama.

Monicca akajibu; nimesamehe John, nenda na uwe na amani. Basi John akarudi kumweleza mchungaji ya kwamba nimeonana na Monicca na amenisamehe. alipofika kwa mchungaji akamwambia mwite mkeo tufanye maombi ya pamoja. Maombi yakafanyika na Mungu akatenda miujiza.

USHAURI WANGU KWA VIJANA:- Usimpe ahadi mpenzi wako ya kumuoa au kuolewa naye kama huna mpango nayeye.

USHAURI WANGU KWA MASHEIKH, WACHUNGAJI, MAPADRE NA WALE WOTE WANAOHUSIKA NA UFUNGAJI WA NDOA:- Kabla ya kufungisha ndoa ifanyike dua au maombi maalum ya kumtenga bwana harusi/bibi harusi mtarajiwa na nafsi za wanawake/wanaume aliowahi kukutana nao kimwili. Ndipo hawa watu wawili wasimame wao kama wao waingie kwenye agano la ndoa. Hii itasaidia kuwaepusha vijana na baadhi ya matatizo ya ndoa kama kutopata watoto, na ndoa zisizodumu. Mana ndoa za wakati huu zinavunjika sana

NB:- Yule wangu tulieachana miaka ile tulishaombana msamaha.

Siku njema
 
griffin2

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2015
Messages
620
Points
1,000

griffin2

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2015
620 1,000
Hakuna kitu kinauma kama mwanaume kucheza na hisia za mwanamke.

Mwenyewe unajimaliza kwa viapo vyote kwa kuamini maneno ya mwanaume anayekuaminisha visivyo.

Anachokitamka mdomoni sicho anachokiamini moyoni mwake na mwanamke anamuamini mwanaume na kumpa moyo wake wote huku akikataa wanaume wengine wenye nia ya dhati kwake.

Na pale anapokuja kugundua kuwa aliyekuwa naye ni mbwa mwitu katika ngozi ya kondoo ndipo anapoishia kujuta na kulaani yeyote aliyemfikisha hapo.

Na Mungu naye si Mjomba lazima ule matunda ya matendo yako.
 
Jembekillo

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2011
Messages
4,173
Points
2,000

Jembekillo

JF-Expert Member
Joined Nov 29, 2011
4,173 2,000

yaani kweli mwanamke umwambie ooh sina lengo la kukuoa nakuchezea tu halafu nakuacha,unadhani utapata mwanamke gani,uongo lazima ndio maana tumeambiwa tuishi nao kwa akili. labda Miss Natafuta pekee ndo anaweza kuvimilia hayo.
 
Jembekillo

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2011
Messages
4,173
Points
2,000

Jembekillo

JF-Expert Member
Joined Nov 29, 2011
4,173 2,000
Hapa najiuliza, kama John ndio aliyemtenda ex wake, ilikuwaje hiyo "adhabu/laana" ikamhusu mkewe pia?

Ujumbe mzuri lakini.

hizi hadithi za kutunga huwa zinaangalia upande mmoja yaani kuonesha mateso kwa aliyetenda kosa tu hawakumbukagi huyu mkosaji akiadhibiwa kuna watu wataadhibiwa indirectly sasa kama mke wa john laana ilimkumba ya nini,au mungu huyo aliyetoa laana ni mungu wa mabua ila Mungu wa kweli hatoagi adhabu kwa wasiohusika
 
Jembekillo

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2011
Messages
4,173
Points
2,000

Jembekillo

JF-Expert Member
Joined Nov 29, 2011
4,173 2,000
Hakuna kitu kinauma kama mwanaume kucheza na hisia za mwanamke.

Mwenyewe unajimaliza kwa viapo vyote kwa kuamini maneno ya mwanaume anayekuaminisha visivyo.

Anachokitamka mdomoni sicho anachokiamini moyoni mwake na mwanamke anamuamini mwanaume na kumpa moyo wake wote huku akikataa wanaume wengine wenye nia ya dhati kwake.

Na pale anapokuja kugundua kuwa aliyekuwa naye ni mbwa mwitu katika ngozi ya kondoo ndipo anapoishia kujuta na kulaani yeyote aliyemfikisha hapo.

Na Mungu naye si Mjomba lazima ule matunda ya matendo yako.
avatar yako tu inaonesha wewe wa mapenzi kwelikweli (jokes)
 
ndetia

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2012
Messages
543
Points
500

ndetia

JF-Expert Member
Joined Jun 9, 2012
543 500
Habari zenu wadau! Leo ninapenda kuzungumza kuhusu kupeana ahadi wakati tunapokuwa kwenye mahusiano. Utasikia ooh! baby nitakuoa, mwingine utamsikia akisema wewe ni mwanaume/ mwanamke wa maisha yangu sitakuacha.

Jamani kama huna mpango wa kuishi au kufunga ndoa na mpenzi uliyenaye usimpe ahadi kama hizo hapo juu.

Naomba kuwashirikisha ushuhuda uliotokea siku ya jana kanisani. Jana nilipokuwa kanisani mchungaji aliruhusu watu kutoa shuhuda na shukrani mbalimbali juu ya mambo Mungu aliyowatendea. Ndipo akasimama kaka mmoja anaitwa John (sio jina lake) na mke wake. Wakasema wanamshukuru sana Mungu kwa wema aliowatendea mana walitafuta mtoto kwa muda wa miaka mitano bila mafanikio ila mwezi huu mke wake anaujauzito wa mwezi mmoja.
Akaendelea kusema; siku moja alichoka kwenda hospital kwa ajili ya tatizo la kutopata mtoto akaamua kwenda kwa mchungaji kumshikisha tatizo linalomsumbua, Mchungaji akamuuliza kabla ya huyu uliyemuoa ulikuwa na nani? Akajibu sijakuelewa mchungaji.. Mchungaji akarudia, nakuuliza hivi kabla ya kumuoa huyu mke uliyenaye ulikuwa kwenye uhusiano na mwanamke gani? John akajibu kuna dada nilikuwa naye anaitwa Monicca. Basi mchungaji akamwambia rudi ukamuombe msamaha monicca.

John akarudi nyumbani kwake akiwa na mawazo wapi atampata Monicca mana mara ya mwisho waliachana monicca akiwa anafanya kazi morogoro ila nyumban kwao ni mwanza. Baada ya week moja akaamua kufunga safari kwenda Morogoro ofisi aliyokuwa anafanya kazi Monicca, cha ajabu alipofika akaambiwa amehamishwa kikazi yupo mwanza. Akajipanga upya kwa safari ya mwanza, Mungu akamsaidia akampata monnicca.

Anasema siku alipokutana na monicca, bibie huyo alilia sana akimlaumu kwa nini alimwacha wakati alimpa ahadi ATAMUOA. Anasema alijiheshimu na kumuheshimu john kama mume amtarajiwa lakini haikuwa hivyo. aliwakataa wanaume wengi kwa ajili yake. John akajikaza, kwa upole akamwambia najua mama ndo maana nimekuja kuomba msamaha wako maana kwa huzuni niliyokupa imepelekea mpaka familia yangu imekosa furaha. Tuachana kwa zaidi ya miaka mitano sasa nimeoa lakini sijapata mtoto nisamehe mama.
Monicca akajibu; nimesamehe john, nenda na uwe na amani. Basi John akarudi kumweleza mchungaji ya kwamba nimeonana na monicca na amenisamehe. Alipofika kwa Mchungaji akamwambia mwite mkeo tufanye maombi ya pamoja. Maombi yakafanyika na Mungu akatenda miujiza.

USHAURI WANGU KWA VIJANA:- Usimpe ahadi mpenzi wako ya kumuoa au kuolewa naye kama huna mpango nayeye.

USHAURI WANGU KWA MASHEIKH, WACHUNGAJI, MAPADRE NA WALE WOTE WANAOHUSIKA NA UFUNGAJI WA NDOA:- Kabla ya kufungisha ndoa ifanyike dua au maombi maalum ya kumtenga bwana harusi/bibi harusi mtarajiwa na nafsi za wanawake/wanaume aliowahi kukutana nao kimwili. Ndipo hawa watu wawili wasimame wao kama wao waingie kwenye agano la ndoa. Hii itasaidia kuwaepusha vijana na baadhi ya matatizo ya ndoa kama kutopata watoto, na ndoa zisizodumu. Mana ndoa za wakati huu zinavunjika sana

NB:- yule wangu tulieachana miaka ile tulishaombana msamaha.

cku njema
Shida mabint nao wanapenda kuuliza, eti babie una mpango gan na mim! vidume ndio vinaanza maelezo!
 
afande kifimbo

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2015
Messages
6,255
Points
2,000

afande kifimbo

JF-Expert Member
Joined Aug 31, 2015
6,255 2,000
afi sana nani kweli ...somo kama hili nilikuwa namegewa namheshmiwa mmoja pili after ibada.....kuna spirit zipo counseling inahitajika...kutenganisha rohoza kingono za wanaume na wanawake wa nyuma...maana utaoa au kuolewaila umefungwana vitu vyazamani
 
Forum statistics

Threads 1,391,812
Members 528,470
Posts 34,090,221
Top