Elections 2015 Ahadi za Kikwete zaitesa CCM

jme

JF-Expert Member
Aug 4, 2013
4,665
4,797
KWA UFUPI
Baadhi ya ahadi za Rais:
1. Kununua meli mpya Ziwa Victoria
2. Kujenga reli mpya Kati kutoka Dar Salaam kwenda bara
3. Kumaliza migogoro ya ardhi
4. Kutokomeza ugonjwa wa malaria 2015
5. Kumaliza matatizo ya walimu
6. Kununua bajaji 400 za kubebea wagonjwa
Nape asema Rais ametekeleza kwa kiasi kikubwa ahadi zake, wasomi , wanasiasa wasema utekelezaji ni mdogo

Dar es Salaam. Ahadi zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwa wananchi katika mikutano mbalimbali nchini wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2010, huenda zikawa mwiba kwa CCM katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, kutokana na nyingi kutokutekelezwa au kuwa katika hatua za mwanzo.

Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, kwa nyakati tofauti alitoa ahadi kusaidia kuwakwamua wananchi kutoka kwenye dimbwi la umaskini, maradhi na kuboresha upatikanaji wa elimu nchini. Ahadi hizo zilitarajiwa kukamilika kabla hajatoka madarakani.

Ikiwa imebaki takriban miezi 10 ya uongozi wa kipindi cha pili cha awamu ya nne kufikia ukomo, muda unakwenda haraka na utekelezaji wa ahadi hizo unasuasua jambo linalotia shaka iwapo kila ahadi itatekelezwa kwa wakati.

Kushindwa kutekeleza ahadi hizo ambazo zimo katika kitabu cha ahadi za Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania, Jakaya Kikwete wakati wa kampeni za urais 2010, kilichondaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, kunaiweka Serikali ya CCM katika wakati mgumu hasa pale itakaporudi kwa wananchi kutoa ahadi nyingine kwenye kampeni za uchaguzi mkuu ujao.

Nape

Alipoulizwa kuhusu ahadi hizo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema Rais Kikwete ametekeleza ahadi zaidi ya inavyoahidi ilani ya CCM.

"Ukitaka kumtendea haki Rais Kikwete katika utekelezaji wa ahadi zake, lazima uangalie kitabu chote cha ahadi harafu upate ushahidi wa viongozi wawakilishi au kuzunguka kwenye maeneo zilizokotolewa ahadi hizo," alisema na kuongeza;

"Kwa ufupi tu, Rais huyu amefanikiwa kutekeleza ahadi nyingi ambazo ziko kwenye ilani na zile alizotoa papo kwa papo."

Hata hivyo Nape alimwahidi mwandishi wa gazeti hili kutoa ufafanuzi wa ahadi zilizotekelezwa na Rais kwa kipindi chote alichokaa madarakani wiki ijayo.

Turuka

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk Florens Turuka alisema ofisi yake kwa sasa iko kwenye uchambuzi na uandaaji wa kitabu kitakachoeleza utekelezaji wake.

Turuka alisema kazi hiyo itakamilika kwa miezi miwili kuanzia sasa."Yapo mengi sana aliyoyafanya rais, lakini tutaweka wazi wala siyo siri, kazi zote alizofanya zinaonekana ila kwa sasa itakuwa vigumu kubainisha kiwango cha ahadi alizotekeleza," alisema Turuka.

Rais Kikwete alipokuwa wilayani Bunda, Mkoa wa Mara aliahidi kutokomeza ugonjwa malaria ifikapo mwaka 2015, lakini mpaka sasa ugonjwa huo umebaki kuwa tishio na ukipoteza maisha ya Watanzania wengi kila mwaka.

Rais Mstaafu wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Primus Saidia alisema jana kuwa kwa mujibu wa malengo ya Milenia, Tanzania imepunguza vifo vitokanavyo na malaria licha ya kuendelea kukabiliwa na changamoto kadhaa.

Alisema kwa hali ilivyo hivi sasa nchini, ambapo dawa hazipatikani kwa kiwango kinachotakiwa ni vigumu kufanikiwa kutokomeza ugonjwa huo kwa asilimia 100 mwaka huu.

"Kama tukipata Rais mzuri ambaye ataweka nguvu kwenye sekta ya afya, malaria inaweza kuondoka kwa asilimia 100 baada ya miaka 15," alisema Dk Saidia.

Akiwa wilayani Nzega mkoani Tabora, Rais Kikwete aliahidi kuwa Serikali yake ingejenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya Ziwa, lakini mpaka sasa ahadi hiyo haijakamilika ingawa tayari ameshakutana na Kampuni ya China Railway Group Limited inayotarajiwa kutekeleza mradi huo.

Pia, akiwa Tanga Mjini, Rais Kikwete aliahidi kuhakikisha kuwa mkoa huo unakuwa jiji la viwanda. Ahadi hiyo mpaka sasa haijakamilika ingawa tayari maeneo kwa ajili ya wawekezaji yamekwishatengwa.

Akiwa wilayani Igunga mkoani Tabora, Rais Kikwete aliahidi kuwa wananchi wa Tabora wangeanza kutumia maji kutoka Ziwa Victoria. Ahadi hiyo mpaka sasa haijakamilika japokuwa akijibu swali bungeni, Naibu Waziri wa Maji, Dk Binilith Mahenge alisema mwaka 2013/14 Serikali ilitenga Sh450 milioni kwa ajili ya upembuzi yakinifu, usanifu wa kina na uandaaji wa nyaraka za zabuni.

Ahadi nyingine za Rais Kikwete ni pamoja na kumaliza migogoro ya ardhi nchini, wakulima kuacha kutumia jembe la mkono na kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba iliyozama Mei 21, 1996.

Pia, kiongozi huyo wa nchi aliahidi kuimarisha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), kwa miaka mitatu, kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali na kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalumu chenye vifaa vya kupambana na wahalifu.

Katika orodha ya ahadi hizo, pia Rais Kikwete aliahidi kumaliza tatizo la walimu nchini. Hata hivyo, bado walimu wameendelea kuinyooshea kidole Serikali wakilalamikia kushindwa kuwapandisha madaraja, malimbikizo ya madeni na mishahara midogo.

Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Ezekiah Oluoch alisema licha ya kuwa Rais Kikwete amefanya mambo mengi tangu alipoingia madarakani, ataiacha nchi ikiwa njiapanda kielimu.

Alisema Rais Kikwete aliahidi kutatua tatizo la kupandishwa madaraja walimu, lakini mpaka mwisho wa mwaka huu kutakuwa na walimu 120,000 wanaostahili kupandishwa madaraja.

Akifafanua alisema: "Mwaka jana walimu 40,000 hawakupandishwa madaraja, mwaka huu wengine 40,000 walitakiwa kupandishwa na Julai, 2015 wengine tena watahitaji kupandishwa madaraja."

Oluoch alieleza kuwa Rais Kikwete aliwaahidi walimu kuwa angewaanzishia tume yao, lakini mpaka sasa hakuna hata muswada uliotayarishwa.

Pia, alisema Oktoba 5, 2010 huko Songea mkoani Ruvuma, Rais Kikwete aliwaahidi walimu kuwa angeunda Bodi ya Taaluma ya Walimu, lakini jambo hilo bado halijatekelezwa.

"Hili tunaliona kama ni deni, Rais asiondoke Ikulu bila kutekeleza ahadi hizo," alisema.

Aliongeza kuwa: "Serikali ya awamu ya nne inaiacha nchi njiapanda kielimu, elimu haikupaswa kusimamiwa na Tamisemi inatakiwa isimamiwe na Wizara ya elimu."

Vilevile, Rais Kikwete aliahidi kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko ya Kilosa, kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa na kujenga Bandari Kasanga.

Ahadi zingine ni kufufua Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira, kuzuia hatari ya Kisiwa cha Pangani kuzama, kumaliza tatizo la maji katika Wilaya ya Same, kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu mkubwa wa walimu na kununua vyandarua viwili kwa kila kaya.

Rais Kikwete aliahidi kumaliza tatizo la ukosefu wa umeme mkoani Arusha, kukopesha wavuvi zana za kilimo, kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido, kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti na kusambaza maji nchi nzima.

Kuhakikisha Jimbo la Isimani linapata maji ya uhakika, kuweka lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Serikali kujenga upya Bandari ya Mbambabay.

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Samwel Ruhuza alisema Rais Kikwete anaweza kutekeleza ahadi zake kwa asilimia zaidi ya 70 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

"Lazima tuwe wakweli huyu Rais amefanya mengi sana, yaani ukiangalia kuna ahadi nyingi kafanya japokuwa hawezi kumaliza zote kwa muda uliobakia," alisema Ruhuza.

Hata hivyo, aliongeza kuwa baadhi ya ahadi ambazo hazijatekelezwa mpaka sasa ni pamoja na ujenzi wa barabara za Kigoma-Nyakanazi(km330), Lulenge-Mulungarama(km100),Karagwe-Ngara(km150).

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shirikisho la Watendaji wakuu wa Makampuni nchini(CEOs Roundtable-Tanzania),Ali Mufuruki alisema ahadi alizotekeleza n8i nyingi japokuwa hataweza kumalizia zilizobakia.

"Lakini labda nikupatie mfano, unaweza kuahidi watoto wako zawadi na ukawanunulia wote, inatokea wengine wanakosa kwa hivyo sioni kama ni tatizo hilo," alisema Mufuruki.

Chanzo:Mwananchi





 
Arusha tuliambiwa mgao wa umeme utaisha muda naandika hapa hakuna umeme.
 
hivi kile kivuko ( sijui meli ) aliyoahidi kwamba itatoka KYELA itungi port hadi MBAMBA BAY kishatimiza ?
 
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...hadi-za-kikwete-kwa-wananchi-2010-2015-a.html

Orodha ya ahadi za Kikwete kwa wananchi 2010-2015


AHADI - ALIITOA AKIWA WAPI...

  1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
  2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
  3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
  4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
  5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
  6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
  7. Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
  8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
  9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
  10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
  11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
  13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
  14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
  15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
  16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
  17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
  19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
  20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
  21. Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
  22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
  23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
  24. Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
  25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
  27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
  28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
  29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
  30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
  31. Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
  32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
  33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
  34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
  35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
  36. Kulinda haki za walemavu - Makete
  37. Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
  38. Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
  39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
  41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
  42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
  43. Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
  44. Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
  46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
  47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
  48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
  50. Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
  51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
  52. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
  53. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
  54. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
  55. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
  56. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
  57. Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
  58. Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  59. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
  60. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
  61. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
  62. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
  63. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
  64. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
  65. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  66. Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
  67. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
  68. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
  69. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha
 
zikiwa zimepita takribani siku mbili rangu ccm izundue kampeini zake rasmi pale jangwani,na zikiwa zimepita zaidi ya miaka 50 ya uhuru wa nchi hii,chama kikongwe barani africa ccm kimekuwa kinara wa utoaji ahadi kemkem,zenye kila aina ya ushawishi kumfanya mtanzania maskini wa kutupwa aliyesababishiwa umaskini huu na ccm hii hii kutamani kukirudisha tena madarakani,nchi hii 36% ya watanzania wanaishi chini ya dola moja ilhali pengo kati ya maskini na tajiri likizidi kuongezeka kwa kasi,tangu mfumo wa vyama v8ngi uanze ni ahadi lukuki zimetolewa na chama hiki hatahivyo utekelezaji wake ni sifuri,miaka kumi ilopita ccm ilikuja na slogan ya "hali mpya nguvu mpya kasi zaidi,miaka mitano baadaye maisha bora kwa kila mtanzania inawezekana" wananchi walidhani wamepata pa kuponea,kunbe la hasha.huu ni wakti wa kampeini,ccm inatoa ahadi mpya wakti zile za miaka 50 ilopita hazijatekelezwa,ngombea uraisi anatoa maneno matamu matamu huku akijua wazi kuwa ccm ina rekodi mbaya ya utekelezaji wa ilani yake ya uchaguzi,hebu tujiulize,je? Ccm inayotoa ahadi mpya ni ile ile au ccm mpya?? kazi kwenu
 
Mie najiuliza sana ahadi gani mpya anazosema MUUZA NYUMBA wakati jk alitoa ahadi zote ambazo zinapaswa kutolewa na wagombea urais hadi 2025.
 
Mie najiuliza sana ahadi gani mpya anazosema MUUZA NYUMBA wakati jk alitoa ahadi zote ambazo zinapaswa kutolewa na wagombea urais hadi 2025.

ACHENI USHAMBA NYINYI, NJOONI HATA NCHI ZILIZOENDELEA ZA EUROPE AU MAREKANI WAKATI WA KAMPENI AHADI HUWA ZINAROTATE HAPO HAPO; AFYA, makai, elimu social services in general; MALOFA NA WAPUMBAVU KWELI NYINYI MKAPA HAKUKOSEA
 
ACHENI USHAMBA NYINYI, NJOONI HATA NCHI ZILIZOENDELEA ZA EUROPE AU MAREKANI WAKATI WA KAMPENI AHADI HUWA ZINAROTATE HAPO HAPO; AFYA, makai, elimu social services in general; MALOFA NA WAPUMBAVU KWELI NYINYI MKAPA HAKUKOSEA

Matusi ya nini sio ujanja nitaeleza kidogo wewe huelewi hata unachozungumza CCM kupitia kwa mgombea wao 2010-2015 walitoa ahadi ambazo hawakuzitekeleza kuhusiana na hayo hayo uliyoyataja ilani za vyama zina kusudi ya kuboresha huduma za kijamii kama ulivyozitaja hapo juu sasa mfano unatoa ahadi ya kujenga reli mpya standard gauge halafu hukuitekeleza na zipo nyingi kama mia nane unatoa ahadi nyingine tena juu ya zile au hizi ahadi ni kama fasheni tu kuwafurahisha wapiga kura au mdo ushujaa na wewe ndo unaona poa tu!Aaaagh!haya bana wewe ni mjanja mie sikuwezi.
 
Eti magufuli anataka kulinda twiga na tembo wa Tanzania

Wakati wahusika wako naye meza kuu
 
Magufuli ameishasema atawalinda na atalinda chama, awrzi kuwa na jipya zaidi ya kuongea kwa mahaba ya kwenda magogoni. Huyu mtu pale watu wanapoitaji suluisho yeye utoa maneno ya kejeli like waogelee.
 
Ukiona watu wanakumisi wakati uliwapa ahadi hewa, Fahamu ni matatizo ya lishe duni utotoni.
 
Back
Top Bottom