Ahadi za Kikwete zafikia Trillion tisini (90 trillion tsh)

Itabidi niwasiliane na university ya St thomas (USA) ili wachukue phd fake waliyompatia Kikwete (take it back).
 
Mdahaloooooo!!! kama kuna neno mkwele halipendi basi ni "mdahalo". Mimi namsifu sana mkwele na chichiem yake kwa kujitambua jinsi wasivyoweza kujieleza na kujenga hoja. hakika wangeaibika sana. kupambanisha Dr. (ya heshima) na Dr. (darasani) ni uonevu kabisa. ndiyo maana hata kwenye kampeni zake maneno anayoweza kuongea ni kuahidi tu, nitajenga barabara, nyumba za walimu, madaraja, vyoo, bafu, bajaji, n.k, n.k. mkwele hawezi kuchambua 'issues'. uliona wapi "halo halo" wanaweza kujieleza. ukimpeleka kwenye stori za kiudaku kapo ndiyo umemleta kwenye uwanja wa nyumbani.

Pipooooooooooooooooooooooooooooooooz .........................
 
Itabidi niwasiliane na university ya St thomas (USA) ili wachukue phd fake waliyompatia Kikwete (take it back).

Inachekesha sana watu wengi maarufu kama The Clintons, Mandela etc. wanazo hizo 'honorary' PhD lakini hutosikia wakijitambulisha ama kutambulishwa Dr........
Tena hao watu maarufu kama akina Clintons hizo honorary PhD zao wamezipata toka ivy league ama elite universities lakini hata siku moja hutosikia Dr Clinton ama Dr Mandela.
Huyo mkwere amepata hiyo honorary PhD toka kwenye vyuo hivyo vidogo vya pembezoni kama St Thomas Univ ndio inakuwa nongwa....eti nae Dr?
Ha ha ha ha.
Mzaramo/mkwere kazi unayo
Ndio yale yale ya waziri wake Dr Aisha Kigoda ambaye hana PhD wala MD degree ila ni Medical Assistant lakini nae ni DR Kigoda ha ha ha ha
 
Wanahela nyingi sana hawa ati..hawajaamua tu. Ila tusiwape kura wasije wakaweka maisha yetu majaribuni
Mbona nasikia tetesi kuwa sasa hivi huko serikalini masuala ya fedha ni mshike mshuike, kuna ukata wa hali ya juu... watu wamezuiwa hata kusafiti kwa sababu hakuna fedha za posho
 
Hii ni kipande nemekinukuu toka hotuba ya Mhe. Mkulo ya Bunge la Bajeti ya 2010/11. Soma katikati ya mistari halafu ujiulize kama hizo ahadi za JK zina ukweli wowote. Bila shaka utangundua kuwa ni uongo na usanii wa mchana kweupe. Kulingana na Bajeti ya Serikali ya Tshs matumizi itawachukua CCM MIAKA ZAIDI ya 10 ijayo kutekeleza ahadi zote!!!!!!!!!!!!!!!!Kweli CCM mnachekesha hata na waliokufa!!!! Kwa ahadi hizi na bajeti inavyoonyesha JK inaitengenezea CCM KIFO CHA MENDE 2010/2015.

In total, the budget revenues will be as
follows:
Tshs. bn
Domestic Revenue..................................... 6,003
Grants and Loans.......................................3,275
Domestic borrowing................................... 1,331
LGA collections..................... ......................173
Domestic borrowing (Roll over) ......................798
Privatisation Proceeds................................... 30
Total Revenue............................................11,610

In meeting the 2009/10 budget,alternative financing sources were explored including borrowing from the domestic financial markets. It was envisaged that recurrent expenditure will be fully funded by domestic revenue. However, the revenue target
was not achieved due to shortfalls in a number of taxes, including the excise duty due to decrease in production of taxable products such as cigarettes, beer and soft drinks. By March 2010 a total of Tshs 424.4 billion worth of bonds were sold in the domestic market.Donor dependency is expected to decline for the upcoming year with a decrease in budgeted revenue from grants and loans to comprise 28% of the total annual budget of 2010/11 (compared to 33% for the 2009/10 budget)

Expenditure
The Government is proposing to
spend Tshs 11,610 billion in 2010/11
as follows:
Tshs bn
Recurrent......................................... 7,791
Development.................................... 3,819
Total Expenditure............................ 11,610

Government expenditure in 2010/2011
will focus on:

• Ensuring that the National elections planned for October 2010 take place as scheduled;
• Improving infrastructure;

• Improving productivity in the agriculture and livestock sectors;

• Increasing access to clean and safe water;

• Strengthening and developing

I like this, very interesting to the future life of Tanzanians
 
huyu mkwere atakuja kutuweka wananchi wake bond cajabu tayari were bond.
P...................po be aware its tme to change now.
 
Heri Mimi Sijasema!

Ahadi za JK zafika trilioni 90/-

na Mwandishi wetu

AHADI zilizokwishatolewa na mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, zimefikia sh trilioni 90, Tanzania Daima Jumatano limejulishwa.

Takwimu hizo ni kwa mujibu wa mchumi mmoja kutoka moja ya mabenki makubwa nchini, ambaye alisema ahadi zote za Kikwete tangu alipoanza kuzitoa hadi sasa thamani yake imefikia zaidi ya sh trilioni 90.

Kwa hali hiyo, duru za kiuchumi zinadai kuwa ahadi za mgombea huyo wa CCM, haziwezi kutekelezeka kwa kipindi cha miaka mitano kama anavyojinadi kwenye mikutano yake ya kampeni.

Kwa mujibu wa mchumi huyo ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, kwa kuwa bajeti ya sasa ya serikali ni sh trilioni saba, ukichukua kwa kiwango hicho bila kujali kupanda au kushuka kwa thmani ya shilingi, Serikali ya Kikwete itahitaji miaka 12 kutimiza ahadi hizo.

"Nimepiga mahesabu ya jumla ya thamani za ahadi alizotoa Kikwete katika kampeni zinazoendelea. Kwa kifupi thamani yake ni sh trilioni 90.

"Kwa kuwa bajeti yetu ni sh trilioni saba kwa sasa, ukichukua kwa kiwango hicho hicho, atahitaji miaka 12 kutimiza hizi ahadi ikiwa bajeti yote itatumika yote kwa ajili ya kutimiza ahadi zake," alisema mchumi huyo.
Mchumi huyo alidai kuwa endapo Rais Kikwete ataamua kutumia 30% ya bajeti kutimiza ahadi zake, ni wazi kwamba atahitahiji si chini ya miaka 45 kutimiza ahadi zake alizozitoa mwaka huu kwenye mikutano yake ya kampeni.

"Nilichokifanya nikuchukua ahadi zake zote zilizonukuliwa kwenye vyombo vya habari. Katika mahesabu yangu ambayo nitawapa nakala, sikutumia kanuni kama Net Present Value or Discounted Cash flow, or err etc," alisisitiza mchumi huyo.

Hadi sasa, Kikwete ambaye yuko kwenye wakati mgumu kutetea kiti chake, ameshatoa zaidi ya ahadi 80 tofauti na wagombea wenzake, Dk. Willbroad Slaa (CHADEMA) na Profesa Ibrahim Lipumba (CUF).

Baadhi ya ahadi hizo ni pamoja na kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya Ziwa-Nzega, Tabora, kujenga barabara za juu katika Mkoa wa Dar es Salaam ili kukabiliana na kero kubwa ya foleni.

Kujenga Machinga Complex mbili kwenye kila wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam, kujenga hospitali katika kila jimbo na kuhakisha tatizo sugu la maji linabaki kuwa historia nchini.

Pia zimo ahadi za kuifanya Wilaya ya Geita kuwa na hadhi ya mkoa ifikikapo Januari mwakani, kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro, kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa, kujenga bandari Kasanga, kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira, kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini, kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi -Dar es Salaam.

Pia aliahidi kuwa Mkoa wa Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria, kulipa madeni ya Chama cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga (SHIRECU), wakulima kuacha kutumia jembe la mkono, kuwapatia trekta wakulima wa kata ya Mrijo, Dodoma, kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera, kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba Mjini, kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma, Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda, mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme.

Nyingine ni kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba, kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali, kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza, kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalumu chenye vifaa vya kupambana na wahalifu, Mwanza.

Kikwete pia ameahidi kumaliza tatizo la maji katika Wilaya ya Same, kuboresha barabara za Igunga –Tabora, kununua vyandarua viwili kwa kila kaya mkoani Mbeya, kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN).

Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami urefu wa kilomita 109, kujenga barabara Musoma hadi Mto wa Mbu Arusha, kuanzisha jimbo la Ulyankulu, mkoani Shinyanga.

Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora, kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini, kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida-Dodoma, kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido, vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji, tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha.

Pia amepanga kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, wilaya ya Musoma, kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido, kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro, kusambaza maji nchi nzima, kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima.

Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha, kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika mkoani Iringa.

Imo pia ahadi ya kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote nchini na kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada.

Kwa upande wake, Dk. Slaa ametoa ahadi 17 hadi sasa ikiwemo kurudisha pesa za ununuzi wa rada, kushughulikia suala la taasisi ya kuweka na kuvuna pesa (DECI), kujenga nchi isiyo na ufisadi, kufufua Tanganyika ili irejee mezani kujadili muungano na Zanzibar, kufufua uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo.

Pia ameahidi kukata asilimia 20 ya mshahara wa rais, kupunguza mishahara ya wabunge kwa asilimia, kuweka Mwenge wa Uhuru Jumba la Makumbusho-Kilimanjaro, kutoa huduma bora za afya na elimu bure. Katika elimu amesema elimu ya awali itakuwa kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita na itakuwa ni lazima kwa kila Mtanzania.

Dk. Slaa pia ameahidi kufuta kodi ya vifaa vya ujenzi, kutoa ruzuku taasisi za kidini, kusambaza magari aina ya shangingi kwa Jeshi la Polisi yatumike kwa ajili kukabiliana na wahalifu, badala ya mawaziri kuyatumia kwa anasa.

Chanzo: Tanzania Daima Jumatano 27 Oktoba, 2010
 
Hapo serikali bado haijafanya matumizi yake ya kawaida(recurrent), kama mishahara, mafuta ya magari etc.
Ni vichekesho na ngoma ya KIDUKU hii!
 
Hii ni kipande nemekinukuu toka hotuba ya Mhe. Mkulo ya Bunge la Bajeti ya 2010/11. Soma katikati ya mistari halafu ujiulize kama hizo ahadi za JK zina ukweli wowote. Bila shaka utangundua kuwa ni uongo na usanii wa mchana kweupe. Kulingana na Bajeti ya Serikali ya Tshs matumizi itawachukua CCM MIAKA ZAIDI ya 10 ijayo kutekeleza ahadi zote!!!!!!!!!!!!!!!!Kweli CCM mnachekesha hata na waliokufa!!!! Kwa ahadi hizi na bajeti inavyoonyesha JK inaitengenezea CCM KIFO CHA MENDE 2010/2015.

In total, the budget revenues will be as
follows:
Tshs. bn
Domestic Revenue..................................... 6,003
Grants and Loans.......................................3,275
Domestic borrowing................................... 1,331
LGA collections..................... ......................173
Domestic borrowing (Roll over) ......................798
Privatisation Proceeds................................... 30
Total Revenue............................................11,610

In meeting the 2009/10 budget,alternative financing sources were explored including borrowing from the domestic financial markets. It was envisaged that recurrent expenditure will be fully funded by domestic revenue. However, the revenue target
was not achieved due to shortfalls in a number of taxes, including the excise duty due to decrease in production of taxable products such as cigarettes, beer and soft drinks. By March 2010 a total of Tshs 424.4 billion worth of bonds were sold in the domestic market.Donor dependency is expected to decline for the upcoming year with a decrease in budgeted revenue from grants and loans to comprise 28% of the total annual budget of 2010/11 (compared to 33% for the 2009/10 budget)

Expenditure
The Government is proposing to
spend Tshs 11,610 billion in 2010/11
as follows:
Tshs bn
Recurrent......................................... 7,791
Development.................................... 3,819
Total Expenditure............................ 11,610

Government expenditure in 2010/2011
will focus on:

• Ensuring that the National elections planned for October 2010 take place as scheduled;
• Improving infrastructure;

• Improving productivity in the agriculture and livestock sectors;

• Increasing access to clean and safe water;

• Strengthening and developing

HII inashanganza mapato na matumizi yanalingana.. yaani lazima tutumie kila senti tunayopata... hatuwezi ku-save? naomba wachumi wanieleweshe
 
Labda atatumia uwezo wa shehe yahya ambaye anampa ulinzi.

Bunge hili lifanye yafuatayo kusaidia utekelezaji wa ahadi za mhe jmk kwa watz 1.Kuandika katiba mpya wadanganyika tupate mgawo wa 50% ya mapato yote ya rasilimali za mji hii 2. Hilo likishindikana watunge sheria inayotupa uwezo wa kisheria kiongozi anayetoa ahadi na kushindwa kuzitekeleza ama makusudi, kwa nia ya kujijengea umaarufu, kujipatia kura au kwa makusudi serikali kukosa ubunifu wa kukusanya mapato sawa na ahadi za mgombea wao au makusanyo kunufaisha baadhi ya watz kiufisadi 3. Mhusika kuachia ngazi mapema baada ya kubaini serikali yake kukosa uwezo wa kutekeleza zilizoahadiwa
 
Back
Top Bottom