Ahadi za JK za trilioni 90 zawasahau wastaafu wa EAC...............

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Nimepitia rundo la ahadi za JK lakini nilishtushwa kujifunza ya kuwa wastaafu wa EAC hawamo kwenye mipango ya CCM ya kuwalipa haki zao za kimsingi za takribani miaka 33 hivi...........

Leo nilikuwa nikiwaangalia wastaafu hao kupitia luninga na nikajionea wazee hao ambao wengi wao ninaamini walikipigia CCM kura kiendelee kubaki madarakani lakini wastaafu hao wao bado wanaendelea kupigwa mchakamchaka mahakamani..............kweli wajinga ndiyo waliwao...................mimi ningelikuwa kwenye kundi hilo la wastaafu yaani kura yangu ningeipeleka upinzani......potelea mbali na lakuwa wacha liwe tu...................

Leo wazee hao shauri lao limetupwa nje na mahakama la kusisitiza hukumu ambayo walishindwa................na hata jaji hayuko tayari kutoa haki kwa visingizio kebekebe...................mojawapo ni kuwa wastaafu hao hawakuzingatia sheria wakati walipoleta madai hayo..........................huu mziki babu zetu watacheza mpaka wakome ubishi wa kukichagua chama cha mafisadi................

Hata kwenye maandiko matakatifu imeandikwa.............Mwenyezi Mungu ameturuhusu tujichagulie viongozi wetu tukiwachagua wabaya kutuongoza tusirudi kumlilia Mwenyezi Mungu kwa sababu hatatusikiliza kutokana na sisi kutumia vibaya madaraka yetu ya kujichagulia viongozi............
 
Back
Top Bottom