Ahadi ya manji kwa yanga

matambo

JF-Expert Member
May 14, 2009
727
117
Wana - Yanga, ahadi hii ya Manji vipi?
ban.blank.jpg


Mwandishi wetu


MEI 15 mwaka huu, magazeti mengi katika kurasa za michezo na burudani yalipambwa na vichwa vya habari visemavyo “Neema yanukia Yanga”, “Njaa sasa imekwisha Yanga”, “Wachezaji Yanga kuuaga umaskini,” pamoja na mengine yaliyoashiria kweli neema hiyo ipo Jangwani.
Wapenzi wengi wa soka nikiwemo; tulifarijika kwa kujua sasa ni wakati wetu kutamba katika soka barani Afrika na dunia kwa ujumla.
Taarifa hiyo ilisema, kuna Kampuni moja ya Japan, yenye maskani yake katika jiji la Tokyo inataka kuingia mkataba wa udhamini na Yanga wa zaidi ya sh bilioni sita za Tanzania kwa muda wa miaka mitano ambapo Yanga itakuwa ikipata wastani wa sh bilioni 1.3 kwa mwaka.
Fedha hizo ni nyingi ikilinganishwa na mikataba yote iliyoipata Yanga toka kuumbwa kwa dunia hii.
Mazungumzo hayo yalikuwa baina ya Kampuni ya Japanese Multinational na Mfadhili Mkuu wa Klabu ya Yanga Yussuf Manji.
Manji aliahidi kwa kusema Yanga sasa imepata neema na viongozi wawili wa Yanga wataenda Japan kukamilisha zoezi hilo haraka iwezekanavyo.
Manji aliwataja watakaokwenda huko kuwa ni Mwenyekiti wa Yanga kwa wakati ule Iman Madega na Katibu Mkuu wa Yanga Afrika Lawrence Mwalusako wakiongozana na Manji mwenyewe.
Lakini hadi leo nabaki nimeduwaa sielewi nini kilichokwamisha zoezi hilo la utajiri kuanguka pale Jangwani, huku Mfadhili Manji akiwa kimya kama vile kamwagiwa maji, kapoa kabisa.
Najiuliza ni kitu gani kilichojificha nyuma ya pazia kwa Manji hadi akae kimya kiasi hicho. Au zoezi zima la uchaguzi lililomweka madarakani Mwenyekiti wa sasa Lloyd Nchunga na wenzake ndio limesababisha yote hayo?
Wapenzi na wanachama wa Yanga mumemuuzi nini Mfadhili huyo hadi asitishe zoezi hilo tamu kabisa katika maisha ya mpenda maendeleo yeyote wa soka? Hususani wapenzi na wanachama wa Yanga.
Leo ni mara ya pili kuandika makala za Manji kuhusu kuonesha mambo muhimu na mazito aliyofanya ndani ya Klabu ya Yanga kwani angalau ameweza kuifanya kuwa bora kiuchumi na kikubwa ameleta utulivu na amani jambo ambalo kwa kipindi fulani lilikuwa adimu.
Nimekuwa nikifuatilia udhamini wa Manji toka alipoibuka Yanga Juni 2006; na amekuwa msaada kwa wachezaji kwa kutoa pesa kwa wachezaji ikiwa ni njia ya kuwahamasisha ili timu ipate ushindi na hii iliongeza hamasa kwa wachezaji kujituma na wengine kuipenda timu tofauti na hapo nyuma kidogo.
Mbali ya misaada hiyo kwa wachezaji nani asiyejua kuwa Manji ndiye aliyejitoa kwa hali na mali kuyavunja makundi makubwa ndani ya yanga ya Yanga asili, Yanga kampuni na Yanga Akademi, licha ya mgogoro ule kusuluhishwa kwa njia za kisheria yaani mahakama, ilishindikani kutokana na misimamo mikali ya makundi hayo.
Kwa kuwakumbusha tu kundi la kampuni ambalo ndio lilikuwa madarakani lilikuwa linaongozwa na Francis Mponjori Kifukwe, kundi la Yanga asili lilikuwa linaongozwa na Yussuf Mzimba huku kundi la Yanga Academ lilikuwa chini ya Constantine Kibo Merinyo, Manji alifanya juhudi kubwa.
Manji mbali ya hayo amefanya jambo la kihistoria ambalo kamwe hatasahaulika la kukara bati jengo la Makao Makuu ya Klabu hiyo yaliyopo Makutano ya Twiga na Jangwani, kariakoo jijini Dar es Salaam.
Jengo hilo ambalo kwa miaka mingi lilikosa ile hadhi yake kutokana na kuharibika kwa miundombinu, sasa lipo katika hali nzuri hadi kufikia timu kuweka kambi hapo katika hilo nakupa Bravo Manji.
Manji vilevile kupitia kampuni yake ya Quality Group ameendelea kuhakikisha kuwa wachezaji wa Yanga wanapata mishahara yao vizuri na pia wanakula vizuri na kulala vizuri.
Lakini kila nikiamka nafungua radio, televisheni na kusoma magazeti sioni ni lini Kampuni hiyo Japaness Multinational itaanza mkataba wake.
Ni lini Mwalusako na Nchunga wataenda huko Japan? Ni lini Yanga watavuna hayo mamilioni na kuondokana na suala la ombaomba na kutokuwa na uhakika wa kumlipa kocha Papic au wachezaji?
Ni lini Manji utavunja ukimya kuhusu hili? Mbona uko kimya… tunabaki tumeduwaa tunajiuliza ni Manji huyu huyu aliyewaita kwa makeke mno waandishi wa habari Mei 14 2010 na kuwathibitishia kuwa Yanga kesho watakuwa na uwezo mkubwa.
Manji; Ni kweli Watanzania tulio wengi ni wepesi wa kusahau lakini tupo wengine maneno matamu kama yale hatuyasahau kamwe,.
Najiuliza mambo yote uliyoyafanya huko nyuma ni mfano wa kuigwa na ni vema hata hili la udhamini wa Japan usiliache hewani, watu wanajiuliza maswali mengi kuwa huenda ukufurahishwa na uongozi uliopo au suala hilo lilikuwa ni la Imani Madega lakini yote kwa yote Manji wana Yanga wanakutegemea na katika suala hilo usilaze damu midhali umeshalitamka kwa kichwa chako mwenyewe ni vema ukalitekeleza na kama likishindikana julisha umma kwa njia ile ile ya awali.
Katika moja ya makala zangu niliwahi kusema kwa mpango huu wa Manji kuitafutia Yanga udhamini utaoifanya kupata zaidi ya sh bilioni moja kwa mwaka hakuna tofauti na wale wazee wetu waliotangulia mbele ya haki kama Kondo Kipwata na Tabu Mangala waliojitolea kwa hali na mali kuhakikisha wanatuachia majengo ambayo hadi leo yapo.
Yanga inataka nini tena kama kweli mpango huu utafanikiwa, itakuwa ni neema kwa Klabu hiyo kwani itafanya ijiendeshe kiuhakika kwa maana ya kifedha.
Hii itawafanya hata viongozi wa Klabu hiyo kuongoza kwa urahisi lakini kipato kitakachotikana ni vema wakakitumia vizuri kwa ajili ya kujenga mazingira mazuri ya kujitegemea na kuanzisha vitega uchumi. Ni wakati sasa wa Uongozi wa Yanga unaongozwa na Nchunga na Wasaidizi wako David Mosha, Tito, Mzee wa Alamba Yussuf, Mtaalam wangu Ally Mayai Tembele na wengineo kusogea karibu na Manji na kuufuatilia mkataba huo wa Japan.

Lakini wakati huohuo ni vema mkahaha huku na kule kusaka udhamini kama huo. Ondokaneni na fikra mgando za kutegemea mapato ya milangoni ili mlipe posho kwa wachezaji wenu na matumizi mengine.
Hii ni ya 21; hivyo mawazo ya namna hiyo yamepitwa na wakati.
Huu ni wakati wa kujipanga vizuri ili msiendelee kupewa samaki kila siku bali tafuteni nyavu mvue wenyewe.
Wanachama wenu walikesha saa 24 wakiwapigia kura ni kazi kwenu sasa kuwaonesha imani yao kwenu kwa kufanya vitu vya karne ya 21 na si vinginevyo.
Makala hii ni mahususi kwa Manji kila kitu kitapita lakini maneno yako hayatapita kamwe tunausubiri huo udhamini wa Japan kwa hamu. Wanayanga leo wamebaki wanatahayari wanajiuliza mambo mengi na kwamba hawaridhiki na mwenendo mzima wa timu yao. Mkataba na Kocha Mserbia Kostadin Papic nao umeisha Oktoba 15 na mlipaji mwenyewe ndio Manji, mfadhili mwenyewe yuko kimya, ni hatari kweli kweli.


h.sep3.gif

Mwandishi wa makala hii ni Kocha na Mfanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi Bandari; Kitengo cha Uhandisi 0713243711
kennymwaisabula@yahoo.com
 
Hii ndo hatari ya kuwa tegemezi, viongozi wanatakiwa wae creative badala ya kutegemea fadhila za mtu mmoja, maana akikasirika tu basi, fikiria juu ya sakata la mkataba wa papic kwa sasa mbali ya malalamiko ya mishahara kwa wachezaji wa yangama mara kwa mara

viongozi badilikeni muwe wabunifu!!!!!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom