Ahadi ya katiba mpya Jk ameamua kung'atuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ahadi ya katiba mpya Jk ameamua kung'atuka

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Gsana, Jan 3, 2011.

 1. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Salaam Jf, tangu jk atoe ahadi ya katiba mpya, nimeanza kukumbuka sana tukio lilitokea zama zilizopita ktk maisha ya kijijini kwetu. Wawindaji 2 walienda kuwinda msitu wa mbali na bahati mbaya walipata sungura peke ake na mbwa aliemkata alikuwa mbwa wa mzee,mzee alimchinja sungura na kumla, akimnyima kijana aliyekuwa naye eti mbwa wake halifanya uzembe. Siku ya nne mwituni njaa ikakaza na mzee kuanza kulia,kijana akamshauri mzee kuwa ili aishi,avue viatu vyake vilivokuwa kama vya maasai yan vpande vya tairi za gari na kukata vipande vidogo na kuvimeza! Mzee akaukwaa ushauri na kula viatu vyote, Mzee alijikokota mpaka kijijini ila maisha yake yakaishia hapo maana tumbo lilivimba na kupasuka kwa viatu alivomeza! Kijana kamumaliza mzee yule kwa ujanja! Sasa naogopa,aliyemtega Jk viatu hivi ni nani?? Akivila itakuwaje!? Baada ya stori hii, leo nahoji uhamuzi wa Jeykey kutoa ahadi ya katiba mpya ndani ya siku 70 za utawala wake kama alivohaidi dr.Slaa kutupa katiba mpya ndani ya siku 100,ama kweli akili za kuambiwa changanya na zako,ila ------ hajazchanganya,ametoa ndo maana siku zimepungua toka 100 za dr.SLAA kuja less 70. Ni tafsiri yangu tu,ila mimi nilitaka Great Thinkers wajadili kama ------ akiamua japo kwa kusoma nyakati kutoa ahadi ya katiba mpya,ambayo pia iko NJE ya ilani ya Ccm si kama kujistaafisha mwenyewe?! Nasema ivi kwa sababu naamini mchakato wa kujenga katiba mpya hakuwezi kuchukua miaka 5 , je ikipatikana mwaka 2012-2013 si itaanza kutumika?na je ikianza kazi si itabidi kila ibara yake ifuatwe?na zikifuatwa si itaruhusu kuhoji utapeli uliofanya ktk kujumlisha kura mwaka 2010?au the past shall be exclusive?! Hapa binafsi naona jk kakubali kwenda Msoga kupumzika endapo kipengele icho kitatambulika mapema,ikumbukwe kuwa bado chadema wanaandaa ushaidi na haijulikani itawachukua muda gani,ambapo wanaweza kuukamilisha siku moja baada ya kupata katiba mpya na kuupeleka Mahakamani hapo ndipo Jk anaweza kujifunga bao mwenyewe au akapigwa goli la kisigino hadharani. Pia itapelekea Viongozi Waandamizi wakiwemo wastaafu kufikishwa mbele ya pilato. Tusichukulie mambo simple simple,yanaweza kutokea na hapo ndo anaweza akapitikana Rais wa wananchi baada ya katiba mpya. Haya matukio si ili mradi wataalam wameshagutuka,------ anataka kusign mwenyewe kuwa sheria mama imtafune mwenyewe na hapo ndo ukweli utajulikana kuwa wananchi walipiga kura. Ktk ili na mengine mengi yatakayojiri, mi kwa maoni yangu,JK HAS DECIDED TO Sow the seed for his own destruction. Hapa hata jk ataelewa kuwa "Haki hainyimwi ila ucheleweshwa tu" ,lets wait n see. I stand 2wait corrections! Nawasilisha!
   
 2. quimby_joey

  quimby_joey JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 361
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  mkuu ungetumia paragraph topic ingevutia zaidi watu kuisoma na kuchangia, fanya editing if possible...
   
 3. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Powa mkuu ila leo nko kijijini situmii komputa ndo tatizo ila ntajitahidi soon.
   
 4. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  No! JK hapa anayo nafasi ya kuenziwa. Kwa kukubali kuandikwa Katiba mpya haina maana kwamba itamgeukia hata yeye mwenyewe. Uamuzi aliouchukuwa kama ni wa kwelikweli ni wa usanii wenye tija kwake. Waliopita watahukumiwa kwa taratibu zilizokuwapo kwa wakati wao, ukisema katiba mpya itumike kuwahoji hata waliopita unamaanisha hata mifupa ya mwalimu JKN ifukuliwe na kusimamishwa mahakamani kwa maamuzi aliyoyafanya na ambayo hata yeye alikujayaona akiwa amekaa pembeni na kuyatubia hata kwa machozi.

  Ikumbukwe kuna mambo mengine ni matokeo ya washauri wabaya, maana uraisi sio mtu bali ni taasisi.Hata wewe kama mwananchi unayo mengi ya kuhukumiwa kama tukiifuata katiba mpya ikufukue hata wewe ulikojichimbia. Katiba mpya haiandikwi ili kujilipiza kisasi bali kujiimarisha kama nchi katika taratibu ambazo tutalazimika kuzifuata baada ya kukubaliana. JK kawazidi kete waliomtangulia kama kweli anakubali katiba iandikwe upya. Haina maana kwamba mambo yaliyomo kwenye katiba ya sasa yote ni mabaya, bali yatakuwa msingi na kioo cha kujua wapi tulikuwa fyongo na tunaandika mpya kwa kujirekebisha na tusahau ya kale na kuganga yaliyopo na yajayo. Vigogo wengine, sikatai kwamba wanapokataa katiba mpya wana wasiwasi kwamba hiyo katiba mpya huenda itawarudi, hayo ni kusutwa kwa dhamira zao kwa uozo wao uliopita, lakini uozo wao ndio msaada wa kuandikwa kwa katiba mpya ambayo itaandikwa ili kudhibiti mianya ya kikatiba iliyotumiwa na hao kujinufaisha pasipo mtu kuruhusiwa kuwauliza.

  Bravo JK kwa hapo, lakini kwa kuwa katiba ya sasa inamzuia JK kurudi tena madarakani mara ya tatu na siamini katiba mpya itamruhusu, basi yeye yuko salama, ni kimojawapo kitakachomsababisha JK akumbukwe na historia ya nchi hii kwa miaka mingi ijayo kama Gobavhev wa Tanzania, W. de Clark wa Tanzania. CCM sasa wasome maandiko ukutani maana katiba iliyowaruhusu kufanya chochote kwa kiburi sasa kinaishia ukingoni. Ndio maana kina Makamba et al. wanahaha.

  Tukiuweka ushabiki pembani, kunyamaza kwa JK wakati wasaidizi wake wanaropoka mchana kweupe kupinga madai ya wananchi tena wakitukana kwamba wananchi wanadodai katiba mpya ni mabata na wahaini, yeye kuibuka na kuungana na waajiri wake (wananchi) ina maana kubwa kwamba amewaumbua wanafiki wake waliofikiri atawaenzi kwa kuropoka kwao. Hata kina Dowans japo hakuwasemea katika kuukaribisha mwaka mpya inamaanisha ni mlolongo wa ubovu wa katiba tuliyo nayo ambao ikiandikwa upya Dowans na Richmonds wengine hawaji tena kirahisi, kwa sababu mikataba yote italazimika kuanikwa wazi kwa wananchi kabla ya kusainiwa, hata kama ni kupitia wawakilishi wao - wabunge. Labda tuchague wabunge wasio na kitu vichwani au waganga njaa. Anayekutesa anakukomaza akili usilalelale.

  Ila najiuliza swali la CCM kuhodhi mali zote zilizotafutwa na watanzania wote wakati wa chama kimoja ambazo sasa wao wanadai ni vyao peke yao kama paka na mnofu. Je, katiba mpya itarudisha mali hizo serikalini isiwe ya chama kwa vile watu wote walizifanya kuwapo mali hizo? Hiyo ingefaa sana ili mchezo wa siasa uwe wa haki sawa kwa vyama vyote, sio mmoja Tyson na mwingine Nchumali wapambane uwanja mmoja wakati hata uwanja na marefa ni mali ya Tyson.
   
 5. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
   
 6. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #6
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
   
Loading...