Ahadi ya Kansela Angel Merkel kujenga kiwanda kikubwa cha mbolea Tanzania ilikuwa ni uongo?

chase amante

JF-Expert Member
Feb 24, 2018
5,553
2,073
Mnamo mwaka 2019, Kansela wa Ujerumani alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na hayati Rais Magufuli na kumuahidi kujenga kiwanda kikubwa cha mbolea kuliko vyote Afrika hapa nchini.

Ningependa kujua, kama kimejengwa au kipo katika hatua ya ujenzi.

Kwa mwenye taarifa, naomba anijuze.

Ahsante
 
Mnamo mwaka 2019,kansela wa ujerumani alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na hayati rais magufuli na kumuahidi kujenga kiwanda kikubwa cha mbolea kuliko vyote afrika hapa nchini.

Ningependa kujua, kama kimejengwa au kipo katika hatua ya ujenzi.

Kwa mwenye taarifa, naomba anijuze.
🤣🤣🤣Hahaha! Yaani uliamini zile hekaya na propaganda za Kurugenzi ya Habari? Mbona mie wakati huo huo nili post thread nimeiweka hapo chini kwamba Markel hawezi kutoa ahadi ya vitu ambavyo utekelezaji wake ni wa private sector na vitafanyika wakati hayupo madarakani? Ule ulikuwa ni uongo kuna issue walikuwa wanajaribu kufunika ndio wakasema Magufuli kapigiwa simu na Merkel.

Kama si hivyo walifanyiwa prank call na kwa kutokuwa na busara wakaamini ni Merkel! Wanakurupuka sana hawa watu hadi wanatia aibu. Who was Magufuli hadi apigiwe simu na Merkel?

Mnamo mwaka 2019,kansela wa ujerumani alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na hayati rais magufuli na kumuahidi kujenga kiwanda kikubwa cha mbolea kuliko vyote afrika hapa nchini.

Ningependa kujua, kama kimejengwa au kipo katika hatua ya ujenzi.

Kwa mwenye taarifa, naomba anijuze.

Ahsante
Ukiwaza hayo nami nakuongezea je uwanja wa mpira Dodoma umeshaanzwa kujengwa?
 
Ukiwaza hayo nami nakuongezea je uwanja wa mpira Dodoma umeshaanzwa kujengwa?

..Wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Hailemariam Desalegn serikali ilidai Ethiopia wataanza kutumia bandari ya Dsm kupitisha mizigo yao.
 
Mnamo mwaka 2019,kansela wa ujerumani alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na hayati rais magufuli na kumuahidi kujenga kiwanda kikubwa cha mbolea kuliko vyote afrika hapa nchini.

Ningependa kujua, kama kimejengwa au kipo katika hatua ya ujenzi.

Kwa mwenye taarifa, naomba anijuze.

Ahsante
Kingejengwa si ungejua, sasa unataka ujuzwe kitu gani!

Na hata hivyo taarifa yako si sahihi.

Mipango ya ujenzi wa kiwanda hicho cha mbolea na kampuni ya ujerumani haikuwa ahadi ya Anjela. Mpango huo ulikuwepo tokea zamani hata kabla ya Magufuli.

Kwa nini hakijajengwa hadi leo, hilo ni jambo ambalo sote tunependa kujua sababu zake ni nini.
 
Back
Top Bottom