Ahadi ya JK kwa vijana yashtukiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ahadi ya JK kwa vijana yashtukiwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Nov 18, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 18, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,701
  Likes Received: 82,626
  Trophy Points: 280
  Ahadi ya JK kwa vijana yashtukiwa Wednesday, 18 November 2009 08:23 *Ni ile ya kuwateua kuwa mawaziri 2010
  *Lipumba asema ni kampeni, haiaminiki
  *Nape: Suala si ujana bali uwezo, uzalendo

  Na Reuben Kagaruki
  Majira

  MPANGO wa Rais Jakaya Kikwete kuwa endapo atachaguliwa tena kuwa rais mwakani atateua mawaziri vijana umeshutukiwa na kuelezwa kuwa analenga kuwasogeza karibu ili wamuunge mkono katika uchaguzi wa mwaka 2010.

  "Hiyo ni kampeni, kwenye siasa tunasema anawakonyeza vijana ili wamuunge mkono katika uchaguzi mkuu, lakini ukweli ni kwamba Rais Kikwete haaminiki, hawezi kusema kitu tukakiamini," Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba.

  Alisema Rais Kikwete anafahamu kuwa katika uchaguzi ujao anahitaji kuungwa mkono na vijana, ndiyo maana ametafuta mbinu ya kuwavuta karibu kwa ahadi ya kuwapa uongozi.

  Akitoa mfano jinsi Rais Kikwete asivyotekeleza ahadi zake, Profesa Lipumba alisema mwaka 2005 aliahidi ajira za vijana na kuongeza mapambano dhidi ya ufisadi, mambo ambayo alidai ameshindwa kuyatekeleza.
  "Anawakonyeza vijana ili wawe na matumaini kuwa watapata uongozi, alitakiwa kuonesha ni jinsi gani amewaandaa mapema kushika nafasi hizo," alisema.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa TPP-Maendeleo, Bw. Peter Mziray, alisema ahadi ya Rais Kikwete ya kuwapatia vijana uongozi hawezi kuitekeleza kwa kuwa na wenyewe wameishajifunza ufisadi wakiwa ndani ya CCM.

  "Hao vijana atawapata wapi? Ndani ya chama hicho (CCM) vijana wanajifunza ufisadi, wengine wana digrii zenye matatizo sasa hao atakaowapa madaraka atawapataje?" alihoji Bw. Mziray.

  Alisema kama ana mpango huo basi hata yeye aachie nafasi yake ya urais hawaachie vijana kwani amekuwa ndani ya serikali tangu awamu ya kwanza.

  "Tangu awamu ya kwanza alikuwa kiongozi, ikafuata awamu ya pili na ya tatu vipindi vyote akawa waziri, leo hii ni rais, ana jipya gani?" aliuliza Bw. Mziray.

  Bw. Mziray alisema anachoweza kufanya Rais Kikwete ni kuongeza idadi ya wanawake katika safu ya uongozi ili kuleta uwiano.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), Bw. Augustino Mrema alisema kauli ya Rais Kikwete ni ya kuhamasisha vijana waunge mkono serikali yake. "Anawapa matumaini ili waishi kwa imani na tumaini jipya," alisema.

  Wakati wanasiasa hao wakibeza mpango huo wa Rais Kikwete, Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umepokea mpango huo kwa kicheko kwamba umedhihirisha jinsi alivyo na imani nao.

  Katibu Mkuu wa UVCCM, Bw, Martin Shigela alisema Rais Kikwete anajua uwezo wa vijana, hivyo kauli yake hiyo inatoa matumaini makubwa kwao.

  "Rais anajua alikuwa kiongozi wa vijana, anaelewa vijana wana uwezo na elimu ya kutosha, wanaweza kuongoza bila matatizo yoyote," alisema na kuongeza;

  "Tunapenda kuwa na uhakika wa taifa la kesho, uhakika huo utapatikana kwa kuongeza vijana katika safu ya uongozi," alisema. Alisema vijana hawana mashaka na mpango huo wa Rais Kikwete.

  Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), Bw. Nape Nnauye, alisema mpango huo wa rais ni mzuri na amekuwa nao tangu alipoingia madarakani lakini hoja si idadi ya vijana bali vijana wenye uwezo na uzalendo wa kweli kwa maneno na matendo yao.

  "Tangu aingie madarakani mtazamo wake umekuwa wa aina hiyo, hivyo alichosema ni ahadi kuwa atafanya zaidi. Anadi ni nzuri kama itatekelezwa kwani vijana wana haki ya kutoa mchango wao kwa maendeleo ya nchi yao leo na kesho wasiache mpaka wamechoka ndo waanze kupewa dhamana," alisema Bw. Nnauye.

  Naye Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi wa UVCCM, Bi. Esther Bulaya, alisema mpango huo wa rais utaondoa dhana iliyojengeka kuwa maisha ni ndani ya siasa baada ya kustaafu.

  Akizungumza na vijana wa nchi kadhaa za Afrika, Rais Kikwete alisema;

  "Wale viongozi wa rika langu, lazima waanze kuwaachia nafasi vijana, tunahitaji wakuu wa wilaya vijana zaidi, wakuu wa mikoa vijana zaidi na hata mawaziri vijana zaidi. Ndivyo ilivyotokea kwetu tulipokuwa vijana."
   
 2. P

  Prior Master Member

  #2
  Nov 18, 2009
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  All ministers wawe below retirement age, below 60, kama mtu kastaafu utumishi wa umma kama say mwalimu au katibu mkuu hiyo nguzu ya kukimbizana na taasisi kubwa kama wizara au ikuku inarejuvenate wapi?
   
 3. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #3
  Nov 18, 2009
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Hii yawezekana ni campaign gimmick.

  Kuanzia sasa mtasikia sana kuhusu VIJANA (na WANAWAKE) kwa kuwa mwaka wa uchaguzi unakuja. wanasiasa akina Kikwete wanataka kuwapa matumaini ili wapate kura.

  Suala muhimu hapa SI UMRI, ila ni kuchagua/kuteua viongozi WENYE UWEZO wa kuchapa kazi, WAPENDA NCHI, WASIO MAFISADI wala kuwa WAPAMBE WA MAFISADI.

  I'm doubtful.
  After Lowassa's resignation, Kikwete announced the new cabinet in which he gave important Cabinet posts to 'wanamtandao'. Sofia Simba (sic!) akapata post yenye ofisi Ikulu kabsaaaaa.

  Remember, suala NI UWEZO, SI UJANA.
   
Loading...