Ahadi ya Gadaffi kuwapatia nyumba wakazi wa Kilosa imekuwa Ahadi ya CCM uchaguzi 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ahadi ya Gadaffi kuwapatia nyumba wakazi wa Kilosa imekuwa Ahadi ya CCM uchaguzi 2010

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by bagamoyo, Sep 6, 2010.

 1. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,528
  Likes Received: 2,110
  Trophy Points: 280


  Mh. Raisi J.M Kikwete ametoa ahadi kuwajengea nyumba wakazi waliokumbwa na mafuriko wilayani Kilosa ktk kampeni yake ya uchaguzi. Pia itakumbukwa kuwa Kiongozi wa Libya alitoa ahadi kama hiyo, ila CCM hawajaeleza kama ile ahadi ya Kiongozi wa Libya itakuwa siyo ahadi inayobebwa na CCM wakati huu wa kampeni.

  Tujikumbushe: Januari 2010
  [​IMG]
  Katika hatua nyingine Raisi Muammar Gaddafi wa Libya ametoa misaada mbalimbali kwa waathirika wa mafuriko Kilosa pamoja na kuahidi kujenga Nyumba 200 zenye thamani ya Shillingi Billioni 1.5 kwa ajili ya waathirika hao. Du jamaa kweli ana moyo wa huruma !

  [​IMG]
  Kiongozi wa Libya Kanali Gadaffi (kulia) na Waziri Mkuu wa Italia (kushoto) Belsconi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ajabu ya uyu jamaa ni kuwa na walinzi wanawake tu.
   
 3. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hamna lolote hapo. Hiyo hela ndogo sana Mwana wane. Nyumba ya Gavana wa BoT ilikuwa ya kiasi gani vile???!!!!
   
 4. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Makubwa, mwaka huu tutakoma kwa ahadi
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Sep 6, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mkuu, hii haimo katika mada inayozungumzwa hapa.
   
 6. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,424
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Hapana zinatosha kabisa, ni Shs 7.500.000 kwa kila nyumba, kama watajenga mira mraba 50 kwa kila nyumba yaani vyumba vitatu, sebule na sehemu ya stoo bila choo, wakafanya matofali na kupiga plaster na rangi tu, sakafu ya kawaida(screed) na bati G 28, inatosha sana! Itakuwa kwa kila mita moja wamejenga kwa Tshs 150,000 ambazo ni nadra sana kwa wale wanaofidiwa wanapovunjiwa kuzipata, INAWEZEKANA.

  Sasa isije ikawa Kikwete anataka kudandia hii!
   
 7. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #7
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mitanzania kila siku inasaidiwa na Gaddafi, halafu humu ndani ya JF kuna baazi ya mitanzania how come they dare wanamtukanaga Bwana Gadafi, mimi hupatwa na uchungu sana.........Mitanzania ya aina hii haifai kabisa ktk jamii ya watu wastaarabu, inatilisha aibu sana....SHENZ TYPE!!!!!!!!!!!
   
 8. Bakari Maligwa

  Bakari Maligwa Member

  #8
  Sep 6, 2010
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ...Mwanzo nilidhani Wabongo hawafuatilii mambo..sasa nafarijika kwamba watu wa Tanzania wanafuatilia mambo nyeti ya uongozi wa nchi yetu. Gaddaf alitoa ahadi ya kuwajengea nyumba wahanga wa mafuriko ya Kilosa kama msaada wa kiutu na au kibinadamu. JK na CCM baada ya kuona kwamba wamewatelekeza watu wa Kilosa akaona ni afadhali atumie fursa ya kuwapa ahadi "mpya" juu ya ujenzi wa nyumba za kuishi kwa fedha ya "ahadi" kutoka kwa Gaddaf.

  Kama kawaida ya wapiga-siasa wa CCM, ahadi ndiyo mtaji pekee unaoweza kuwarubuni wasiyo na ufahamu wa jinsi ahadi zinavyotolewa na au zinavyotekelezwa. Huu ni wakati wa uchaguzi na upigaji wa siasa hutegema jinsi mpiga-siasa anavyoweza kutumia ujanjaujanja wa kuwalaghai na au kuwarubuni wapigakura na hatimaye kujizolea kura kibao kuelekea ushindi wa kishindo! CCM na viongozi wake wameshachukuwa mtindo uleule uliyokuwa unatumia kwenye hadithi ya "Wajinga ndio waliwao" na au "Ujanja wa Abunuwas" kujenga nyumba hewani.

  Ahadi ya ujenzi wa nyumba Kilosa ni ahadi zilezile za ununuzi wa meli kubwa (Ziwa Victoria) na ujenzi wa kiwanja cha ndege cha kimataifa Kigoma! Imetoka hiyo na ikirudi...JK atakuwa ameanguka mara 100 na ziadi..Kazi kwenu wapigakura wa Kilosa...chukuweni muweke kwa CCM mambo yawe "waaaaa" kwao na nyinyi mtabaki kwenye mahema hadi Adolf Hitler atakaporudi Ujerumani na Karl Peters kutembelea Msowero ya Sultan Magungo!!!
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  Sep 6, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sasa kama akituhonga na vijisenti (TSh 1.5bn) ili apate sapoti kwenye issue zinazohusu Waarabu, akiboronga tumkodolee macho tu?
   
 10. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #10
  Sep 6, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  CCM kwa kudandia
   
 11. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #11
  Sep 6, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145

  Ulitarajia miujiza gani?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. P

  Percival JF-Expert Member

  #12
  Sep 7, 2010
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 2,567
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  long live Ghadafi - the true son of Africa. Liberating and uniting Africa has been his lifelong goal. show me who else has helped other fellow Africans and devoted his time for good of Africans than him. He backed his words with with wealth of his country for the sake of Africa. Who else was pouring millions for liberation of African states under colonialism if not Ghadafi ?

  And yet there are many ungrateful Africans who never recognise his contribution - Fadhila ya punda ni mashuzi na mateke.
   
Loading...