Ahadi ya CCM daraja la Kigamboni na Hatari ya Kupoteza Maisha sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ahadi ya CCM daraja la Kigamboni na Hatari ya Kupoteza Maisha sasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gurudumu, Feb 3, 2011.

 1. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0

  Attached Files:

 2. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ....ni hatari kubwa sana kuwa na viongozi waliojawa na maneno, wasiojali maslahi ya watu na maisha ya watu wao kwa ujumla!
   
 3. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  cha ajabu ni kwamba hata hakuna urgency kutengeneza hilo lililoharibika, kama unavyoona kwenye picha.
   
 4. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2011
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Acheni upuuzi. NSSF inajenga daraja beginning in the next 2 months.
   
 5. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  unamaanisha nini mkuu? wananchi waache upuuzi wa kukerwa na jinsi serikali inahatarisha maisha yao? Au ccm iache upuuzi wa kuahidi daraja tangu 2000, hata baada ya kupewa pesa za kujenga daraja na ubalozi wa Uholanzi? Au NSSF iache upuuzi wa kuahidi kujenga daraja tangu 2007? Naomba unifafanulie mkuu wangu
   
 6. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #6
  Feb 4, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Wafanya biashara wa Kigamboni wamelalamika kwamba tatizo la kivuko limewatia hasara. Wanashindwa kupata bidhaa za biashara zao na pia bidhaa zingine kama samaki zimeharibika. Ni tatizo siyo tu kwa wasafiri wa kawaida bali kwa uchumi binafsi.
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Feb 4, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Silly you... you cant take a mickey out of people's life... unatia kinyaa ana kuleta utani kwenye hili la maisha ya watanzania
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Feb 4, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Daraja kigamboni ni mfano hai sana wa jinsi wakubwa wetu wanavyogeuza maisha ya watu kama mafaili... once they are in their offices, they open files read and put back to the shelves

  Mimi binafsi nimeshawahi kufuatilia hili tangu 2005 na nilifikia hadi kuona draft contract kati ya NSSF na wale jamaa wa Netherland. kama kawa serikali ya Kikwete kwa kushirikiana na maswahiba wetu NSSF chini ya Dau na Binamu yangu mmoja, waoo waliona yote haya ni mafaili tu

  Nothing has been done zaidi ya kujilimnikizia maeneo kuanzia mjimwe, geza, mwongozo, mbutu, hadi pemba mnazi.... NSSF guys dont invest kama hakuna personal gains, i mean personal gains kwao individuals and not wananchi wa kawaida

  Naiomba serikali ifikirie sana, IWAPO UNASHINDWA KWENDA MITA MIA TATU KUTOKA IKULU, HALI IKOJE HUKO SUMBAWANGA>???

  wizara ya magufuli ichukue mradi ijenge yenyewe na nssf wabaki wakimuosha manji miguu

  TUMECHOKA SASA, na huyo mbuge ndio kiazi kabisa, zaidi ya kutembea upande-upande na kujipendekeza hana jipya
   
 9. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #9
  Feb 4, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ujenzi wa daraja la Kigamboni uko kwenye Ilani za Uchaguzi za CCM za mwaka 2000 na mwaka 2005. Sina nakala ya Ilani ya 2000 lakini ukirejea ukurasa wa 54 wa Ilani ya 2005 utaona hii ahadi. Lakini Hansard ya Bunge ya tarehe 3 Agosti 2007 inawakumbusha Wabunge na Watanzania kwamba ahadi ya ujenzi wa daraja hili ilikuwepo hata kabla ya Ilani ya 2000. Bahati mbaya Mbunge aliyetamka haya maneno hakutaja mwaka hasa ambao ahadi hii ilianzishwa na CCM.

  Hansard mbali mbali za 2006 na 2007 zinaonesha Wabunge, hasa wa Dar es Salaam (Zungu na Msomi) wakiulizia maendeleo ya ujenzi huu mara kwa mara. Kila mara wanajibiwa majibu ambayo hasa hayana mshiko.

  Lakini tarehe 3 Agosti 2007 Wabunge hawa wakiungwa mkono na wenzao wengi walitia pressure kubwa na serikali ililazimika kujibu kikamilifu.

  Kwamba NSSF ilianza upembuzi yakinifu 2003 uliogarimu dola za kimarekani 20,000, ambazo zililipwa kwa Howard Humfrey. Mwaka 2004 wakafanya upembuzi wa kina kwa garama ya dola 230,000. Kisha serikali ikasema kwa kuwa CCM imeliweka daraja hili tena kwenye Ilani yake ya 2005, basi ni lazima litajengwa na mchakato umefika mahali pazuri.

  Awali Hansard ya 1 Agosti 2007, Waziri wa Kazi Ajira na Maendeleo ya Vijana alijibu swali Bungeni kwamba daraja litajengwa kwa sababu tayari Waraka wa Baraza la Mawaziri umeshatayarishwa. Kwamba waraka huo umeshapita kwenye ngazi ya Sekretariati ya Baraza la Mawaziri. Kinachosubiriwa ni Waraka huo ufike kwenye Baraza la Mawaziri na ambalo kama likiridhika litamshauri Rais aagize kuanza ujenzi wa daraja hilo la Kigambani. Waziri alisisitiza kwamba daraja hili litajengwa kabla ya 2010, kama ilivyoahidiwa kwenye Ilani ya CCM ya 2005.

  Mheshimiwa Zungu aliibana serikali zaidi ieleze gharama za hili daraja na kama ni kitu ambacho serikali kweli imeshindwa kujenga. Alijibiwa tarehe 3 Agosti 2007 kwamba garama za kujenga daraja la Kigamboni ni Euro millioni 45 ambazo ni sawa na Shilingi billioni 91. Pia akaarifiwa kwamba Euro milioni 22.5 zitatolewa kama msaada na serikali ya Uholanzi.
   
 10. T

  Topical JF-Expert Member

  #10
  Feb 4, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kigamboni kuna nini? mpaka tutumie fedha zote hivyo?

  Jengeni barabara ya kuungaisha Kigoma na Rukwa tuongeze pato la taifa kutokana na biashara ambayo tumei-block kwenda Kongo
   
 11. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #11
  Feb 4, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kigamboni kuna wantanzania mkuu, kwani Kigoma kuna nini?

  Gharama ya daraja shilingi Bilioni 91, na tuzo ya Dowans ni shilingi billioni 94. Hapo vipi, mvua na jua bora kipi?
   
 12. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #12
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hiki chama kishachoka na viongozi wake wote.... hawana jipya la kutumabia sababu hapo walipofika ndio mwisho wa uwezo wao wa kufikiri.... Njia pekee ya kupata maendeleo ni kuwaambia kwa nguvu na kwa lazima watupishe. Kwani tunataka tuweke wengine wanaojua watanzania wanahitaji nini na sio maneno matupu na usanii kila kukicha!!
   
 13. T

  Topical JF-Expert Member

  #13
  Feb 4, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kila mahali kuna Watanzania?

  Kigamboni daraja hilo kutumia billions zote hizo kwa ajili ya kusafirisha watu kuleta madafu mjini???

  Kiasi hichi ikijengwa barabara ya Rukwa -Iringa au Rukwa - kigoma

  Naamini ni economicaly wise decision..itaongeza tax base ya nchi
   
 14. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #14
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Gurudumu, nakupongeza kwa taarifa na ushahidi unaojitosheleza kuhusu ahadi hii ya CCM. Huu ndio uandishi unaotakiwa na sio ushabiki!

  Mimi na wewe na wengine tunajua tatizo liko wapi! Ahadi zinatolewa kuwafurahisha wananchi! Ndio maana miaka 10 baada mtu anauliza 'kigamboni kuna nini tutumie fedha nyingi hivyo'. Gharama za ujenzi huo ni Bil. 91 kwa mujibu wa taarifa yako, fedha za kuwalipa Dowans ni Bil. 94!! Hizo sio nyingi! Fedha za daraja zitarudi, kama sio zote ni nusu au robo! Na pia tutasaidiwa! Halikuwa na umuhimu! Halina haraka kama Dowans!

  Hilo ni moja ya mengi Gurudumu. Kwa kuyaweka wazi itasaidia! Tunakushukuru!
   
 15. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #15
  Feb 4, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Yaani umeniwahi nikitaka kumuuliza swali kama hilo
   
 16. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #16
  Feb 4, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Asante mkuu, lakini sahihisho kidogo tu. gharama ya daraja shilingi bilioni 91 ilitolewa na serikali bungeni tarehe 3 mwezi wa nane 2007. na wakati huo serikali ya Uholanzi ilikwishajitolea shilingi bilioni Euro millioni 22.5 (nisaidie exchange). kwa hiyo nahisi kilichotakiwa kutoka serikalin ni kiasi kidogo sana cha pesa.

  inashangaza kwa nini serikali ikaamua kufanya ujenzi wa daraja hili uwe na wa kibiashara. ndiyo maana NSSF ilibidi itafute wabia wa kushirikiana kujenga hilo daraja ili waje kutoza wananchi toll. pamoja na hayo, bado hawajajenga, na pamoja na matatizo yote yanayoonekana sasa hivi, bado hawana haraka.
   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Feb 4, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kweli kiazi ni kiazi tu

  Kigamboni is the blue diamond of this country, the area runs to about 70Km north of Dar, ni potential source ya income kwa serikali na kama itawekwa vyema basi its going to be the only true modern city in east africa...

  Kikubwa zaidi kigamboni ni jimbo la watanzania linaloanzia chini ya nusu kilomita kutoka ikulu... more important ni kwamba hiyo pesa ni sawa tu na ile ya kumlipa rostam ili aende kununua khanga na vitenge kwaajili ya maamuma kama wewe
   
 18. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #18
  Feb 4, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kule kuna pesa ya MCA inayotekeleaza MDG... na tax base ya kigamboni inaweza kushinda RUkwa, Kigoma combined... je unajua kwamba kinondoni pekee inakusanya kodi mara ngapi ya kigoma?
   
 19. T

  Topical JF-Expert Member

  #19
  Feb 4, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kweli mbaazi ni mbaazi

  Kwani kuwa karibu na ikulu kuna ongezaje "national income"

  Jaribu kufikiri ewe kondoo wa bwana
   
 20. T

  Topical JF-Expert Member

  #20
  Feb 4, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kwa kuuza nini kutoka kigamboni?? ehe nieleze??

  Kinondoni inakusanya kwasababu miundo mbinu imewekwa..tukiweka Rukwa (barabara tu) wataongeza biashara na tax base kwa eneo kubwa la nchi...
   
Loading...