Ahadi ya ajira milioni moja changa la macho?

Hapana wazee wangu, he was very impressed na hasa topic ya bajeti ya Elimu ambayo Mzee Moshi, aliichangia kwa namba, kilichomuuua zaidi ni issue ya Inflation ambako pia Mzee Moshi alikuwa ameweka namba alizozikuta JK, na zilivyo sasa, akasema kwamba yeye katika maisha yake hakujua kabisa kuwa kna kitu kama hiki, yaani forum kwenye internet, akaniomba nimpe forum zote kali, nikampatia na kwamba from now on hatakuwa nyuma tena,

Halafu mjadla wa Mama Salma na ndege ya rais nao ulimuua sana, yes kuna issue nyingi ambazo alinifafanulia ki-undani, lakini baada ya ile issue ya Manji sasa ninahitaji kwanza kuthibitisha kama ni ukweli ndipo ni uweke hapa,

jina kumtaja hapa siwezi kwani hiyo inamaa kuwa next time sitapata tena info!, lakini ni mmoja wa the big three katika siasa za bongo!, ambao sasa hivi ni JK, EL, na JM, hao in my understanding ndio the big three, kwani hakifanyiki kitu sasa hivi bila ya hao watatu kukubaliana kwanza!
 
neno juzi means few days back na wewe Mzee umekuwa nje ya Nchi karibi wiki 3 sasa ukaanzia Cuba na sasa tupo wote hapa US mnakula Nchi na JK . Naweza kuamini kwamba ni JK mwenyewe alikuwa anafuatilia ama ana print lakini pia nashindwa kuamini zaidi maana atakuwa yuko busy sana unless useme ana laptop na printer hapo hapo .Vinginevyo kwa kusema kwako juzi kwa maana ya siku 3 nyuma ama hata wiki si JM wala EL .
 
Sambamba na ahadi ya Rais ya kutengeneza ajira milioni moja kwa ngwe yake hii na pia kujikita zaidi katika kilimo, mipango imekamilika kuajiri kwa kuanzia mabwanashamba lukuki kama mnavyoona. This is good for our country....more jobs coming...


Mabwanashamba 2,500 kuajiriwa

2007-04-28 11:03:14
Na Lucy Lyatuu


Serikali inakusudia kuajiri mabwanashamba 2,500 katika kipindi cha mwaka huu. Hayo yalisemwa na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Stephen Wassira alipokuwa akizindua Bodi ya Watu 10 ya Wakala wa Mbegu za Mazao jijini Dar es Salaam jana.

Bw. Wassira alisema hatua hiyo inafuatia kukosekana kwa uhusiano wa kutosha kati ya wataalam wenye shahada wanaomaliza Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na wakulima.

Alisema wataalam watakaoajiriwa, watatakiwa kwenda vijijini na sio kukimbilia mijini ili kuwaelimisha wakulima juu ya kutumia mbegu bora za kilimo ili kuboresha hali ya kilimo nchini.

``Mabwana shamba wanatakiwa kwenda kijijini kujua matatizo ya wakulima ili kuweza kushirikiana na serikali za mitaa kupata suluhu yao``, alisema Bw. Wassira.

Hata hivyo, alisema wizara yake inafahamu kinachowakimbiza kijijini ni ukosefu wa nyumba.

Alisema wataanzisha mpango wa kujenga nyumba katika vijiji vyote nchini ambapo ujenzi huo utazingatia penye ukosefu wa nyumba.

``Kazi zenu sio za maofisini, tutawakopesha baiskeli ili kuwawezesha kukaa kwenye vituo vyenu vya kazi kisha kuwanufaisha wakulima,`` aliongeza.

Akizungumzia Bodi iliyozinduliwa, Bw. Wassira alisema inatakiwa kuhakikisha kuwa mbegu bora zinazalishwa kwa wingi na kusambazwa ili ziweze kuwafikia wakulima.

Alisema Bodi hiyo imeundwa ili kutoa ushauri kwa wakala wa mbegu nchini.

Aliongeza kuwa mahitaji ya mbegu bora ni makubwa ambapo kwa mwaka imekadiriwa kuwa zinahitajika tani 120,000 kwa mwaka, huku mahitaji halisi ni tani 30,000 kwa mwaka.

Alisema pamoja na mahitaji hayo matumizi ya mbegu bora yamefikia tani 12,800 kwa mwaka.

``Tofauti hii ya mahitaji na upatikanaji wa mbegu bora inaonyesha wazi kazi kubwa iliyo mbele ya wakala na Bodi ili kuhakikisha kuwa yanaongezeka,`` alisema Bw. Wassira.

Bw. Wassira aliwataka kupanga mikakati mbalimbali itakayowezesha kuongeza uzalishaji na vilevile matumizi ya mbegu bora ili kuwa sawa.

Alisema kauli mbiu ya kiongozi ni ``kuwa kiongozi katika uzalishaji, usindikaji na usambazaji wa mbegu bora za mazao ya kilimo kwa wakulima katika misingi endelevu,`` alisema.

Bodi hiyo ya watu 10 inaundwa na Bw. Peniel Lyimo, Dk. F. Mizambwa, Dk. Jeremiah Haki, Dk.Hamis Saadan, Dk. Amano Maerere, Bw. Hariel Msanga, Bw.Mahenye Muya, Bw. Mick Kiliba, Bw. Leonard Mtama na Bw. Sirael Ngwediagi.
 
Wewe mzee wa BBC unaleta bonge la twist . Umeshindwa kusema juu ya matumizi mabaya ua Serikali unaendelea yale yale magazeti ya Tanzania hapa ukiwa Ulaya ? Kuna hoja mmezikimbia umeibuka na sifa za ajira ? Nikisema ninyume basi mnaenda Mahakamani ?
 
Taasisi ya kuzuia rushwa yatangaza ajira 400


Na Mwandishi Wetu

TAASISI ya Kuzuia Rushwa (PCB) imetangaza nafasi 400 za kazi ya wachunguzi wasaidizi, walinzi na madereva.

Kulingana na taarifa ya taasisi hiyo iliyotolewa jana, kati ya nafasi hizo, wachunguzi wasaidizi 200 wanahitajika pamoja na walinzi 100 na madereva 100.

“Waombaji wa nafasi za ulinzi wanatakiwa wawe wamehitimu na kufaulu kidato cha nne au sita na kufuzu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)," inasema taarifa hiyo na kuongeza:

“Au wawe wamefaulu mafunzo ya awali ya mgambo au mafunzo ya zimamoto kama sifa ya ziada.”

Kwa madereva, waombaji wanatakiwa wawe wamefaulu kidato cha nne au sita na kuwa na leseni ya daraja C, pamoja na uzoefu wa kazi hiyo isiyopungua miaka 3.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa waombaji wenye vyeti vya ufundi na udereva kutoka Chuo cha Usafirishaji (NIT), Taasisi ya Teknolojia (DIT), Chuo cha Ufundi Stadi (Veta) au chuo chochote chenye usajili wa Veta, watapewa kipaumbele.

Aidha mwombaji wa nafasi hizo ambazo mwisho wake wa kuomba ni Mei 20, anatakiwa awe na umri usiozidi miaka 35.


Observation


No comments!
 
Qualifications za wachunguzi mbona hazijasemwa hapa na mambo mengine kuhusiana na kazi hizo ?Ama ndiyo kupelekana kimya kimya ?
 
Itasaidia pia tukijenga mazingira ya kupita hapa, wana ajira nyingi huzitangaza mara kwa mara.

Sasa hivi ni wakati muafaka kwa wazalendo wa kweli kujitokeza na kushiriki katika maendeleo ya nchi ikiwa ni pamoja na kupashana habari kuhusu kazi hizi.

Mugishagwe:
Yes ni hoja nzuri hiyo umetoa inabidi kuwakumbusha wahusika kutangaza utaratibu wa ajira utakavyokuwa itasaidia sana tukiwa na transparency at all levels.

Tutafikisha salam zako bila shaka, ni wazo zuri saana.
 
HII NI PAMOJA NA KUONGEZA MAZINGIRA YA AJIRA NA PIA UFANISI KATIKA KAZI. MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA YANAWEZEKANA...


Mishahara minono bajeti ijayo-Kikwete

2007-04-29 10:05:09
Na Godfrey Monyo
SOURCE NIPASHE


Watumishi Serikalini kuchekelea bajeti ijayo, kwa kuongezewa mishahara, kwa mujibu wa kauli ya Rais Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam jana.

Rais Kikwete, katika utekelezaji wa dhati wa ahadi zake, amewahakikishia walimu pamoja na watumishi wengine wa serikali kwamba, wataongezwa mishahara yao katika bajeti ijayo na itaendelea kuongezeka katika kila bajeti na kuboresha mazingira yao ya kufanyia kazi.

``Suala la mishahara katika bajeti ijayo, itaongezeka na itaendelea kuongezeka kila bajeti na tutaendelea kuboresha mazingira yenu ya kufanyia kazi, pamoja na ya watumishi wote,`` alisema Rais Kikwete.

Alitoa ufafanuzi huo jana alipokuwa akifungua jengo la kisasa la Kitega Uchumi `Mwalimu House` ambalo limejengwa na kumilikiwa na walimu nchini.

Jengo hilo lenye thamani ya Sh. bilioni 5.7, liko katika Manispaa ya Ilala, Jijini Dar es Salaam.

Alisema nia ya Serikali ni kuongeza mishahara ya watumishi wake na kwamba itaendelea kuongeza kwa kadri mapato ya serikali yatakavyokuwa yakiongezeka.

Rais Kikwete alisema wakati serikali inaendelea kuongeza mishahara hiyo, pia itakuwa ikiendelea kujenga mazingira mazuri ya kazi na yale ya kufundishia kwa walimu na watumishi wote wa serikali.

Hata hivyo, Rais Kikwete alisema, serikali ililazimika kuondoa posho kwa watumishi wa umma, ikiwamo ya kufundishia kwa walimu na kuziingiza kwenye mishahara ili kuwawezesha watumishi kupata mafao mazuri pale wanapostaafu.

``Hili la posho naomba nilisema hivi, ingawa halitawapendeza sana. Serikali katika miaka ya 1995/96, iliamua kuzifuta posho zote pamoja na hii ya kufundishia, baada ya kugundua kwamba wafanyakazi walikuwa wakiishi maisha mazuri kwa kupata posho hizo, lakini walikuwa wanapata mafao duni baada ya kustaafu kwa kuwa posho hizo hazikuwa zinaingizwa kwenye mishahara,`` alisema Rais Kikwete.

Aliongeza kuwa, kutokana na hali hiyo, ndipo ilipopendekezwa kwamba posho hizo ziwe sehemu ya mishahara ili kutunisha mafao ya kustaafu hatimaye mtumishi awe na maisha mazuri baada ya ajira yake kumalizika.

Rais Kikwete alilazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya baadhi ya walimu waliohudhuria sherehe hizo, kumuomba kupitia nyimbo na ngonjera walizoimba, aangalie uwezekano wa kuwarejeshea posho ya kufundisha.

Kuhusu jengo hilo la kisasa ambalo linamilikiwa kwa asilimia 100 na walimu, Rais alisema kukamilika kwa mradi huo ni kielelezo cha heshima waliyonayo walimu kupitia kazi yao ya ualimu.

``Naamini uzuri wa jengo hili ni kielelezo cha wazi cha kazi nzuri mnayoifanya ninyi walimu hapa nchini mwetu na sote tunatambua kuwa kazi ya ualimu ni ya heshima na jasho...hili mlilolijenga kwa nguvu zenu linadhihirisha heshima hiyo, alisema na kuwapongeza.

Alisema uamuzi wa walimu kuwa na kitega uchumi chao ambacho wamekijenga kwa jasho lao na kukimiliki wenyewe, ni mfano unaotakiwa kuigwa na vyama vingine kwa kuwa ni kielelezo kizuri cha matumizi ya fedha na raslimali za wanachama wake.

Rais aliwataka walimu nchini kupitia chama chao, kuendeleza mipango mizuri ya matumizi ya fedha za wanachama wao na zitakazotokana na kitega uchumi hicho kwa kutunisha mitaji ya vyama vyao vya kuweka na kukopa.

Alibainisha kuwa, uamuzi huo kama utatekelezwa vizuri utasaidia sana katika kuongeza kipato cha walimu na kuboresha hali ya maisha yao kwa kipindi hiki na kwa siku za usoni.

Hata hivyo, aliwashauri walimu kujipa muda na kutafakari kwa kina mpango wao wa kutaka kuanzisha Benki ya Ushirika ya Walimu.

``Wazo la kuwa na Benki yenu ya Ushirika ni zuri, lakini naamini linahitaji kufanyiwa kazi zaidi kwa kuwashirikisha wanachama wote na kupata ushauri wa kina kutoka kwa wataalam wa mambo hayo, halitakuwa jambo jema kuanzisha mradi ambao hatimaye utawashinda kuendesha au mkapata hasara,``alisema Rais Kikwete.

Akitoa taarifa fupi ya ujenzi wa kitega uchumi hicho, Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu, Bw Yahya Msulwa, alisema jengo hilo halikuweza kukabidhiwa kwa CWT mwaka jana baada ya kupewa ushauri wa kulifanya liwe la kisasa zaidi.

Alisema hadi sasa, asilimia 70 ya jengo hilo limepangishwa huku mteja mkubwa akiwa ni benki ya NMB.

Alifafanua kuwa, mtaji wa ujenzi wa jengo hilo ni michango ya kila mwezi ya walimu na unatarajiwa kurejeshwa katika kipindi cha miaka 10.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bi. Margaret Sitta ambaye katika salamu zake aliwataka walimu kumpa muda Rais Kikwete kuzishughulikia kero zao mbalimbali.
 
Hili la mishahara juu labda wachumi watusaidie. Sioni kama huko mbele
litakuwa na faida kwa hao wafanyakazi au wananchi, kwa ujumla. Inflation nayo itapanda, na ongezeko la mishahara kwa asilimia kumi, litafuatwa na ongezeko la vitu kwa asilimia 20

Mishahara TZ iko juu mno ukilinganisha na nchi za Asia. Huko tunakoenda itakuwa sio rahisi TZ kufungua viwanda ambavyo vinaweza kupambana na vitu vinavyoagizwa kutoka Asia. Kwa TZ sasa ni ngumu kumpata graduate
kwa chini ya dola 100 wakati China unawapata wengi tu.

Badala ya kuongeza mishahara, nguvu kubwa ingewekwa kwenye kuimarisha
huduma mbalimbali kama shule, hospitali, barabara nk. ili mwananchi asitumie mshahara huo huo kwenda kutoa rushwa ili mwanawe alipie au kulipia tuition na hata kulazimika kumpeleka mwanawe private school.
 
Tatizo la Tanzania ni kubwa sana. Mishahara imekuwa ianongezeka kwa kasi ndogo ukulinganisha na gharama za maisha. Wakati Mkapa anadhibiti inflationa alifanya hivyo kwa kusaidiwa na kukamua watu bila kupaandisha mishahara kwa kiwango cha kuridhisha. Sasa Rais Mpendwa akipandisha mishahara wakati ameshindwa kudhibiti inflationa atakiona cha mtema kuni.

Anatakiwa kwanza apunguze matumizi ya kisrisisri ya serikali kama haya ya marupurupu ya waofiza yanayozidi mishahara yao. Huu ni upuuzi sana, mtu unamlipa malupulupu makubwa ya kukaa kwenye kikao wakati hiyo ni sehemu ya majukumu yake. Nilipokuwa nafundisha pale UDSM tulikuwa tunalipwa mishahara mdiogo sana, kama Tsh 50,000 hivi ila kulikuwa na allowances za zaidi ya laki mbili: Tutorial allowance, Fuel Allowance, na Housing Alllowance: Ujinga kweli ule, unanilipa tutoriala allowance wakati kazi yangu ni kutoa hiyo tutorial!!!

Vile vile abane ufujaji wa pesa za serikali kama zile za misamaha ya kodi na idadi ya maofisa anaokwenda nao kwenye safari za nje. Apunduze pia ukubwa wa serikali.
 
mnaonaje huu mwaka mmoja na nusu,...tuliahidiwa ajira milioni moja...vipi ukichanganya walimu,majeshi,pcb,...,mabwana shamba[extention officers ],sekta ya makampuni binafsi..ets tumeshafikisha ajira hata 100,000 tangu awamu ya nne ianze? maana sio tushabikie tu...na je tumeshapoteza nafasi ngapi za kazi kwenye informal sector kutokana na sababu mbalimbalin mf waliovunjiwa vibanda,kuyumba kwa baadhi ya mazao ya kilimo,kuyumba kwa sekta ya mifuko [rift valley fever]....toa alafu jumlisha!!
 
Uwezo wa uchumi wetu hauruhusu kabisa kuongeza mshahara hata kwa senti hamsini; badala yake kunahitajika kupunguza matumizi kwanza.

Kuna mahala nilitoa mfano wa uwezo wa uchumi wetu ni kama gari (pick-up) ya uzito wa tani moja na nusu lililobeba mzigo(matumizi) unaozidi tani tano. Gari hilo haliwezi kwenda linakokusudia. Hapo zinahitajika external forces kulisaidia; japo suluhisho la kweli ni kupunguza mizigo isiyo ya lazima hadi ifikie uzito unaolingana na uwezo wa gari.

Vinginevyo ni kuchapisha minoti.....kama enzi ya mzee Rukhsa. Au kuomba msaada(mkopo) kutoka WB/IMF ili kulipa mishahara. Matokeo yake si vigumu kubashiri......

JK akiitwa msanii, wapambe wake wanakuja juu. Inakuwaje?
 
Invincible unapotea, lakini ukiibuka vitu vizito kwelikweli! I hope Kulikoni amekusoma, maana naona naye kaingia kwenye mkumbo wa kumwaga misifa bila kutafakari!
 
Hili la mishahara juu labda wachumi watusaidie. Sioni kama huko mbele
litakuwa na faida kwa hao wafanyakazi au wananchi, kwa ujumla. Inflation nayo itapanda, na ongezeko la mishahara kwa asilimia kumi, litafuatwa na ongezeko la vitu kwa asilimia 20

Mishahara TZ iko juu mno ukilinganisha na nchi za Asia. Huko tunakoenda itakuwa sio rahisi TZ kufungua viwanda ambavyo vinaweza kupambana na vitu vinavyoagizwa kutoka Asia. Kwa TZ sasa ni ngumu kumpata graduate
kwa chini ya dola 100 wakati China unawapata wengi tu.

Badala ya kuongeza mishahara, nguvu kubwa ingewekwa kwenye kuimarisha
huduma mbalimbali kama shule, hospitali, barabara nk. ili mwananchi asitumie mshahara huo huo kwenda kutoa rushwa ili mwanawe alipie au kulipia tuition na hata kulazimika kumpeleka mwanawe private school.

China sasa wasomi wengi wanapata mishahara mizuri kulikoni awali na graduate wengi wanapata zaidi ya dola mia,Hiyo mishahara ya dola mia na chini ya dola mia kwa china ni ya wale wenye elimu ya kidato cha sita na wenye elimu ya vocation college.Hiyo Dola mia kwa china unaweza ukabangaiza sana ktk maisha ya kila siku ukaweza kumudu kula na kuvaa kutokana na uwezo wa kipato chako,ukawa na mawasiliano ya uhakika kwa mwezi mzima,ukasafiri kwenda na kurudi mwezi mzima kazini na zikamuwezesha mtu kuishi bila ya Rushwa.Tanzania wengi wenye mishahara ya aina hiyo hawawezi kuhimili maisha bila ya udanganyifu aidha rushwa au kugushi.
 
Mwanasiasa Kulikoni ni mwandishi na Mtangazaji Mahili na yeye ana lako lengo kumwaga sifa lazima ili aibuke .Unategemea nini ? Nenda kwenda Blogu yake uone atakavyo mwaga misifa
 
Mwanasiasa Kulikoni ni mwandishi na Mtangazaji Mahili na yeye ana lako lengo kumwaga sifa lazima ili aibuke .Unategemea nini ? Nenda kwenda Blogu yake uone atakavyo mwaga misifa

Lunyungu, blog yake ni ipi? Pamoja na kwamba mwenyewe hajatukaribisha, lakini tunayo shauku ya kuchungulia huko.
 
Mwanasiasa Kulikoni ni mwandishi na Mtangazaji Mahili na yeye ana lako lengo kumwaga sifa lazima ili aibuke .Unategemea nini ? Nenda kwenda Blogu yake uone atakavyo mwaga misifa

Blogu yake iko wapi?
 
Back
Top Bottom