Wacha1
JF-Expert Member
- Dec 21, 2009
- 16,681
- 8,233
Rais SSH ulisema suala la tozo linafanyiwa kazi na muda si mrefu litatolewa uamuzi. Kitu cha kushangaza uamuzi baada ya kufanyika wewe umejificha Ikulu anamtuma waziri wa fedha kuja kulitolea ufafanuzi. Rais SSH hii ni dharau ambayo sisi Watanzania hatukutegemea kutoka kwako baada ya kutoa ahadi ya kulifanyia kazi.
Isitoshe uamuzi uliofanywa wa kuendelea kuwakamua walalahoi haukuzingatia mambo muhimu ambayo kisheria ni uonevu tu.
Mfanyakazi wa kawaida anapotuma pesa kwa rafiki ndugu au jamaa yoyote yule hiyo pesa inakuwa tayari imelipiwa income tax, sasa inakuwaje tena Serikali yako inatoza kodi nyingine tena ambayo kwanza Serikali haijaifanyia kazi?
Serikali inashindwa kupata kodi halali kwenye mauzo na inaamua kuchukua njia rahisi ya kuwakamua walipa kodi. Hii ni aibu!
Rais umeonyesha upendeleo katika utendaji wako hasa pale ulipotoa zawadi ya gari kwa Rais mstaafu kwamba anahitaji gari la chini zaidi kwa sababu ya kushuka, lakini unasahau kwamba Rais huyo ana pata pension ya kutosha vile vile ana ndugu ambao wana uwezo wa kumnunulia gari la chini.
Vipi sisi wa kiwango cha chini ambao tunalipa kodi mara mbili? Je, huu ndio ubunifu wa Serikali yako kupata kodi haramu?