Ahadi ni deni: Je, nini kilifanya watu wavute sigara, wakina dada wavae high heels (viatu mchuchumio)?

CalvinKimaro

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
244
312
Hakuna kitendo binadamu anatenda ambacho hakina historia yake. Bahati mbaya sana Waafrika tulifungia akili kabatini tukakataa kusoma masomo kama evolution, anthropology, n.k. Wakati waliotuketea imani zao wao wakiendelea kusoma.

Moja ya somo walilotukataza linaitwa "semiotics". Semiotics ni taaluma ya kujua tabia, mienendo na matendo ya binadamu. Mfano huwezi kuwa "nusanusa" au "FBI" au "CID" au ""NJAGU" mahiri kama hukusoma somo hili. Nina uhakika wengi wenu ndio mara ya kwanza toka mzaliwe ndio hapa mnasikia kuna hili somo. Na nina hakika mtakimbilia ku-Google 😄.

Niwape kiduchu watafiti wa taaluma hii wanasemaje?

Sikiliza! Binadamu anawasilisha ujumbe sio kwa kusema (mdomo) bali kwa kutumia viungo vyake vya mwili na kinara ni uso wake.

Binadamu ana uwezo wa kuasisi ishara laki 7 (700,000) kwa kutumia viungo vya mwili wake ambapo ishara 1000 (alfu) anatumia mwili (body) wake, ishara 5000 (alfu 5) anatumia mikono yake, ishara 250,000 (laki 2 unusu) anatumia uso wake! Idado iliyobaki anatumia viungo vinginevyo vya mwili ikiwa pamoja na nywele, masikio, ulimi, pua, idara nyeti, n.k.
Taaluma mbalimbali hasa ya upelelezi wa jinai, uajiri sehemu sensitive, n.k. hutumia sana fani hii ya SEMIOTICS.

Nawapa mfano:
Wakati mtu anasema uongo hizi ndio message kutoka kwenye viungo vyake: mboni za macho hukikunyata (contraction) na kuonekana ndogo kuliko akiwa hadanganyi au kawaida ya macho yake. Pia pembe ya mdomo hutikidika (twitching) na nyusi (eyebrow) moja huinuka ikawa iko juu kuliko nyusi ya pili. Haraka ubongo humtuma atabasamu (smiling), atikise kichwa juu chini kama anakubaliana na Jambo (infact anakubali uongo wake unamsaidia), na hukonyezakonyeza (winking).

Ubongo unaitikia uongo kwa kumlazimisha afanye mambo haya matatu bila hiari yake. Waongo wabobezi hujifunza kuzia haya yasimtokee. Anahitaji mbobezi wa SEMIOTICS kumgundua.

Kitaalam mpelelezi anatakiwa aweze kusoma hii. Inaitwa "reading the facial grammar". Yaani uso wa binadamu una maandishi yenye grammar inayosomeka na wabobezi.

Basi kwa kuwa nakua akili zenu kwa leo niishie hapa ili somo liingie kwenye medula oblangata. Somo lijalo ni kuvuta sigara na kuvaa viatu virefu: Tabia hizi zinaelezeka kitaaluma. Kama ambavyo msema uongo haogopi kuumbuka ndivyo ambavyo mvuta sigara mvaa high heels haogopi kuumia. Katika tabia za binadamu sigara na viatu virefu vilikuwa ni njia mojawapo ya binadamu kufikisha ujumbe kwa mwenzake au wenzake!

Hata kwenye siasa watu wangekuwa wamesoma SEMIOTICS wangeepuka mabalaa au watu wa hovyo hovyo. Wanasomeka! Wana grammar kwenye nyuso zao na vitabia vyao flaniflani. Hata kwenye interview ya ajira ukikuta kuna "semiotists" utakoma!

Insha'Allah panapo uhai nitaendelea sasa ili mjue kwa nini licha ya sigara kuwa na madhara na viatu virefu kuwaumiza dada zetu, kwanini hawaachi?

Niwaache na hizi sura muzisome "facial grammar" huku mkijiandaa na somo lijalo.
 

Attachments

  • 1592828108613.png
    1592828108613.png
    194.3 KB · Views: 2
... hebu nyoosha maelezo.

Namkumbusha mdau hapo mleta mada kwamba kusoma sura ya mtu na kutambua amedanganya ni kipaji, kama ilivyo kusema uongo pia ni kipaji. Kuna watu wana uwezo wa kudanganya mashine zinazopima wanaodanganya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom