Ahadi hii aliyosahau kuitekeleza Jakaya Kikwete itamgharimu kura nyingi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ahadi hii aliyosahau kuitekeleza Jakaya Kikwete itamgharimu kura nyingi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MwanaHaki, Jun 1, 2010.

 1. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #1
  Jun 1, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Alipoingia madarakani mnamo mwaka 2006, Rais Jakaya Mrisho Kikwete alionekana dhahiri kuwa ndiye mkombozi wa wananchi aliyekuwa akitarajiwa. Alifanya ziara nyingi za kushtukiza, katika kile kilichotafsiriwa kuwa kutaka kuleta mabadiliko ya kweli.

  Mojawapo ya ziara hizo ilikuwa ile aliyoifanya kutembelea magereza yaliyopo Dar es Salaam, yakiwemo gereza la mahabusu la Keko na Segerea, pamoja na gereza la Ukonga, ambako alikutana na masahibu ya aina yake. Tukio ambalo lilimsikitisha kuliko yote lilikuwa la kukutana na mwanamke aliyefungwa kwa kosa la mume wake, tena akiwa na mtoto mchanga. Tukio hili lilionekana dhahiri kumsikitisha.

  Rais Kikwete alitoa ahadi ya kuunda tume haraka iwezekanavyo ili kuhakikisha kwamba kasoro zote zilizopo kwenye magereza zinapatiwa ufumbuzi wa kudumu, mojawapo liliwa tatizo sugu la msongamano.

  Wakati awamu ya kwanza ya utawala wake - kisheria - ikiwa inafikia ukingoni, si tu kwamba hakuna kilichofanyika, bali, hali imezidi kuwa mbaya.

  Vitendo vya polisi kuwabambikia raia wasio na hatia makosa makubwa ya jinai, vitendo vya kuongezeka kwa maambukizi kwa wafungwa wakiwa mahabusu na gerezani, vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vya wanawake wakiwa magerezani na mahabusu, na vitendo vya watoto kuchanganywa na watu wazima huko gerezani, vyote hivi vimeongezeka.

  Kimsingi, ahadi aliyoitoa Rais Kikwete haikutekelezwa.

  Wananchi watalikumbuka hili ifikapo Oktoba 2010, watakapokuwa kwenye mstari, kupiga kura.

  ./Mwana wa Haki
   
 2. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Da! sidhani mkuu.
  Raia wakishapew kanga, tshert na mapilau, kero zote zitasahaulika.
   
Loading...