Ahadi hewa za wanasiasa za 2010 ninaweza kuwafungulia kesi 2015 wasipotekeleza? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ahadi hewa za wanasiasa za 2010 ninaweza kuwafungulia kesi 2015 wasipotekeleza?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mwanawao, Mar 26, 2012.

 1. mwanawao

  mwanawao JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2012
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 1,983
  Likes Received: 1,639
  Trophy Points: 280
  Wakuu kumekuwa na mchezo mchafu wa wanasiasa kuwarubuni wananchi wake kipindi cha chaguzi kwa kuwapa ahadi hewa za kuinua maisha yao.

  Wanapopewa nafasi ya kutetea haki za wanyonge wao wanaishia kuwanyonga na kusubiria muda mwingine wa uchaguzi wa kuja kudanganya kwa mara ya pili. Kwa kuwa wananchi wengi wamekuwa wakisahau waliyoahidiwa na wagombea katika kipindi husika na wanapokuja kwa mara ya pili huishia kurubuniwa na vikofia, visahani vya pilau, vihela kidogo vya pipi n.k. na kuishia kuwachagua tena mara ya pili bila kutekeleza waliyoahidi kwa mara ya kwanza.

  Sasa ninaomba kujuzwa kama kuna uwezekano wowote wa kuwashtaki wanasiasa wanaotoa ahadi hewa kwa wananchi, ili waweze kuwa makini na kuwajibika wanapopewa dhamana ya kuwaongoza wananchi. Siyo tu kwamba wahofie kutokuchaguliwa kwa msimu mwingine bali wawe na hofu ya kushtakiwa kwa kutokutekeleza ahadi zao kwa wananchi.

  Nawakilisha.
   
 2. M

  MANGI1979 Member

  #2
  Mar 26, 2012
  Joined: Mar 15, 2012
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  una machungu kama mimi lakini kwa tanzania ya kwetu kuwawajibisha bado labda kama ni proposal to be used ten years 2 come
   
 3. mwanawao

  mwanawao JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2012
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 1,983
  Likes Received: 1,639
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mangi, viongozi wetu bila kufika mahali na kuwajibishwa kwa wanayoshindwa kufanya tena kwa makusudi tu nchi yetu itabakia tu kuwa shamba la bibi.
   
Loading...