Ahadi hewa za viongozi zinafanya kuchelewa kwa maendeleo

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,191
4,104
Ili jamii iweze kuendela inahitaji mambo mengi sana ikiwamo mipango ya muda mfupi na muda mrefu. Katika kuhakikisha mipango ya mabo mbalimbali inatokea katika uhalisia viongozi wamekuwa wakitoa ahadi lukuki katika kufanikisha mipango ya maendeloeo na kutatua kero za wanachi wa jamii husika pale wanapohitaji madaraka au wanapokuwa madarakani.

Imekuwa ni kawaida sana kwa viongozi kutoa ahadi kwa wananchi bila kuangalia uwezekano wa kutekelezeka kwa ahadi hizo. Wapo wanatoa ahadi ambazo hawana uwezo wa kuzitimiza au wanajua fika kwa wakati huo haziwezekani lakini hufanya hivyo ili waweze kukuza umaarufu wao au kuweza kupata madaraka ambayo wanakuwa wanayahitaji.

Hutumia maneno mengi ya kuwalaghai wananchi amabo wanakuwa na uwezo mdogo wa kugundua kuwa ahadi hizo ni ulaghai mtupu na hana uwezo wa kuzitimiza. Wapo wanakwenda mbali zaidi na kuwafanya wananchi wadhani watawala hutatua kero au kutimiza mahitaji yao ya kuwajengea vitu wanavyohitaji kama barabara, madaraja nk kwa kutumia pesa zao mfukoni,lengo likiwa ni kupata kile wao wanahitaji. Na kwa kuwa wananchi wanakuwa hawatambui kuwa kila mradi unahitaji mipango katika bajeti na kupitishwa na bunge basi wao huwaamini na kusubiri kutimizwa kwa ahadi ambayo itachukua miaka au kutotimia kabisa.

Kutokuwepo kwa uwajibishwa wa viongozi wanatoa ahadi zisizotimizwa kumewafanya watawala kutumia uelewa mdogo wa wananchi kama mtaji kwao kwani wanajua wakihitaji tena kupata madaraka yaleyale au mengine kwa kipimdi kingine watarudi kusema muda ule haukutosha kutimiza niongeeni mwinge niweze timiza, na wanafanya hayo kwa kuwa wanajua hakuna wa kuwawajibisha hivyo hudanganya ili wao wanufaike.

Jambo hili linasababishwa na
  • Ujinga miongoni mwa wanajamii
  • Kukosekana kwa sheria inayowawajibisha viongozi wasio timiza ahadi zao au wanatoa ahadi zisizotimia
  • Rushwa
  • Jamii kutokuwa na nguvu ya kuamua nani awe kiongozi
Ahadi hewa zimekuwa zikiua mbegu ya imani kwa jamii kuwaamini viongozi wao na hata kukosa imani kwa watu wengine wanaotaka kuongoza kwa hofu kuwa hata tukiwachagua wengine huenda watafanya kama hawa hawa.

Athari za viongozi wa naotoa ahadi hewa
  • Kuchelewa au kukosekana kwa maendeleo
  • Kutengeneza jamii isiyo na matumaini
  • Kuwa na jamii isiyo na furaha
  • Kufanya uchumi kushuka au kubaki vilevile kwa kuchelewa kwa maendeleo
  • Vifo na maradhi yasiyokusudiwa
Nashauri
  1. Kuwepo na sheria ya kuwawajibisha viongozi wanaotoa ahadi hewa, mfano, ukishindwa kutekeleza ulichoahidi kwa kipindi husika unapoteza sifa ya kuendelea kuwa kiongozi.
  2. Wananchi waendelee kukumbusha ahadi walizoahidiwa bila kuchoka
  3. Wananchi waelimishwe kuhusu ukomo wa uwezo wa wanaowapa madaraka kuhusu nini wanaweza kutekeleza, mfano, wajue kazi ya mbunge ni kupeleka hoja hana uwezo wa kumjengeo chochote.
  4. utolewe elimu ya uzalendo kwa viongozi ili wajue kujinufaisha wao ni kuinyima haki jamii nzima
Watawala/Viongozi toeni ahadi zinaweza kutekeleza na kuwaletea wananchi maendeleo kusudiwa ili waweze ishi katika mazingira mazuri. Ahadi hewa zinaumiza jamii kwa miaka mingi sana.
 
Back
Top Bottom