Ahadi bila kuonyesha source the hela maana yake NINI? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ahadi bila kuonyesha source the hela maana yake NINI?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by mti_mkavu, Oct 7, 2010.

 1. m

  mti_mkavu Senior Member

  #1
  Oct 7, 2010
  Joined: Dec 23, 2008
  Messages: 116
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wakubwa naomba kueleimishwa na aina ya siasa ya bongo! Hivi kwa mtaji huu kila mtu si atakuwa mwanasiasa kama kazi ni kutoa ahadi pasipo kuwatajia source ya hizo hela zitatoka wapi? Mimi ninaamini kwa sasa hamna hela serikalini basi tunapopewa ahadi pia tuambie kitafanyika nini ili kuongeza kwa ajili ya kutimiza hizo ahadi. Mimi naona watu tunafanywa kama watoto au wajinga fulani. Basi wagombea wote wanaotoa ahadi waainishe hela zitapatikanaje kwa maana hizo ahadi hazipo kwenye bajeti! Tuelezwe vizuri kama kutakuwa source mpya za mapato. Nimechoka kusikiliza wagombea wetu. Nchi tunahijua kwa kipato chake.
   
 2. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,508
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Mkwere kishasema anategemea misaada hata alipokuwa Iringa alipokea simu kutoka NY kwa balozi kuhuhakikishia kuwa TZ misaada ni bwerere kutoka US. Kwa hiyo Kigoma kuwa Dubai, Viwanja vya ndege 3, Meli 3, Madalaja, laptop kwa kila mwanafunzi, barabara ya lami kuunganisha mikoa na...........................!!! Obama na hao wafadhiri anaowazungukiaga washatuhakikishia.

  Kuhusu Slaa, yeye kasema ataongeza ufanisi katika ukusanyaji kodi na kuanzisha vyanzo vipya vya mapato, atapunguza gharama za matumizi, no more mashangingi, pesa zinazonufaisha wachache kama za EPA, kujenja mahekaru ya BOT zitawafaidisha wananchi wote, mishahara na marupurupu ya wabunge vitalipwa kutokana na mapato ya taifa, mapato kutoka kwa wawekezaji kwenye migodi yetu ataongezeka kutoka 3% ya sasa mpaka 30+ %, Safari za matanuzi nje ya nchi na kubembea ughaibuni kama ilivyokuwa awamu ya nne hazitakuwepo, Ndege ya Rais haitatumiwa na mkewe, Urais hautakuwa wa familia na marafiki, Party ikulu kwa marafiki, Miss Wilaya, Miss Mkoa, Miss TZ, waburudishaji........................marufuku ikulu. Waimba kwaya na mashiri ni uwanjani siku ya sherehe za kitaifa. Kukutana na akina Drogba, kwenda Real Madrid, England kuangalia mpira hiyo haitakuwa sehemu ya kazi za rais wenu..................................!!!! Nafikiri mpaka hapo ushajua pesa za elimu na afya bure zitapatikanaje.
   
 3. T

  Tz Asilia Member

  #3
  Oct 7, 2010
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli wewe ni Mti mkavu, yaani na karne hii ya 21 ujui source ya hela? ushauri wa bure mtafute Profesa Lipumba akueleze.
   
 4. m

  mti_mkavu Senior Member

  #4
  Oct 7, 2010
  Joined: Dec 23, 2008
  Messages: 116
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nadhani hujanielewa! Yaani nchi tunajua source za hela na ni kwa kiasi kipo. Je? hizo ahadi zinazotolewa na wagombea mbalimbali ni mpya na tulitegemea pia kuwena namna mpya ya kuongeza hiyo hela. Je tutaongezaje? Shule bure! sawa lakini kivipi? meli, nk kivipi? Mmarekani amehadi meli? mi sijasikia.
   
 5. T

  Tz Asilia Member

  #5
  Oct 7, 2010
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Source ya fedha inaeleweka ila utashi wa viongozi wetu na utekelezaji wa ahadi zao ndiyo problem and not source of money. Upo hapo?
   
 6. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  heeeeeeee source ni misaada toka nje ndo maana mkuu hakosi kwenda nje mara kwa mara
   
 7. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  nimekuelewa saana mkuuu!
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Swali la msingi hili. Ila sidhani kama kuna mwanasiasa anaweza kulijibu hili. Wote wanaogelea kwenye dimbwi lilelile.
   
 9. m

  mti_mkavu Senior Member

  #9
  Oct 7, 2010
  Joined: Dec 23, 2008
  Messages: 116
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nashukuru kwa kuwa mmoja wapo wa kuelewa. Watanzania tusiwe tuelezwa vitu hewani bila kujiuliza mara mbili. Lini tutakuwa na watanzania wa kuweza kuuliza maswali ya msingi na siyo maneno matamu yasiyotekelezeka. Ndiyo ndiyo mzee mpaka lini? Ni wakati wa kutijoa mhanga kuwa na wanasiasa wenye mikakati yakufikia malengo. Hamna mkakati wa kutimiza hayo malengo utayafiaje? Kila chama kina dira je tutafikiaje hizo dira tupe mikakati!

  NIMECHOSHWA
   
Loading...