Agustino Mrema na Mkewe Kutangaza utalii wa ndani

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
187
442
Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labor Part (TLP), Agustino Mrema leo Machi 28, 2022 amemtambulisha rasmi Mkewe Doreen Kimbi katika ukumbi wa Keys hoteli uliopo Moshi.

Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labour Part (TLP) Agustino Mrema amesema yeye na mke wake Doreen Kimbi wanatarajia kwenda fungate katika vivutio vya utalii nchini ikiwa ni moja ya jitihada zake za kuunga mkono mipango ya Serikali ya kukuza utalii wa ndani.

Moshi. Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labour Part (TLP) Agustino Mrema amesema yeye na mke wake Doreen Kimbi wanatarajia kwenda fungate katika vivutio vya utalii nchini ikiwa ni moja ya jitihada zake za kuunga mkono mipango ya Serikali ya kukuza utalii wa ndani.

Mrema na mkewe Doreen Kimbi walifunga ndoa Marchi 24, 2022 katika kanisa katoliki parokia ya Uwomboni jimbo katoliki la Moshi, tukio ambalo lilivuta hisia za watu wengi na leo amemtambulisha rasmi mkewe huyo.

Akizungumza na vyombo vya habari leo jumatatu machi 28, 2022 mjini Moshi Mrema amesema amepokea salamu mbalimbali za pongezi ikiwemo kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Mrema amesema Doreen kwa sasa ni mke wake na kwamba watafanya kazi ya kizalendo ya kukuza utalii kwa kwenda kufanya fungate katika vivutio vya utalii nchini ambapo watatembelea hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Tarangire, Manyara na Ngorongoro.

Amesema tayari amezungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii na kumuahidi ushirikiano nae ili kufanikisha ziara yao ya kutembelea vivutio vya utalii nchini hatua ambayo wanaamini itachochea na kukuza utalii wa ndani.

Amesema ziara hiyo ya kutembelea vivutio vya utalii wameipa jina la 'Mr&Mrs Mrema Honeymoon tour’ na kwamba itaanza aprili 9, mwaka huu na lengo ni kumuunga mkono Rais Samia na kazi anazofanya za kukuza utalii wa ndani.

20220328_145837.jpg
20220328_140915.jpg
 
Mzee angeajiri wahudumu wa afya manesi wa kutosha shift masaa , wangemsaidia Sana hata tiba masaji mwili mzima. Ila kwa hiyo ndoano Nampa pole.
Kwahiyo manesi wabadilishane na kupangiana ratiba ya kumsaidia na kumfanyia usafi wa mwili? kutakuwa na usiri hapo? Naamini Lyatonga ameshagawa kila kitu, hawezi jisahau kama Mzee Mengi. Huyo dada anamgao wake, kama mke atatunza siri za Mzee.
 
Upuuzi mtupu.

Ccm mna tumia nguvu sana kuzuia moto wa Mbowe. Ila jueni moto wenu ni wa mabua. Chadema ni namba nyingine
 
Upuuzi mtupu.
Ccm mna tumia nguvu sana kuzuia moto wa Mbowe. Ila jueni moto wenu ni wa mabua. Chadema ni namba nyingine
Pata glasi ya maji baridi kwanza upate utulivu wa nafsi. Mbowe ni mtu muhimu kwenye nchi ila kumtumbukiza kwenye stori hii umelazimishia sana.. Hausiki hapa, mwache Lytonga ainjoi spotlight yake.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom