Agundulika akiwa sio mwanamke

MstahikiMeya

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
1,633
559
Ndugu zangu wapendwa kuweni makini na wasichana wa kazi za ndani.

Kuna mama mmoja kaletewa house girl akaishi nae miezi 8 nyumbani kwake hapo jana mama huyo akaibiwa baadhi ya vitu vyake baada ya kumuuliza huyo dada wakazi 'nani kaiba na wewe ndie ninaekuachia nyumba' yule mfanyakazi hakutaka kujibu ndipo yule mama akaamua kumpeleka polisi akawajibishwe ili aseme ukweli.

Wakati polisi wa kike wanamvua nguo ili kumtishia umeme aseme ukweli ndipo wakakuta ni mwanaume si mwanamke.

Kumbe alikuwa anaweka matiti ya bandia.

Na kwa vile mwenye nyumba anashinda kazini hakupata muda wa kumchunguza sana jinsia yake,yeye alidhani ni mwanamke ila ana sura mbaya iliyokomaa kumbe dume, mbaya zaidi alikuwa anamlaza na watoto wa kike chumba kimoja.

Mtahadharishe na mwenzako.

AHSANTE.
 

Attachments

  • 1432366009437.jpg
    1432366009437.jpg
    44.9 KB · Views: 2,251
  • 1432366067718.jpg
    1432366067718.jpg
    49.9 KB · Views: 4,419
Aisee, kweli dunia hadaa, sasa tutaanzaje kuwapekua wanapokuja kuanza kazi?
 
Duh aisee hiyo shida inamaana miezi yote nane hakuwahi kuhisi sio mwanamke... Sauti mienendo... Basi huyu jamaa anatabia za kike
 
Kama mke wangu angeniletea huyo mfanyakazi hata kama angekuwa mwanamke nisinge mpa kazi, ukizingatia hatumjui mtu ana sura ngumu hivyo halafu unamwachia wanao alee, si unaweza ukayapata kama yale ya house girl wa Uganda.
 
Inaonekana jamaa atakuwa ni wale wanaume wenye kupenda uwanamke,kama wale ambao huomba kuvaa sketi shule wakati ni wanaume.
 
Hii Story ya zamani sana,Nadhani kuna picha moja imeonyesha hadi kiungo chake cha ndani,ilitokea UGANDA.
 
Back
Top Bottom