Agosti kila mtanzania atalala kwenye chandarua -JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Agosti kila mtanzania atalala kwenye chandarua -JK

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jun 7, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  RAIS Jakaya Mrisho Kikwete amesema serikali yake itahakikisha ifikapo mwezi Agosti mwaka huu kila mtanzania analala ndani ya chandarua ili kuweza kupambana kuuondoa ugonjwa wa malaria nchini.
  Ameyasema hayo jana wakati akihutubia Mkutano wa 12 wa Wadau na Watafiti wa Dawa za Malaria (MMV) uliohudhuriwa na mabingwa wa kupambana na malaria kutoka mataifa mbalimbali uliofanyika jijini Dar es Salaam.

  Amesema Serikali yake imedhamiria kutokomeza ugonjwa huo, kwa kutumia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kugawa bure vyandarua kwa wananchi ili kujikinga na mbu wanaosababisha ugonjwa huo.

  Katika mkutano huo imedaiwa kuwa kila mwaka watanzania wapatao 60,000 hadi 80,000 hupoteza maisha kila mwaka kwa ugonjwa wa malaria.

  Alisema malaria huchangia umasikini ambapo ugonjwa huo unagharimu uchumi wa Afrika dola bilioni 12 za Marekani kwa mwaka kwa kuhudumia wagonjwa .
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,381
  Likes Received: 22,253
  Trophy Points: 280
  wale wanaolala miytaroni wataning'iniza wapi neti zao?
  La kwanza ilitakiwa tuhakikishe kila mtu ana lala ndani ya nyumba, bila kujalisha ni ya jinsi gani ndipo wazo la vyandarua lije
   
 3. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2011
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,880
  Likes Received: 1,051
  Trophy Points: 280
  Jamani Matamshi mengine sijui hata yanatoka wapi. I think President aliteleza ulimi!! Ama alikuwa anawapunga hao wa kuja ili apate ngawira ya kuganga njaa. Si unajua tena Lugha laini ya kuombea misaada hiyo ili majamaa yaingie laini yakutoa.. Naona Mheshimiwa ni bingwa wa fund raising!!
  MALARIA INAKUBALIKA??????????????!!!!!!!!!!!!! Maana labda litengenezwe lichandarua moja kuifunika Tanzania. MALARIA INAKUBALIKA!!!!!!!!!!!!!!?????????????!!!!!!!!!
   
 4. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,792
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  Tutamkumbuka kikwete kwa sera yake ya vyandarua!hana jingine atakalo tuachia.watu wanalala chini yeye anazungumzia chandarua!ule msaada wa cuba kutokomeza mbu umeishia wapi?
   
 5. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,120
  Likes Received: 6,604
  Trophy Points: 280
  zidumu fikira mbofu mbofu.................. zidumuuuuuuuuuuuuuuuuuu.
   
 6. M

  MPG JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Akili mgando,anawaza kwa kutumia makamasi,aache ulopokaji,zitudume fikra za mwenyekiti
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Jun 7, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,498
  Likes Received: 19,913
  Trophy Points: 280
  wape wananchi elimu ya uhakika net zinachakaa elimu haichakai
   
 8. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #8
  Jun 7, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ngoja tusubiri agosti si keshokutwa!!!halafu ishu hii ilishawahi kuzungumziwa baada ya bush kutoa msaada kwa tanzania miaka ileeeeeee alipotembelea pesa iliingia ila matumizi yake hatujayaona
   
 9. chobu

  chobu JF-Expert Member

  #9
  Jun 7, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  NAOMBA NIMSHAURI RAIS WETU KWAMBA, KUMALIZA TATIZO LA UGONJWA WA MALARIA SI CHANDARUA KWA SABABU; (i) SI KILA MTANZANIA ANA NYUMBA YA KUISHI NA KITANDA; (II) UNAWEZA KUUMWA NA MBU HATA UKIWA UMEKAA KWENYE SEHEMU ZA STAREHE USIKU, UKIPATA KILAURI. LA MSINGI HAPA AIBUE MPANGA MKAKATI WA KUMALIZA MAZALIA YA MBU TANZANIA. HILO NDIO JIBU LA KUMALIZA UGONJWA WA MALARIA KATIKA NCHI YETU!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 10. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #10
  Jun 7, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,120
  Likes Received: 6,604
  Trophy Points: 280
  na vishandarua vyenyewe ni futi 3x3 ila Zitasaidia kukinga vifaranga wasiliwe na mwewe.
   
 11. N

  NCHABIRONDA JF-Expert Member

  #11
  Jun 7, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 238
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mi siyo mwanasiasa lakini tangu huyu JK ashike Madaraka sitaki hata kusikia sera zake mana hana jipya maneno yake yamejaa tu uswahili. Hivi yeye anafikiri hayo mavyandarua yake yatatusaidia nini? Akitaka kujua kwanini nasema hivi, atembelee vijijini ndipo atajua hayo mavyandarua yake hayana faida yoyote kwa mtanzania mwenye maisha ya hali ya chini. Mkuu tafadhali sana kama umekosa ya kuongea bora uendelea kukaa zako ikulu uendelee kula zako kuku kwa mrija. Acha kutupa ahadi ambazo hazina faida yoyote, nimeongea haya mkitaka mnichukulia hatua yoyote kwani hata mkiniua sioni faida yoyote ya kuendelea kuishi.
   
 12. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #12
  Jun 7, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  tunalala baada ya tumbo kushiba.....angesema kila mtz atapigia miayo ndani ya chandarua, then xllent
   
 13. F

  FJM JF-Expert Member

  #13
  Jun 7, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hii ajenda ya vyandarua wala si ya Kikwete. Imeletwa na Wamerakani kwa maslahi yao wenyewe. Wakubwa hawa wa Marekani wamemsoma mtu wetu wakamjua vilivyo na kama mnakumbuka yeye alikuwa ni rais wa kwanza toka Africa kuonana na Obama baada ya uchaguzi wa Marekani. Haikuwa bure. Wamemwahidi kumpa Kikwete vyandarua in return watachukuwa Uranium! Biashara kichaa lakini ndio hivyo - mosquito nets for uranium!
   
Loading...