#COVID19 Agosti 22 kuwa siku ya kupata Chanjo kimkoa kwa Dar es Salaam

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
RC wa DSM Amos Makala ametoa siku ya jumapili wiki hii kuwa siku ya chanjo kimkoa katika uwanja wa Taifa kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 10 jioni kwa Watu wote bila kuangalia umri na endapo hawatomaliza kwa muda huo, mda utaongezwa mpaka wote wamalizike.

RC Makala amesema sababu ya kuweka siku ya jumapili Watu wachanjwe kwa hiari yao katika eneo la wazi ni baada ya kupokea malalamiko kwamba Watu wanaenda lakini wanashindwa kupata chanjo kutokana na foleni kubwa na wanatakiwa katika majukumu mengine ya kazi.

RC Makalla amesema siku ya Jumapili Uwanja wa Taifa kutakuwa na Wahudumu 100 watakaotoa huduma ya chanjo, pia amewaagiza Wakuu wa Wilaya zote za DSM kuweka siku moja itayoruhusu Watumishi wote na Wananchi kupata chanjo ili kuwezesha wengi kuchanjwa
 
Napendekeza ziambatane na mikesha ya mwenge, zi-karibu ku-expire…. kila mtu apate.

Sandakalawe.
 
Tunakwenda Kanisani.
Mtabadili kila mbinu.
Mungu atawapinga kila Kona si hamtaki kumtaja Mungu aliyetuokoa na mawimbi yote yaliyopita.

Kawakusanyeni mateja muwajaze vituoni,walaliane mseme Tanzania watu wagombania chanjo.

Mtajuta kuleta chanjo.
Mpkaka mtajua Mbingu Zina miliki na kutawala.
 
Haah Sasa Kama huko walishindwa sababu ya foleni, hapo uwanja wa taifa foleni si ndio itakuwa kubwa zaidi?
 
RC wa DSM Amos Makala ametoa siku ya jumapili wiki hii kuwa siku ya chanjo kimkoa katika uwanja wa Taifa kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 10 jioni kwa Watu wote bila kuangalia umri na endapo hawatomaliza kwa muda huo, mda utaongezwa mpaka wote wamalizike.

RC Makala amesema sababu ya kuweka siku ya jumapili Watu wachanjwe kwa hiari yao katika eneo la wazi ni baada ya kupokea malalamiko kwamba Watu wanaenda lakini wanashindwa kupata chanjo kutokana na foleni kubwa na wanatakiwa katika majukumu mengine ya kazi.

RC Makalla amesema siku ya Jumapili Uwanja wa Taifa kutakuwa na Wahudumu 100 watakaotoa huduma ya chanjo, pia amewaagiza Wakuu wa Wilaya zote za DSM kuweka siku moja itayoruhusu Watumishi wote na Wananchi kupata chanjo ili kuwezesha wengi kuchanjwa
Asante kwa taarifa.
Ila kusema ukweli viongozi wetu jiongezeni kwa kutumia akili za Ziada.
Hivi inaingia akilini kweli ukawakusanye watuntaifa yaani wahudumu 200 tayari nishida!
Bado wataka watu mkoa wa Dar kuanzia Mbezi, Kibamba, Tegeta, Bunju Mbagala nakwingineko waje Taifa pamoja na foleni na tatizo la usafiri.
Ni kwanini hamkufikiri kuwagawa hao wahudumu 200
Kwa kila wilaya viwanja na mashule ziko nyingi huduma ikawa nyepesi? Vipe wazee wanaendaje huko?
Kama kweli mnataka kutoa huduma tengueni hii kitu haraka na kuwe na utaratibu shirikishi tuache kuwataabisha wana Dar Es Salaam.
Akili kubwa!!.
 
Serikali bhana,,, wanaita watu taifa ili Jumapili wasisikie kelele za Gwaji boy waende taifa...

Unakataza mikusanyiko wakati huohuo unaita mikusanyiko...

Akili kumkichwa na ujinga kumkichwa pia
 
Back
Top Bottom