Agost 27: Hukumu ya mch. Mtikila kwa kusambaza waraka chochezi dhidi ya Rais Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Agost 27: Hukumu ya mch. Mtikila kwa kusambaza waraka chochezi dhidi ya Rais Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gumzo, Jul 26, 2012.

 1. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [h=3][/h]

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imesema Agosti 27 mwaka huu, itatoa hukumu ya kesi ya kusambaza waraka wa uchochezi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila dhidi ya Rais Jakaya Kikwete.

  Hayo yalisemwa jana na Hakimu Mfawidhi Ilvin Mugeta muda mfupi baada ya shahidi wa pili wa upande wa utetezi katika kesi hiyo ambaye ni Mpiga Picha wa Gazeti la Mwananchi, Mpoki Bukuku kumaliza kutoa ushahidi wake na Mtikila mwenyewe kumaliza kujitetea.

  Hakimu Mugeta alisema anakubaliana na ushauri wa Mtikila uliosema ameamua kufunga ushahidi wake jana licha hapo awali aliahidi kuleta mashahidi wake 10 ili waje kumtetea kwasababu endapo mashahidi hao angewaleta wangezungumza mambo ambayo ameishayazungumza yeye na Bukuku na kwamba hukumu ya kesi hiyo ataitoa Agosti 27 mwaka huu.

  Mtikila akimaliza kutoa utetezi wake jana alidai kuwa mashitaka aliyoshitakiwa nayo siyo sahihi na kwamba waraka aliousambaza wenye kichwa cha habari kisemacho “Kikwete kuungamiza kabisa ukristo!


  KWA HABARI KAMILI BOFYA HAPA GUMZO LA JIJI
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Alhamisi, Julai 26, 2012 | Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

  MWENYEKITI wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila anatarajia kuhukumiwa Agosti 27, mwaka huu kwa makosa ya kusambaza waraka wa uchochezi dhidi Rais Jakaya Kikwete kwamba anataka kuuangamiza Ukristo.

  Uamuzi huo, ulitolewa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Hakimu Mkazi, Illivin Mugeta anayesikiliza kesi hiyo baada ya Mtikila kufunga ushahidi.

  "Mheshimiwa nafunga ushahidi, ilikuwa nilete mashahidi 10 lakini wawili wanatosha kwa sababu wengine walikuwa maaskofu kutoka Mwanza ambao naamini wangekuja kueleza kile kile nilichoeleza.

  "Nahofia kupoteza fedha za Serikali kwa kuwaleta mashahidi hao, hawana kitu tofauti,"alidai Mtikila.

  Hakimu Mugeta alisema uamuzi wa Mtikila ni mzuri asipoteze fedha za umma kama anaamini hivyo, alikubali kufunga ushahidi na kupanga Agosti 27 mwaka huu kwa ajili ya kusoma hukumu.

  Mtikila ambaye ni shahidi wa kwanza upande wa utetezi alidai kesi hiyo ilifunguliwa kutokana na chuki zilizokuwepo kati yake na mchungaji mwenzake lakini kwa upande wa Rais Kikwete hakumshitaki pamoja na kwamba alimpa nakala ya waraka huo unaodaiwa wa uchochezi.

  Shahidi wa pili wa upande wa utetezi, Mpoki Bukuku kutoka Gazeti la Mwananchi alidai mahakamani kwamba, walichapisha habari yenye kichwa cha habari ‘Mtikila apiga kampeni kanisani kumpinga Kikwete'.

  Pia liliandika achunguzwa na Polisi kwa kumwaga sumu, Rais Kikwete asichaguliwe mwaka 2010 na kuongeza kuwa habari hiyo iliripoti kilichotokea Mwanza na ilikuwa ya kweli kwa sababu kati ya polisi na Mtikila, hakuna aliyekanusha.

  Alidai habari hiyo, ilikuwa ikielezea mafundisho waliyokuwa wakitoa viongozi wa dini katika lile kongamano.

  Mtikila, anadaiwa Aprili, 2010 mjini Dar es Salaama alisambaza waraka anaodai wa kuunusuru Ukristo wenye lengo la kuangamizwa na Jihad ya Rais Jakaya Kikwete na kwamba Wakristo wajitoe muhanga kukomesha ugaidi.

  "Kikwete anaangamiza Ukristo, amekuwa jasiri wa kuingiza Uislamu katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,"alidai Mtikila katika waraka wake.Alidai waraka uliosambazwa alisaini akiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya kuunusuru Ukristo na walichapa nakala 100,000 lakini aligoma kutaja mahali walipochapishia nakala hizo.

  Maelezo yote hayo yalitolewa mahakamani kama kielelezo na SSP, Ibeleze Mrema aliyemuhoji Mtikila Aprili 14, 2010 na alipotakiwa kueleza chochote kuhusu kielelezo hicho, mshitakiwa alisema hana swali na akakubali kipokelewe na mahakama.
   
 3. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Mtikila anasema kweli na kama huamini subiri uone kama atapatikana na kosa, labda uamsho wahamie Iran
   
 4. Whisper

  Whisper JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2012
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 502
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mwenye macho haambiwi TAZAMA. Wote tunaona na tunatambua ni nini kinachoendelea.
   
 5. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,834
  Trophy Points: 280
  Ngoja tuone!
   
 6. j

  jembe mwanaharakati Member

  #6
  Jul 26, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mtikila hajakurupuka kuna kitu hapo,huu waraka unapatikana site gan au umepotezwa?
   
 7. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Mtikila yuko sahihi sana
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Sijui ni lini viongozi wa nchi hii wataacha kuwadharau wananchi na kufanya kazi zenye tija? Mtindo wa kujizushia kashfa na hata kesi ni wa-kizamani sana, na nilitegemea kuona ustaarabu na utashi toka kwa viongozi wetu wa kufanya mambo kisasa. Mtikila amepewa ajira ya kudumu ya kendeleza porojo kwa maslahi ya wachache huku akipoteza muda/resources za walipa kodi kuendesha kesi ambazo ziko kimaslahi zaidi.

  Angekuwa kweli analeta mtafaruku huyu Mtikila angekuwa Mabwepande, lakini kila kukicha yuko mahakamani! Kuna watu wanaozea rumande kwa sababu majaji wako busy ni kesi za ki-mtikila! Mwaka 2012 bado tunafanya mambo kwa mtindo wa cheusi-chekundu! Bahati mbaya sana.
   
 9. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Jukwaa la siasa
   
 10. t

  tabu kuishi JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 354
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Natamani niuone huo waraka,unapatikana wapi wajameni?
   
 11. C

  Careboy wamuntere Senior Member

  #11
  Jul 26, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanaosema mtikila yuko sahihi, ni wanafki kwa sababu kama kuna dini inayoangamizwa na serikali basi ni uislam na porojo ya Mtikila ni kupotezea waislam akili, lkn nakuambieni waislam wa leo wako macho 24 hrs na hawadanganyiki, lkn tu nionye kwamba haya mambo ya kidini siyo ya busara anayehisi kusali au kufanya ibada basi aende msikitini au church, mambo ya serikali iachieni yenyewe, na kama mtaendeleza hii mijadala ya kidini ni kwamba mnatega bomu ambalo likilipuka sijui kama mtakuwa na wasaa wa kuingiza udaku kwenye mitandao. mi nashangaa sana, watu badala ya kuelimishana mna post udaku kila kukicha. this is injustice.
   
 12. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #12
  Jul 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  tupe sababu 3 jinsi serikali invoangamiza uislamu tanzania
   
 13. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mtikila is right 100%.
   
 14. peri

  peri JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  hakuna asiyemjua mtikila na porojo zake nchi hii, kinachonishangaza ni watu wanomtetea.
  tz ya leo hatuhitaji udini ili tuendelee na tukiendelea kushabikia hizi porojo zitatupeleka pabaya.
   
 15. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Nijuavyo mimi:
  • Kusoma/kutoa hukumu = Kutoa maamuzi ya kesi kwamba mshitakiwa ana hatia au la
  • Kuhukumiwa = Kumtia mtu hatiani na kutangaza matokeo stahiki kama kifungo, faini, nk

  Kwa mtikila tarehe 27 August ni siku ya kusomwa/kutolewa hukumu na ndiyo itajulikana kama ana hatia (atahukumiwa) au la. Mbona wewe unaandika kana kwamba unajua maamuzi ya kesi kwamba ameshatiwa hatiani kabla hukumu haijasomwa?

  MY TAKE:
  Ivi kiswahili ni kigumu kweli kiasi hicho au ni matokeo ya kujaza ma*i kichwani badala ya ubongo?
   
 16. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #16
  Jul 26, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,635
  Likes Received: 4,739
  Trophy Points: 280
  Wewe na huyo Mtikla wote sawa hakuna dini inayoangamizwa na serikali, ila watanzania kwa ujumla wao wanaangamizwa na serikali dhalimu ya CCM, hizi porojo za udini ni janja ya CCM kuwagawa kwa misingi ya kidini ili wasiwe wamoja kuipa nafasi serikali dhalimu kuifisadi nchi. Huu upuuzi wa udini ni kanunu ya watawala dhalimu siku zote kuwagawa wananchi kama walivyofanya wakollni.Mtu yoyote anayeshabikia mambo ya udini ni mpumbavu kabisa kwani suala la dini ni jambo binafsi kati ya mwanadamu na muumba wake (kama yupo kwani haya mambo ya dini mapokeo tu.)
   
 17. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,198
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Swaumu kali nini?
   
 18. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #18
  Jul 26, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Mtikila nae na upmbf wake!!
   
 19. Fyengeresya

  Fyengeresya JF-Expert Member

  #19
  Jul 26, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 60
  Sijui unakataa lipi na unaunga mkono lipi, waislam wanapotaka mahakama za Kadhi kwa Serikali wapo sahihi iache Serikali ijiamulie, Wakristo wakilalamika kwa lolote kuhusu Serikali unaita ni udini. Kuwa muwazi mkuu. Ukitaka amani unatakiwa kufanya mambo kwa uwiano.
   
 20. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #20
  Jul 26, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  From my heart nimemkukmbuka Mtikila, hasikiki au ndiyo kanyamazishwa nini?
   
Loading...