Hayo maujenzi sijui vipi. Ndo bei za ujenzi, nyumba na viwanja zikawa zinapaa kila kukicha. Tulikuwa kama tuko newyork au London. Maisha yakuigiza kabisa yale.
Waliokuwa wanakimbilia kila MTU mijengo na mahoteli ya thamani kubwa Kwa kipato cha wateja wapi? Au kutegemea mazungu ya unga?
Mauwekezaji kwenye ujenzi yalikuwa ya gharama sana na kila mmoja alikuwa anakimbilia huko Kwa sababu zake kuanzia watu binafsi mpaka taasisi za umma.
Unajenga jengo la bilioni 5 wateja wenyewe WA vipato vya laki 5 Kwa mwezi. Utapata wapi wateja kufanya marejesho na kupata faida baada ya kutoa garama za uendeshaji?
Ukisikia kuiga biashara ndo huku. Watu walijua kipindi cha kuhonga semina za serikali zikafanyikie hotelini kwao kitaendelea milele
Bora hata bosi slim angekuwa amefungua kiwanda cha uzalishaji. Uwekezaji kwenye maujenzi ulikuwa wazi ungefeli tu. Lilikuwa suala la muda
Sema imetokea haraka zaidi
Hali hii hata mimi niliiona. Nilihisi ongezeko la thamani kwenye ardhi na majengo halikuwa halisi. Sasa ukweli unajidhihirisha. Nimeona pia udhaifu mkubwa wa huyu mwekezaji ktk maamuzi yake. Maamuzi yake ktk kuwekeza yalikuwa based on speculation kwa sehemu kubwa.