Kamukhm
JF-Expert Member
- Aug 30, 2015
- 2,799
- 4,195
Huu utaratibu ni wa kijima sana. Kwanini wasilipwe mishahara kwa mwezi hata laki 8 ..kisha madini yakitema wanapata bonus ya asilimia walau 5 ya faida.. baada ya kutoa gharama za uendeshaji!?Kama swala ndo liko hivyo, waziri kuwazuia wanaapolo kuuza madini yao waliyopata kwenye hayo masalia ni uonevu wa hali ya juu, kwa sababu kimsingi hawezi kuisimamia hiyo 10% anayodai, labda aje hapa atuhakikishie kwamba ataisimamia. Nimeona kwenye reply moja yule masai aliyepata mabilioni alitoa 2.5mil. pekee kwa kila mwanaapolo ambao hawazidi 50 jumla yao. Sasa ukipiga hesabu ya 10% kwenye hayo mabilioni ugawe kwa 50, sidhani kama kila mwanaapolo angeambulia 2.5mil. pekee.