The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,503
- 2,046
Leo nimeamka asubuhi nikitazamia daladala zote zinazofanya kazi hapa mkoani Dar es Salaam zitakuwa zinapakia level seat na abiria wote wakivaa barakoa, sawasawa na agizo la mkuu wetu wa mkoa.
Ukweli ni kwamba hakuna kilichobadilika mtaani, tofauti sana na ilivyokua kwenye wimbi la mwaka jana ambapo baada tu ya tangazo la serikali kuhusu barakoa na level seat kesho yake kila mtu alitimiza wajibu wake.
Polisi ambao ni watekelezaji wa Sheria walikamata mabasi yote yaliyozidisha abiria, huku makondakta wakiwakataa abiria waliozidi. Kwa upande wa raia walikuwa wakali sana wakiona mtu hajavaa barakoa.