#COVID19 Agizo la RC Makala kuhusu ujazo wa daladala na uvaaji barakoa limedharauliwa au halikueleweka?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
761
1,000
Leo nimeamka asubuhi nikitazamia daladala zote zinazofanya kazi hapa mkoani Dar es Salaam zitakuwa zinapakia level seat na abiria wote wakivaa barakoa, sawasawa na agizo la mkuu wetu wa mkoa.

Ukweli ni kwamba hakuna kilichobadilika mtaani, tofauti sana na ilivyokua kwenye wimbi la mwaka jana ambapo baada tu ya tangazo la serikali kuhusu barakoa na level seat kesho yake kila mtu alitimiza wajibu wake.

Polisi ambao ni watekelezaji wa Sheria walikamata mabasi yote yaliyozidisha abiria, huku makondakta wakiwakataa abiria waliozidi. Kwa upande wa raia walikuwa wakali sana wakiona mtu hajavaa barakoa.
 
Vishu Mtata

JF-Expert Member
Dec 15, 2019
1,652
2,000
Ndio nimetoka kushuka kwenye daladala hapa.

Baada ya kuoja tangazo la mkuu wa mkoa nikajua basi huko road hali ni mbaya mpaka nikawa najishauri nitoke au nikache tu.

Kuumbe waaalah hali ni kama kawaida na tulishona ile mbaya. Labda agizo halijaskika na si ajabu wengi hawamjui huyo makala ni nani.
 
white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
6,106

Ni ngumu sana kwa sasa kueleweka, kwani toka mwanzo walitumia sana propaganda za kupotosha juu ya gonjwa hili, na watu wakawaelewa maisha yakaendelea kama kawaida sasa leo tena unabadirika!!mfano mzuri unauona hata kwenye chanjo, wanavyojichanganya waziri anasema wamejirizisha juu ya chanjo hizo kabla hajiletwa, jana msemaji wa serikali anasema kwa sasa tmda, wako wanajirizisha ubora wake kabla hazijaanza kutumika nchini!!wataweka miongozo mingi sana ili waonekane wako pamoja na hao wenyewe, waweze kupewa pesa ila on ground watuache tuishi tulivyozoea tu,
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
24,328
2,000
Kwa sasa viongozi wana kazi kubwa.

Hili la corona hata wanaopingana na gwajima wanapaswa kuwa waangalifu sana,vinginevyo kuna kudharaulika kwa kiwango kikubwa sana.
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
29,637
2,000
stimulus package iko wapi?

level seat inaua biashara

Hasara inafidiwaje? Wapunguze kodi au kuwapa ruzuku wenye daladala ili wabakie pale pale walipokuwa kibiashara kabla ya hizo hatua za level seat au waruhusu nauli kupanda

Kuna maeneo ukiweka level seat watu watafika kazini saa nane mchana badala ya asubuhi sababu ya uwingi wa watu ukilinganisha na idadi ya daladala

Si kutoa maagizo tu peke yake ni lazima kuangalia na factors zingine
 
analgesic

JF-Expert Member
Jul 27, 2013
479
500
Seat level kwa sasa haiwezekani, practically. Mara ya kwanza corona ilileta attention dunia nzima hivyo reaction ilichukuliwa na dunia nzima hivyo kupelekea
1. Mafuta ya diesel na petrol kushuka bei 1500+ vs 1600+ sasa hivi 2300+ hiyo daradara itakayokubali kupakia seat level utaitoa wapi?
2. Wananchi wameshaizoea hivyo hawaoni umuhimu wa kuchukua hatua tena
 
kapandila

Member
Feb 1, 2017
21
75
Serikali ya mkoa ingetoa elimu juu ya uvaaji wa barakoa tu ingetosha kabisa lakini kwenye issue ya level seat kwakweli nikuwaonea tu kuanzia abiria, madereva na wamiliki wa vyombo vya usafiri... Mkuu wa mkoa anaishia kutangaza tu kwenye vyombo vya habari lakini ilitakiwa kuanzia huku mtaani wenyeviti wa mitaa wapite wanatangaza kama sio kutoa elimu maana navyojua mm kwa hapa dar wakazi wengi si wafatiliaji wa habari kutokana na muda huo wa habari wakazi wengi ndo wanakuwa njiani wanarudi... Binafsi nilitegemea zaidi kwenye ile mechi ya simba na yanga wizara pia ingetumia platform ile angalau wachezaji wakati wa kusalimiana wangekuwa wamevaa t shirts zenye ujumbe wa tahadhali ya kujikinga na corona maana watu wengi kwa wakati ule walikuwa wanafuatilia mechi ile..
 
KISIWAGA

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
4,215
2,000
Watu bado wako na access ya zile videos za marehemu wa chato wangewasiliana na YouTube zifungwe maana ngosha alikomalia sana issue ya papai kuwa na korona
 
EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
14,321
2,000
stimulus package iko wapi?

level seat inaua biashara

Hasara inafidiwaje? Wapunguze kodi au kuwapa ruzuku wenye daladala ili wabakie pale pale walipokuwa kibiashara kabla ya hizo hatua za level seat au waruhusu nauli kupanda

Kuna maeneo ukiweka level seat watu watafika kazini saa nane mchana badala ya asubuhi sababu ya uwingi wa watu ukilinganisha na idadi ya daladala

Si kutoa maagizo tu peke yake ni lazima kuangalia na factors zingine
Sometimes akili zinakurudiaga au unazirudiaga?
 
Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
1,485
2,000
Wiki yote iliyopita iligubikwa na maagizo mbambali ya kujikinga na ugonjwa hewa wa corona Tanzania.
Yani ugonjwa wa corona unatafutwa kwa tochi nchini Tanzania.

Dunia inakotoka sisi watanzania ndiyo tunaenda kwa kasi ya 4G!!
Dunia nzima wanaachana na mashariti ya distance na barakoa sisi ndiyo imegeuka wimbo ,hadi watoto wa shule za msingi huko vijijini wanalazimishwa wavae barakoa!

Hivi corona ingeingia mwaka 2019 tukiwa na viongozi wa aina hii ,hali ingekuwaje?
Hata hivyo wananchi wameamka na kupuuza maagizo yote na wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.
 
UHURU JR

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
12,778
2,000
Seat level kwa sasa haiwezekani, practically. Mara ya kwanza corona ilileta attention dunia nzima hivyo reaction ilichukuliwa na dunia nzima hivyo kupelekea
1. Mafuta ya diesel na petrol kushuka bei 1500+ vs 1600+ sasa hivi 2300+ hiyo daradara itakayokubali kupakia seat level utaitoa wapi?
2. Wananchi wameshaizoea hivyo hawaoni umuhimu wa kuchukua hatua tena
Inachofanya serikali ni kutoa matamko ya corona au kukomoana kwa kutumia corona na si kupambana na corona, ndio kama hivyo unatoa matamko ya level seat huku suala la mafuta hujalifikiria na hapo hapo ndio kwanza unaongeza mikodi.
 
Wang Shu

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
2,529
2,000
Acha watu wasafiri wafike haraka kuliko kuwasongamanisha kwenye vituo vya daladala
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom