nyumbatatu
JF-Expert Member
- Jul 19, 2013
- 1,076
- 939
Agizo la rais Magufuli kutakakupandishwa cheo kwa askari wa usalama barabarani koplo Deogratius Mbango halijatekelezwa hadi sasa.
Askari huyo alitawala katika vyombo mbalimbali vya habari mwanzoni mwa mwezi uliopita baada ya kurekodi tukio la yeye kumkamata mke wa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki, kikanda na kimataifa, balozi DK. Augustine Mahiga, kwa kosa la kutotii mojawapo ya sheria za usalama barabarani.
Magufuli alitoa agizo Hilo wakati wa mkutano wake na makamanda wafawidhi wakuu, wakuu wa upelelezi wa mikoa na vikosi uliofanyika mjini Dodona na kumwambia mkuu wa jeshi la polisi (IGP), Ernest Mangu, aliyekuwepo kwenye eneo hilo kuwa: "....yule trafiki anajua kazi, mpandishe cheo. Na huyo waziri na mke wake nimeshawaambia".
....Hata hivyo duru za ndani ya jeshi la polisi zinaeleza kuhusu utata kwa IGP Mangu kukubali kumpandisha cheo mtu ambaye amekiuka kanuni za kudumu za jeshi la polisi(Police General Orders).
Kwa mujibu wa kanuni za polisi kupitia tangazo la serikali (GN), na. 162 ya mwaka 1998, inayosema;-
"without due authority discloses or conveys any information concerning any investigation (bila ya kupewa kibali maalumu askari hatakiwi kufichua au kusambaza taarifa yoyote inayohusu uchunguzi unaoendelea).
Kwenye suala la koplo Mbango kitendo cha kutoa siri za mazungumzo yake na bosi wake kuhusu suala la mke huyo wa waziri kwenye mitandao ya kijamii kinaelezwa kukiuka taratibu hizo za kipolisi na ndiyo maana Mangu anapata shida kumpandisha cheo.
Kitendo alichofanya Mbango kinapaswa kuadhibiwa na Si kupongezwa. Kama askari wote wataamua kuwarekodi wakubwa zao kwenye mazungumzo ya kikazi na kuyasambaza kwenye mitandao, unadhani mwisho wake utakuwa nini?
Kilisema chanzo chetu makini kutoka jeshi la polisi.
Chanzo: Raia Mwema
My take kwa hiyo hapo mkuu kaendelea kukurupuka?.