mchimbadhahabutz
Member
- Oct 15, 2016
- 56
- 49
Ni takribani mwezi na nusu toka mheshimiwa rais Magufuli atoe kauli yake dhidi ya wawekezaji kujirimbikizia maeneo ya uchimbaji madini makubwa ambayo hawayatumii huku watanzania wakifa na njaa. Alizuia wapiga kura wake kufukuzwa hovyo kwa ajili ya muwekezaji mmoja.
Cha kushangaza jana waziri anaehusika na mazingira mh. Luhaga Mpina amekuja katika machimbo ya Mwasabuka wilayani Nyangware mkoa wa Geita na kutoa siku 30 tu kwa wachimbaji hao kuondoka na pabaki na ndege na miti tu.
Waziri huyo alijificha kwenye kichaka cha uharibifu wa mazingira kama sababu ya kuwatimua watanzania hawa.
Ikumbukwe kuwa mgodi huu umesaidia sana kupunguza njaa kwa kujipatia walau kipato kidogo cha kumudu maisha yao.
Sasa nashindwa kuelewa hivi ni kwanini watanzania hawa serikali imekuwa ikiwatesa kiasi hiki?
Kuna watu waliwekeza pesa zao baada ya serikali kuruhusu kupitia mkuu wa mkoa wa Geita na m/kiti wa CCM Geita mh. Msukuma leo tena mnawatimua.
Waende wapi sasa maana wamekua ni kama ng'ombe wanaswagwa tu.
Kwa hali hii kwa nini watu wasiichukie serikali hii? Watashawishika vipi kuichagua tena 2020?