Agizo la Magufuli kukamata magari ya Serikali utata mtupu

Patriote

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
1,718
1,047
Hivi karibuni, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, John Ndunguru alivieleza vyombo vya habari kwamba Serikali iliweka utaratibu unaozuia matumizi ya namba za kiraia kwenye magari yake isipokuwa kwa kibali maalumu. Alisema kuwa hali ya kuzuia namba hizo iliibuka baada ya kubainika kwamba kupitia namba hizo, magari ya umma yanatumika vibaya na baadhi kupotea.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohammed Mpinga alisema Waziri alitarajiwa kutoa ripoti jinsi zoezi hilo linavyoendelea kwa kuwa Waziri mwenyewe ndiye anatakiwa kuzungumzia suala hilo. Alisema zoezi la ukamataji magari linaendelea kwa muda wa miezi mitatu mfululizo lakini hakusema idadi ya magari yaliyokamatwa hadi hivi sasa.

Source:Mwananchi 29/11/2012


Nionavyo mimi

Ufujaji, wizi, matumizi mabovu ya Magari ya Umma hapa nchini umekuwa ni jambo la kawaida na ni tatizo sugu ambalo nadhan hatujawahi kukaa chini kujiuliza na kubaini tunapoteza kiasi gani cha fedha za walipa kodi katika kuhudumia magari haya. Matumizi halali ya Magari haya ni kuwasafirisha watumishi wa umma kutoka point A kwenda B na kuwarudisha Point A wakiwa katika kutekeleza majukumu walioajiriwa nayo.

Ni muda mrefu sasa suala la matumizi mabaya ya magari ya umma limekuwa likizungumzwa. Ieleweke kuwa ni kinyume na utaratibu kutumia magari haya kupeleka watoto wa Mkurugenzi Shule, Kumpeleka Mke wa Waziri Saloon, Kubeba Majani ya Ng'ombe na kumpeleka Mkuu Flani kwenye ukaguzi wa Nyumba anayoijenga huko Bunju. Hata kama gari hilo litaombewa na kupewa kibali cha kutumia namba BINAFSI badala ya ile ya UMMA. Ubadilishaji wa namba toka ya Umma (SU/SM/ST../PT) kwenda Binafsi (T 1000 APX) haiondoi sifa ya Gari la Umma kuwa Gari la mtu Binafsi na kulitumia kwa matumizi Binafsi/ya familia yako.

Uwe waziri, mwenyekiti wa Bunge, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Mkuu, Mkurugenzi, Mkuu wa Mkoa na Hata Mkuu wa Majeshi nchini, si ruhusa kutumia Magari ya Umma kwa shughuli zako binafsi au za Kifamilia. Hayo Magari ni ya wananchi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania na gharama za kuyahudumia magari hayo ni kodi zetu hivyo sio haki, na sheria pia hairuhusu kuyatumia magari hayo kwenye shughuli zisizo za kiserikali.

Ninyi nanyi mna haki ya kuagiza magari yenu toka ng'ambo au mnunue kwenye show rooms ili yahudumie familia zenu. Hamna haki ya kutubebesha matumizi ya familia zenu sisi wananchi, kwanza watu wenyewe ndo mnaotufisadi, mmeona hiyo haitoshi hadi na mizigo ya familia zenu mtubebeshe sisi jamani???? Inatosha jamani!!!Ifike mahali mali za Umma ziheshimiwe na nyie wenyewe muone haya na aibu kuwa ni wizi kufanya hivyo.

Kitendo mnachokifanya cha kutumia magari ya umma kwa shughuli za kifamilia, hakuna tofauti sana na kuchukua mafuta yanayoendesha kiwanda flani cha umma kisha ukaweka kwenye gari lako binafsi. Kimsingi hapo ni sawa na kusema Cost za familia yako/zako binafsi umeamua kuziinject kwenye production ya Kiwanda.

Hivi ni vitendo vya wizi ila ni style unaufanya wizi huo kwa tofauti tu za kuiba. Control la matumizi holela ya magari ya Umma/Serikali sio jambo gumu hata kidogo, ila suala hili linaonekana ni gumu kwa maana linawahusu WAKUBWA!!!Dereva hawezi kutotii agizo la kuacha gari la ofisi, ofisini siku ya ijumaa jioni! Na wala dereva hawezi kutokomea na gari la Serikali na likapotea.

Nionavyo mimi, hata askari wakikesha barabarani kukamata magari haya miezi yote ya mwaka, mwisho wa siku wataishia kuyaachia na yataendelea kutumika vibaya, mana haya hatujaanza kuyasikia leo. Alianzaga Mrema kuyabana enzi hizo, hadi leo hakuna kinachoendelea, ugumu wa katazo hili ni kwamba wanaotumia magari ya Umma kinyume na sheria ni WAKUBWA wa nchi hii!! Wakurugenzi, wakuu wa vitengo, mawaziri etc.

Suluhisho!!

Serikali ipunguze magari yake mana kwa kufanya hivyo itapunguza costs za kuyaendesha. Ikumbukwe kuwa katika kuyahudumia magari hayo, dereva ataiba diesel, mechanics atadoa spare mpya na kuweka za zamani, afisa manunuzi atafanya ufisadi wa kuongeza bei wakati wa kuyanunua na hata kwenye uagizaji wa vipuli vyake, achilia mbali kuuziana magari hayo kwa bei ya kutupa na kukopeshana magari mapya ya serikali. Costs hizi zooooooooooooote zinamwangukia mlipa kodi wa Kidawe, Malinyi, Matombo na Kazuramimba ambaye hajawahi hata kupanda gari hilo.


Nionavyo mimi magari hayo yakishapunguzwa, fedha zitakazopatikana baada ya kuyauza na fedha zitakazookolewa kutokana na kupungua kwa gharama za uagizaji na uendeshaji wa magari hayo ambazo serikali imekiri kuwa ni mzigo mkubwa, zielekezwe kwenye kufufua na kuboresha Public Transport system kuanzia Mabasi, City Trains na hata Underground Trains.

Serikali za nchi ya Dunia ya Kwanza-Norway, Sweden, Denmark etc wameinvest heavily kwenye public transport na hawana upumbavu huu tunaoufanya hapa kwetu, serikali imeiacha sekta ya usafiri kwa watu binafsi ambao kimsingi ni WAKUBWA HAO HAO. Unajua tunaweza sema hata uzorotaji huu wa public trasport unafanywa maksudi ili kuneemesha WAKUBWA. Hivi mmeona daladala kwa wenzetu??c huwa mnashinda huko jamani????

Imagine utakuta ofisi moja maofisa 6 wote mnaelekea kwenye Staff quarters zilizopo eneo moja, Kila mtu anatoka na V8 yake kuelekea nyumbani na foleni hizi jaman mbona hamna huruma??????Afu mbaya zaidi jitu linaloendeshwa kwenye hiyo v8 ndo limetoka ofisini kutufanyia ufisadi kwa style ya EPA/DIPGRIN/MEREMETA ETC. Angalieni how Balozi na NGOs za kimataifa zinavyofanya kazi. Mbona hawana utitiri wa magari na bado wapo more efficient kuliko serikali yetu????


Watumishi wa umma ambao watahisi wanahitaji magari ya kuwapeleka ofisini na kuzungusha wake zao saloon wanunue magari yaobinafsi kama wafanyavyo wafanyakazi wa sekta binafsi. Kitu ambacho serikali inaweza saidia ni kuweka utaratibu utakao wawezesha watumishi wake kukopeshwa magari na kupitia mwajiri kama ilivyofanya kwa Wabunge. Nadhani kwa style hiyo serikali haitakuwa na haja ya kutumia maafisa wake wanaolipwa mishahara na kodi za wananchi, kwenda kuwavizia wavunja sheria barabarani ili wawakamate wakiwa wanatumia hovyo rasilimali za umma.

Utaratibu huo utajenga nidhamu tu ya utumiaji wa magari binafsi. Hali hii pia itafanya wananchi kwa ujumla wetu tuibane serikali kutujengea na kuboresha usafiri wa Umma ili utusaidie wote kusave kidogo kinachopatikana. Lakin kwa style hii ya wafanyamaamuzi kutokuonja machungu ya maisha wayapatayo wafanyiwa maamuzi. Hatutakaa tuone efficient transport system in place.

Ili kufikia maendeleo ya kweli, serikali ni lazma ikubali kufanya maamuzi magumu na kuachana na matumizi ya anasa. Serikali itambue kuwa Kukusanya kodi efficiently ni jambo moja na kutumia kodi efficiently ni suala jingine na haya ndo predictors za maendeleo.

Je wewe mwanajamvi waliongeleaje suala hili???
 
Hata hilo la namba za kiraia kwenye gari la serikali 'kwa kibali maalum' ni upumbavu gani huo??? Kibali maalum ili iweje? Kama hao 'wezi' wanaona aibu kutumia magari yenye namba za serikali si wanunue yao? Na unapokuwa na 'kibali maalum' kuna haja gani ya kuwa na namba za serikali? Si wote tu wapewe vibali maalum?! Haya mambo ya kupendeleana haya...Arrrrrrgggh!
 
.........Pamoja na kukamata magari hayo...... dawa moja moja kubwa ni kulazimisha magari hayo yaandikwe kwenye milango kulingana na idara na mahali kwa mfano andika katika mlango.... OFISI YA MKUU WA MKOA KATAVI, OFISI YA MIFUGO SINGIDA..... OFISI YA MKUU WA WILAYA BARIADI...... OFISI YA TAKWIMU BUNDA NAKADAHALIKA..
 
Back
Top Bottom