Agizo la madawati: Halmashauri sita kati ya saba zakamilisha zoezi la utengenezaji madawati Mbeya

Mar 24, 2016
47
27
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla amesema kuwa kati ya Halmashauri saba za mkoa huo, halmashauri ya jiji pekee ndio haijakamilisha zoezi la utengenezaji wa Madawati licha ya kwamba tarehe ya kikomo imepita.


Akizungumza wakati akipokea msaada wa Madati 400 kutoka kwa Kampuni ya uchimbaji wa Madini ya Panda hili Tanzania Limited ambayo inatarajia kuanza kuchimba Madini adimu Duniani aina ya NIOBIUM, amesema Wilaya ya Mbeya ni miongoni mwa halmashauri sita zilizokamilisha zoezi la utengenezaji wa madawati.


Makala amesema kuwa jiji la Mbeya limeshindwa kukamilisha zoezi hilo kwa muda uliopangwa kwa sababu lilielekeza tenda kwa chuo cha Ufundi VETA pekee.


Makala amesema halmashauri hizo zina ziada ya Madawati na kwamba jiji la Mbeya kwa kushirikiana na ofisi yake wamehamisha Tenda kwa mtu Mwingine ambaye atafanya zoezi hilo kwa muda mfupi.

Chanzo muungwana blog
9b5453d21cd4f9956384ea03bc6de4d4.jpg
 
Back
Top Bottom