Agizo la Kurudishwa Kazini Watumishi wa Serikali

MAKWIZI

New Member
Dec 5, 2014
4
0
Habari za asbh wadau! Naomba mwenye kujua kuhusu taarifa hizi "Inasemekana eti watumishi wote wa serikali na mashirika ya serikali waliofukuzwa kwa utoro, ulevi na sababu zingine waliokuwa wamesaini mkataba wa ajira ya kudumu wanatakiwa kurejea kazini ndani ya wiki moja! Inasemekana agizo hilo limetolewa juzi tafadhali kwa mwenye kujua atujuze kwa ufasaha!
 
Makubwa!yani ufukuzwe afu urudishwe,ni kwamba watu wa kuzijaza hzo chance wameisha?
 
Hiki nacho kitakua kituko kingine, yani mtu afukuzwe labda kwa kuiibia serikali halafu tena arudishwe unadhani nini kitatokea? Kama ni kweli basi utendaji kazi utashuka kwa maana unamrudisha mtoro kazini kisha utegemee ufanisi. Labda kwa kua ni Tanzania inawezekana.
 
Mnashangaa nini? Hivi mnadhani kumfukuza kazi mtumishi wa umma ni jambo linaloweza kufanyika kirahisi rahisi? Serikali huwa inashindwa kesi nyingi sana kwa jambo hili na huishia kulipa fidia. Mfanyakazi wa umma anaweza akafukuzwa au kusimamishwa kazi kwa mbwembwe nyingi na fisi nfyele wakafurahia kusoma habari hizo kwenye magazeti, lakini hurudishwa kazini kimya kimya kwa aibu ya serikali. Ulizeni wale wakurugenzi wa halmashauri waliosimamishwa kazi na waziri wa Tamisemi wakati huo bi Hauwa Ghaasiya eti kwa kosa la kuvurunda uchaguzi wa serikali za mitaa. Wamerudishwa kazini kimya kimya na hadi sasa wapo mzigoni. Ajira serikalini ni kama ndoa ya Kikatoliki, haivunjwi kirahisi rahisi
 
Habari za asbh wadau! Naomba mwenye kujua kuhusu taarifa hizi "Inasemekana eti watumishi wote wa serikali na mashirika ya serikali waliofukuzwa kwa utoro, ulevi na sababu zingine waliokuwa wamesaini mkataba wa ajira ya kudumu wanatakiwa kurejea kazini ndani ya wiki moja! Inasemekana agizo hilo limetolewa juzi tafadhali kwa mwenye kujua atujuze kwa ufasaha!

Umesikia wapi hii? Ninachojua kuna kesi nyingi sana za aina hii zinaendelea kwenye tume ya utumishi na wengine Ikulu kabisa. Sema umesikia wapi ili tukisaidie kutrace
 
Habari za asbh wadau! Naomba mwenye kujua kuhusu taarifa hizi "Inasemekana eti watumishi wote wa serikali na mashirika ya serikali waliofukuzwa kwa utoro, ulevi na sababu zingine waliokuwa wamesaini mkataba wa ajira ya kudumu wanatakiwa kurejea kazini ndani ya wiki moja! Inasemekana agizo hilo limetolewa juzi tafadhali kwa mwenye kujua atujuze kwa ufasaha!
Acha kulalamika lete taarifa kamili imesemwa na nani?
 
Mnashangaa nini? Hivi mnadhani kumfukuza kazi mtumishi wa umma ni jambo linaloweza kufanyika kirahisi rahisi? Serikali huwa inashindwa kesi nyingi sana kwa jambo hili na huishia kulipa fidia. Mfanyakazi wa umma anaweza akafukuzwa au kusimamishwa kazi kwa mbwembwe nyingi na fisi nfyele wakafurahia kusoma habari hizo kwenye magazeti, lakini hurudishwa kazini kimya kimya kwa aibu ya serikali. Ulizeni wale wakurugenzi wa halmashauri waliosimamishwa kazi na waziri wa Tamisemi wakati huo bi Hauwa Ghaasiya eti kwa kosa la kuvurunda uchaguzi wa serikali za mitaa. Wamerudishwa kazini kimya kimya na hadi sasa wapo mzigoni. Ajira serikalini ni kama ndoa ya Kikatoliki, haivunjwi kirahisi rahisi
Na wao wamelitambua hili na ndio mana wameona kuna haja ya kuanza kurekebisha sheria za kazi..inakua ngumu kumuwajibisha mfanyakazi asiye muadilifu
 
Hapo hapo naomba kuuliza....kuna mtu alitoroka kazini miaka mitatu iliyopita....akafutwa payroll bila barua yoyote ile....alikuwa mwalimu...Baadae akapata kazi shirika la umma lakini ikawa ngumu kuajiriwa kisa tyri alikuwa na cheki namba....Baada ya hapo aliomba kibali cha kurejea kazini kwa katibu mkuu kiongozi ikulu....
Juzi kibali hicho kakipata na kinatoa maelekezo arudishwe kazini na kinamwelekeza mwajiri wake wa awali ahamishe cheki namba yake kwenda shirika la umma alikopata kazi tena....
Swali langu....kile kibali kinasema aliacha kazi kwa notice ya 24hrs wakati hakufanya hivyo...
Sasa je mwajiri wake wa zamani ana ubavu wa kukataa kutii maelekezo ya kibali cha utumishi makao makuu kwa sababu ya hiyo heading ya kibali???
 
Hawezi kukataa kutii mamlaka iliyo juu yake kwa vyovyote vile ila swali langu ilikuwaje wanaandika uliacha kazi ndani ya masaa 24 baadala ya utoro.
 
Molembe:...Ahsante kwa ufafanuzi wako...kwanini waliandika 24hrs badala ya utoro hilo wanajua wao maana wao ndo wamefanya vetting for almost two yrs na hatimaye kutoa kibali....
 
Hongera mkuu hawezi kukataa maana amepewa amri iliyo juu yake.
 
Da haya mambo ndugu yangu omba yasikukute kabisa kurudi PAYROLL ni mziki mwingine eti kwa waliofanyiwa vetting na kurudi wataungana na mimi ushauri fuateni utaratibu katika kuondoka kazini hasa serikalini . Yataka moyo ila Utumish wanajibu barua zooote hata km ndani ya miaka miwili jibu utalipata tu
 
Habari za asbh wadau! Naomba mwenye kujua kuhusu taarifa hizi "Inasemekana eti watumishi wote wa serikali na mashirika ya serikali waliofukuzwa kwa utoro, ulevi na sababu zingine waliokuwa wamesaini mkataba wa ajira ya kudumu wanatakiwa kurejea kazini ndani ya wiki moja! Inasemekana agizo hilo limetolewa juzi tafadhali kwa mwenye kujua atujuze kwa ufasaha!
Vipi mzee wewe ni mmoja kati yao,hakuna serikali yenye mawazo hasi kama hayo, ulikuwa mlevi nk ukafukuzwa hakuna msamaha wa raisi nyie sio wafungwa
 
Unazijua faida na hasara za kufukuzwa kazi jukwaani hata kama baadaye utarejeshwA kazini kimyakimya kwa aibu ya serikali.
 
Back
Top Bottom