Agizo la CCM utata mtupu; Wadau wahoji iweje chama kiipinge serikali yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Agizo la CCM utata mtupu; Wadau wahoji iweje chama kiipinge serikali yake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 3, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=3][/h]

  Ni kuhusu serikali kushusha bei ya mafuta ya taa

  *Wadau wahoji iweje chama kiipinge serikali yake


  Gladness Mboma na Stela Aron

  SIKU moja baada ya Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuiagiza serikali kutafuta njia za kushusha bei ya mafuta ya taa, Wananchi wa kada mbalimbali wamesema uamuzi huo ni kielelezo kwamba serikali imeparaganyika na inakoelekea ni kubaya.

  Wakitoa maoni yao kwa nyakati tofauti Dar es Salaam jana, aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Profesa Mwesiga Baregu alisema kauli zinazotolewa na serikali na chama, juu ya bei ya mafuta ya taa nchini zinawachanganya Watanzania.

  "Nakumbuka awali, Baraza la Mawaziri lilipokaa lilijadili kuhusu suala la uchakachuaji wa mafuta, ambapo wote kwa pamoja walikubaliana kwamba ili kudhibiti uchakachuaji bei ya mafuta ya taa ipandishwe.

  "Cha kusikitisha leo (jana) katika vyombo vya habari Kamati Kuu ya CCM nayo imezungumzia suala hilo la mafuta na kuitaka serikali kutafuta njia za kususha bei hiyo, kauli hizi zinawachanganya Watanzania, serikali inatoa agizo hili na CCM nayo inatoa agizo, sasa tumsikilize nani?" alihoji.

  Prof. Baregu alisema kuwepo kwa taarifa hizo za mchanganyiko inaonesha dhahiri kuwa serikali imechanganyikiwa, kwani si kwa jambo hilo hata katika suala la umeme pia.

  Alisema kauli hizo zinatokana na viongozi kutokuwa na maelewano au makubaliano ya agizo lipi litolewe, hivyo suala hili la mafuta kubaki kuwa malumbano ndani ya CCM na serikali.

  "Ni kweli bei ya mafuta imekuwa kubwa na kusababisha wananchi wenye kipato cha chini kushindwa kumudu bei ya mafuta, jambo ambalo limekuwa ni hatari na kuleta gumzo kila kukicha nchini," alisema.

  Alisema serikali ilitakiwa kuangalia kwanza suala la kodi ya mafuta yanayotozwa kwa wafanyabiashara na pia faida inayopatikana kwa wafanyabiashara ili kuwepo na uwiano.

  Kwa mujibu wa Profesa Barefu kodi ya mafuta iko juu jambo ambalo pia linaathiri uchumi wa nchi na kufanya maisha ya Watanzania kuendelea kuwa maskini.

  Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF-Bara), Bw. Julius Mtatiro alisema hali hiyo inaonyesha kuwa CCM sasa imechanganyikiwa kutokana na kudakia mambo ambayo serikali yake ilikwishayatolea maamuzi.

  "CCM imechoka kufikiria na ndio maana sasa imechanganyikiwa kutokana na kauli zao za kujichganganya wasipoangalia sasa wanaipeleka nchi vitani," alisema.

  Alisema kauli iliyotolewa juzi na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi (NEC), Bw. Nape Nnauye kuwa serikali itafute njia za kushusha bei ya mafuta ya taa ni ya kinafiki kwa kuwa CUF walikwishatoa kauli hiyo katika mkutano na waandishi wa habari mwanzoni mwa mwezi uliopita.

  Bw. Mtatiro alisema asilimia 86 ya Watanzania wanategemea mafuta ya taa, wengine umeme, hivyo kitendo cha kupanda kwa gharama ya mafuta kinaweza kupandisha munkari kwa Watanzania na kuanza kuleta vurugu.

  "Watanzania wengi wanatumia koroboi ambazo zinatumia mafuta vijijini na mijini, hivyo kupanda kwa bei ya mafuta ya taa ni hatari kwao," alisema.

  Hata hivyo, Bw. Mtatiro aliitupia lawama CCM kwa madai ya kwamba inawathamini wafanyabiashara wakubwa ambao ndio wafadhili wao na hivyo kushindwa kuwachukulia hatua.

  Naye Waziri Kivuli wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw. John Mnyika, alisema Kamati Kuu ya CCM ilipaswa kutoa agizo la kukubaliana na maoni ya Bajeti Mbadala ya Nishati na Madini iliyotolewa na Kambi ya upinzani Julai 15, mwaka huu ambayo ilipendekeza kodi hiyo ifutwe.

  Pia alisema CCM ilitakiwa kuiagiza serikali kuwasilisha muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Fedha katika mkutano wa bunge unaoendelea, ili kupunguza gharama za maisha kwa wananchi kwa kuondoa ongezeko kubwa lililofanywa kwenye kodi ya mafuta ya taa na pia kupunguza kodi zaidi kwenye dizeli na petroli.
   
 2. mjanja

  mjanja Member

  #2
  Aug 3, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nawambia watanzania tuendeleeeee kumwomba mungu ili atuondolee uoga ili 2kija kukaaa mnazi square iwe historia ya mataifa yote ya africa, mana wanahisi tunauoga na tunaipenda amani yao ya kutubuluza.wacha waendeleeeeeeee kijikanyaga 2
   
 3. L

  Luiz JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Serikali ya ccm ikiongozwa na kikwete kwakweli imeoza kama jalala sasa tunaongozwa na neema ya mwenyezi mungu jamani watanzania tutaburuzwa hadi lini na hawa majuha.
   
 4. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2011
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Hiyo ni tactic ya kivita. Ccm wanaunda tatizo makusudi ili baadaye waoneshe wanalitatua ili watu wavutike nao.
   
 5. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,821
  Likes Received: 10,111
  Trophy Points: 280
  naona kama mbeleni kuna mto, daraja ilishakwenda na maji na dereva wetu haoni kuwa hakuna daraja anaendelea kutupeleka huko. Tunapiga kelele kumuamsha labda yumo usingizini lakini hataki kusikia......haya. Tutadumbukia mtoni atuue sote ila tukifikiria kwa mapana yake, kuliko kumpigia kelele huku anatuua wote ni afadhali kumuondoa yeye kwenye usukani ili mwingne atuokoe na umauti huu.
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,535
  Likes Received: 81,957
  Trophy Points: 280
  Watanzania tumeushtukia upumbavu wao. Kikwete kakaa kimya tangu bajeti ilipotangazwa ambayo ilipandisha bei ya mafuta na kusubiri hadi kikao cha CC karibu miezi miwili baadaye ndio kama Mwenyekiti wa CC anaiagiza Serikali inayoongozwa na Kikwete eti ipunguze bei ya mafuta!!!! Kama Rais wa nchi hakuliona hili bali kaenda kuliona akiwa Mwenyekiti wa CC!!?
   
 7. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Umefika wakati tukatenganisha kofia mbili, yaani Mwenyekiti Wa Chama tawala asiwe Raisi Wa Nchi. Yaani ukichukua orodha ya hao wanaoitwa CC ya Chama Tawala utakuta majority ni viongozi Wa serikali kwenye nafasi nyeti
   
 8. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  siasa za watu wajinga huendana namambo yakijinga kijinga kweli jk hakustahili kuwa rais ila alipewa bila kujua maana kuwaza kwake hata sijui kama hata elimu yake ya chuo kikuu inamsaidia au la? Nahuku ni kudhalilisha taaluma nakuendelea kudhalilisha nchi kwa kila hali huwezi subiri kikao cha chama ndio kitoe maamuzi ya kunyanyasa wananachi huku wewe ukiwa unazunguka, au unatalii tu.
   
Loading...