Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 6,273
- 6,637
Kila mtanzania anamkubali Agrey Mwanri kuwa ni jembe na mchapa kazi. Anajua kuongoza, anajua kuwajibika.
Lakini kwanini kiongozi kama huyu hakupata uteuzi ili aweke mambo sawa kwa manufaa ya umma? Je, kuna tatizo kwa washauri wa rais JPM?
Mbona tuna ona watu ambao uwezo wao wa kuongoza ni mdogo na wanaingia kwenye Cabinet?
Hao wanaomshauri Rais wanakula pesa za bure za walipa kodi? Kwanini mtu kama Mwanri awe benchi, alafu watafuta kick za kwenye Tv ndio wanakula uteuzi?