Aggrey Mwanri hakuwahi "kumsukuma mtu ndani", zilikuwa mbwembwe tu

Madumbikaya

JF-Expert Member
Jun 6, 2018
243
1,000
Uongozi ni hekima na busara, Aggrey Mwanri alikuwa mkuu wa Mkoa mwenye vitisho, mikwara sana lakini hakuwahi hata siku moja kumlaza mtu ndani yaani Polisi

Akiwa Tabora alitembelea miradi kwa umakini na ukali wa kutisha huku akisema Polisi kamata mtendaji huyo na Sukuma ndani, Lakini wakifika polisi anawaambia ondokeni mkachape kazi msirudie

Hawa vijana wa sasa sijui vipi hawajui kuishi na jamii

Jakaya Kikwete kuna wakati alikuwa anatukanwa sana na watu, Lakini akiitisha kikao anatoa msamiati mmoja tu wa Pwani watu wote kicheko wanasahau hasira zote za maisha.

Kuna wakati Kikwete watu walimuambia safari hii "JK hachomoki" Yeye alikaa kimya, Alipopata wasaa wa kuongea na watu wake wa Msoga akawauliza ndugu zangu si mmesikia sichomoki kwani Mimi kuna sehemu Nilichomeka mpaka nishindwe kuchomoa.

Kuna wakati wa Magufuli, Mtu alisema Safari hii "Tutawashikisha ukuta polisi" Akafunguliwa kesi ya uchochezi kisa kasema Polisi Tutawashikisha ukuta, Maajabu haya.

Uongozi ni busara, hekima na kuishi kulingana na watu wako wanapenda kitu gani.

Furaha na Amani ni kila kitu Kwa Raia, Tangu Mama Samia aingie madarakani watanzania wanafunguka sana hata vijiwe sasa siasa zimeanza kujadiliwa habari za siasa.

Mwendazake alidhibiti hata kupiga story za siasa kwenye vijiwe vya shoeshine, Ukianza mambo ya siasa watu wana kukimbia unabaki wewe na shoeshiner.
 

That

New Member
Jun 10, 2021
1
20
Hiyoo ndio democrasia kuwapa watu Uhuru wa kuongea mwendazake hakutaka aliona wanamchelewesha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom