KipimaPembe
JF-Expert Member
- Aug 5, 2007
- 1,285
- 696
Jamani kuna trend imeanza kujitokeza hivi karibuni kwa mambo ya kidini kuingia Bungeni. Sheria ya nchi inazuia kuanzishwa kwa vyama vya siasa vyenye mrengo wa kidini. Pamoja na kuwa wanasiasa wana dini, lakini kuifanya dini agenda ya kisiasa, ni sawa na kuanzisha chama chenye mrengo wa kidini.
- Je, iko haja ya spika kuzuia mijadara yenye mwelekeo wa kidini Bungeni au mijadara ya dini iwekewe muda wake kama ilivyo bajeti?
- Ikiwa wabunge wanaweza kujadili mambo yenye mrengo wa kidini bungeni, iko haja viruhusiwe vyama vya kisiasa vyenye mrengo wa kidini ili wakati wa uchaguzi tuwe tunajua kuwa huyu tukimchagua ataenda kutetea dini yetu?
- Iko haja ya kutoa nafasi za ubunge kwa dini zetu ili wenye utaalam wa masuala ya dini waende kuzisemea dini zao bungeni?
- Je bungeni ni mahali muafaka pa kutetea maslahi ya dini? Wabunge huo uwezo wamepewa na nani?
- Je iko haja wabunge wawe wanaleta na hoja za kidini wakati wa uchaguzi ili tujue kuwa bungeni wataenda kutetea maslahi ya dini zetu vile vile?