Agenda ya muungano jmt vs mapendekezo mengine ya marekebosho ya katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Agenda ya muungano jmt vs mapendekezo mengine ya marekebosho ya katiba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kibunago, Mar 5, 2012.

 1. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kutokana na kile kisemekanacho kuwa changamoto au kero za Muungano wetu, Kwa mtazamo wangu na kwa hekima ya kufuata kanuni ya kuanza kinachostahili KWANZA, bila kumungunya maneno namshauri Mh. Samia Suluhu - Waziri wa Nchi- Muungano kuwa:

  Agenda ya Watanzania kuamua WANATAKA MUUNGANO WA AINA GANI ni ya kipekee na ya muhimu wa KWANZA hata kabla ya kuanza kupokea mapendekezo ya jumla ya tuwe na KATIBA YA NAMNA GANI / AU YENYE IBARA NA VIFUNGU GANI.

  Nitoe mfano mbaya:

  Unawezaje kufikiria kupata mapendekezo ya kuweka ratiba za kusafisha nyumba, kununua chakula, kwenda kusali wapi, nani atamiliki au kuwa msemaji wa mali zipi, kubadilisha / kubeba jina la ubini wa mwenza, malipo ya mahari au zawadi kwa wazazi, mambo gani yawe ya binafsi (yasiyoingiliwa na mwenza wako), mpate watoto au la n.k WAKATI HAMJAJUA KAMA MNATAKA KUENDELEA KUWA MARAFIKI WA KARIBU TU, AU KUWA WABIA WA KI-BIASHARA AU KUOANA NA KUWA MWILI MMOJA KATIKA WAWILI?

  WAKATI HUU NI MUHIMU WATU WOTE (WA PANDE MBILI ZA MUUNGANO), TUWEKWE WAZI NASI TUWE WAZI NA TUAMUE JUU YA HILO LINALOSTAHILI KWANZA KWA UWAZI NA BILA JAZIBA NDIPO TUTAHESHIMIANA NA KUPANGA MENGINE YOTE KWA UPENDO NA UMOJA WA KWELI.
  VINGINEVYO KILA KIONGOZI ANAPOULIZWA JUU YA MUUNGANO ANACHOONGEA (TOKA MDOMONI) UNAKIONA WAZIWAZI KUWA NI TOFAUTI KABISA NA MAWASILIANO YA VIIUNGO VYAKE NA HATA HISIA ANAZOZIONYESHA KWENYE KADAMNASI! (The non- verbal repudiates the verbal communications):yawn:.
   
Loading...