Agenda 21 waanza kukutwa na vizuizi...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,463
39,929
Baada ya kuanza kuja kwa nguvu na jitihada za kuanza kumsafisha aliyekuwa Waziri Mkuu na kulirudisha jina lake kwa nguvu kwenye siasa za Tanzania kundi la "Agenda 21" (Soma KLHN juu ya uundwaji wake) wameanza kukutana na magogo barabarani.

a. Jaribio lao la kuingilia JF na kuinyamazisha liligonga mwamba pale Rais Kikwete alipomuita Manumba Ikulu na kuulizia sakata hili. Ilipojulikana ni nani wako nyuma ya "malalamiko" oda ikatolewa "waachilieni!".

b. Jaribio la kuanza kutumia vyombo vya habari kama TVT kujenga jina la Mhe. Lowassa tena ziligonga mwamba siku ya Jumamosi baada ya matangazo yaliyokuwa hewani "kulazimishwa kukatisha mara moja. (Unaweza kuona video zote mbili kupitia KLHN). Baadhi ya watu wanasema kuwa mahojiano yalikuwa yamefikia mwisho ingawa kama ndio interview zinamalizwa hivyo basi tuna kazi mbeleni.

c. Gazeti la "Mtanzania" nao walianza makala yao moja jana ambayo ilikuwa na mwelekeo wa kuendelea leo na ikiwa na lengo hilo hilo la kumsafisha Lowassa mbele ya Watanzania. Makala hiyo nayo inaonekana "imesitishwa" kiana na sitoshangaa jina la Lowassa na utetezi wake ukaanza kupotea mara moja magazetini.

Kinachotokea sasa hivi ni kujulikana kwa mtandao huu mpya ambao una lengo moja kubwa ambalo wengine tulishalisema hapa miezi kadhaa iliyopita - Kumfanya Mhe. Kikwete kuwa Rais wa kwanza kutawala baada ya mhula mmoja. Lengo la hawa jamaa ni kurudi kwa nguvu 2010 na hawana mpango wa kusubiri 2015.

Baada ya habari za kuundwa kwa Agenda 21 kupenya kambi mbili zinaonekana kujitenga. Kambi ya EL na Kambi ya JK zimeanza kutengana wazi. Kitendo cha JK kwenda kutangaza hadharani kujiuzulu na kusababisha "msukosuko" nchini hakijasamehewa na Kikwete na Kundi lake, na hususan Spika Sitta ambaye aliona kuwa "ametegwa".

Na kilichowatubua wengine ni mtindo wa EL kwenda kwao Monduli na kupokelewa kama shujaa na hivyo kujitangaza kwa namna moja kuwa "he is a power to reckon with". Baadhi ya Wafanyabiashara wakubwa wanaomuunga mkono Lowassa wameapa kuhakikisha kuwa analipiza kisasi.

Siku si nyingi zijazo kuna dalili kuwa wajumbe kadhaa wa Kamati Teule ya Bunge ambayo ripoti yake ilisababisha Lowassa ajiuzulu watakuwa walengwa kwa namna moja na kashfa za Benki Kuu. Majina ya baadhi ya wabunge hao ambao na wenyewe walipata fedha za Import Support na nyingine yameanza kutengenezewa kashfa.

Wakati huo huo, upande wa wabunge waliokuwa Mawaziri na baadaye kujikuta nje ya Baraza jipya na wenyewe wanataka kutumia "njia za Kibunge" aidha kusababishwa uundwaji wa "Kamati Teule" itakayohusu suala la BoT ili na wao waweze kukomba wenzao.

Chanzo kimoja karibu na Kuta za majengeo ya "CCM" kinasema kuwa endapo Kamati Kuu ya chama hicho haitakaa chini haraka na kufikiria njia za kushughulikia mgogoro huo unaofukuta CCM inaweza kujikuta katika mgawanyiko usio wa lazima.

Kwa upande mwingine, jitihada za kuizima Jambo Forums na wanachama wake waandamizi bado hazijakoma na kuna habari kuwa "majina kadhaa" ya watu ambao wanahisiwa ndio vinara wa forum hii yamepelekwa kwenye Balozi za TZ US na UK ili kujaribu kuhakiki kama watu hao ndio wenye "kupiga" kelele zaidi kwenye forum hiyo.

Mojawapo wa watu waliohusika na "interrogation" ya vijana wale wawili amesema (kwa masharti ya kutotajwa jina wala cheo) kuwa mojawapo ya vitu walivyokuwa wanavihitaji kujua ni pamoja na financial information, kumjua "Invisible" ni nani na kama JF inaonesha picha za ngono "live".

Pia anasema maafisa hao wa usalama (mmoja inadaiwa alikuwa ni mwandishi wa habari na blogger anayejulikana) walitaka kujua utambulisho wa mwanachama mmoja mwandamizi. Licha ya kupewa namba yake ili wazungumze naye, maafisa hao walikataa kufanya hivyo wakiamini kuwa mwanachama huyo "ana nguvu kubwa" nyuma yake.
 
Huyo mwandishi na blogger ndie yule anayejulikana kimbogamboga? Mtu huwezi kujificha siku zote, kwani lazma utaonekana tu ukielekea Kijitonyama kuchukua payckeck..
 
nikifufuka, hapana siyo huyo ndugu yangu shabiki wa "dimbwi la maini" bali ni mtu mwingine..

DsL.. ndiyo Rais wetu ana kibarua kizito na asipoweza kufanya kile kinachojulikana kama "mizengwe" hataweza kupambana na hii "nguvu kuu".
 
Mzee Mwanakijiji asante sana kwa hizi nyeti. Inaonekana wazi kuwa kutakuwa na mgawanyiko mkubwa ndani ay CCM. Na zaidi, yutashuhudia kuibuka mtandao wa EL akiungwa mkono na Maswahiba wake kwa upand mmoja na wakati huo huo JK na washirika wake upande mwingine.

Kuna gazeti nilisoma last week linalodai kuwa EL ndiye aliyemuibua JK. JK hakuwa na ndoto ya urais amabo inaelekea EL aliutaka sana. Ni EL alimshawishi JK waende wote DOM wakajaribu bahati yao 1995. Na toka kipindi hich walitangaza ubia ambao umekufa kutokana na Richmond Gate.

Tunasubiri kwa hamu kuangalia nini kitafuata. Lakini wakati haya yote yanatokea, ni vema Watanzania wakatafakari kwamba ni nini kifanyike ili hatimaye mambo kama haya yakome.

Hakika nchi yetu ina kila lililojema isipokuwa tu tupo katika Lindi la umasikini. Ni vema sasa ifiki wakati kila moja atimize wajibu wake au la sivyo awajibishwe na sheria zilizopo.
 
Mgawanyiko wa CCM ndio baraka kubwa. Maneno ya JK Nyerere aliyosema Berlin alipoenda kuhudhuria mazishi ya Brandt yatakuwa yametimia. Kwani ukweli ni kuwa upinzani unaotokana na tofauti ya mawazo ya chama tawala huleta uwiano wa kisiasa, tazama CUF-Zanzibar ilivyo na nguvu. Viongozi wa juu wametokana kamati kuu ya CCM zanzibar. Tuombee mvurugano huo ukomae.
 
Naomba Serikali ya SISIEMU, Mafisadi na Kambi ya Lowassa Rostamu na waroho wote ndani ya serikali watulize boli.

Muda ukifika mimi binafsi nitajitokeza hadharani na kusema mimi ni fulani na nina amini itakua hivyo kwa awanachama kadhaa wa JF.

Hayo majina ubalozini wapeleke tu. Ila ole wao ubalozi waanzishe aina yeyote ya unusanusa, tutawafuata hapo hapo ubalozini na kuwacharaza bakora, baada ya hapo tutawaambia wafute machozi waendelee na shughuli zao na kufyata.

Kumfanyia PESONA LAUNDERING MH Lowassa ni gharama ambayo SISIEMU hawawezi kubeba. Ikitokea kwamba wanabeba itawalemea na hivyo wote kama Chama watazama na Lowassa wao.

Lowassa amesahau kwamba Cheo cha Waziri Mkuu ndicho kilikuwa kinampa Thrust ya kuwashukia watu kwa dhoruba na siyo Kodi ya vijumba vyake vya wizi kule Oysterbay na Sakina.
Tukimfikisha Mahakamani, tena kwa kutumia sheria hizihizi na zile za uhujumu wa uchumi, hata kama itachukua miaka 7 kuanzia leo. Lowassa ajue wazi kwamba tutanadi kila kitu kufidia fedha yetu alo tuibia.

Sijui nani anawadanganya watu wenye akili kama ya Lowassa kwamba wao walizaliwa kutawala.

MH Lowassa ile nguvu ilo kuzuia zamani na kukuona wewe ni mla rushwa na mtu hatari unakimbilia ikulu,ambayo ilikuwepo ikatoweka na sasa ipo, imerudi na imetawanyika kwa Watanzania wengi zaidi.

Gharama ya kujisafisha ili uweze kukalia kiti unacho kitamani sana Thamani yake ni kubwa kuliko Uhai wako. Je uko tayari kuutoa uhai wako ili upate nafasi ya kukalia kile kiti unacho kitamani kuliko jambo lolote?
 

1. Hivi kati ya JK na EL kuna tofauti gani hasa ambayo inaweza kutupa matumaini? Kuna yoyote hapa anayeweza kusema...

2. Je kuna yoyote hapa anayewaamini kwa dhati hawa waheshimiwa wawili kama viongozi makini wa Tanzania?
 
Gharama ya kujisafisha ili uweze kukalia kiti unacho kitamani sana Thamani yake ni kubwa kuliko Uhai wako. Je uko tayari kuutoa uhai wako ili upate nafasi ya kukalia kile kiti unacho kitamani kuliko jambo lolote?


Lowassa ana malengo...watch this space; Tanzania media na CCM wakiendekeza unafiki wao huu wanaouonyesha sasa...atafanikiwa malengo yake.
 
Bottom like is,as Waswahili wasemavyo,USHIRIKA WA WACHAWI HAUDUMU.Mbinu nyingi chafu zilitumiwa na wanamtandao kuhakikisha wanachukua madaraka 2005.At that time,nobody forecasted the possibility of the Mtandao kuja kuwa dude kubwa lisilodhibitika.It started with Mtandao Maslahi and Mtandao whatever.The people in the know claim that the reasons behind mgawanyiko huo wa mtandao at that time are 2:those who thought they were "forgotten" ie hawakuambilia chochote licha ya mchango wao mkubwa katika mafanikio ya mtandao kuingia ikulu.And second,Lowassa's aspirations to become JK's successor (at that time,he was complying with the "informal timetable" that his chance would come in 2015).

Came a time when Migiro vacated Uwaziri wa Mambo ya Nje (a post Lowassa's camp thought would fit someone unpopular,with no presidential ambitions,and would pose no stumbling block to EL's road to Ikulu).Rumours had it that EL was opposed to Membe's nomination because he thought the guy,being as close JK's friend as he-EL-is,could turn the table against him-EL).Open hostlity began to emerge in the open,and rumours started flowing that EL had broken the "informal pact" that his turn would come in 2015.

Wakati hayo yote yakiendelea chinichini,ukaja uchaguzi wa CCM dodoma.Inasemekana perfomance ya EL haikuwa impressive,and that created a feeling that ile pact ya "subiri mpaka 2015" inaelekea kuvunjika.Though I have never heard of the Agenda 21 before,I can make an assumption that huo ndio wakati timu hiyo ilipoundwa au kujipanga vizuri zaidi.

El knows that if JK didnt want him to go,he could have easily done that but he chose not to.That signalled the "burial" of the "informal pact."From that moment on,strategy imekuwa ni kuhakikisha EL anaingial Ikulu 2010 come what may.

Nyerere alitabiri kuwa upizani wa kweli utatoka ndani ya CCM.What he didnt know was one day EL would become such an influential figure in CCM "nasty" politics.Ni kweli kuna dalili ya kuzaliwa upinzani mpya,lakini hautakuwa wa kweli kama alivyobashiri Mwalimu.Huu utakuwa upinzani wa maslahi,na mbovu kuliko ule uliosambaratisha NCCR ya Mrema.

Kama JK yuko serious,now is the time to stop huyu Mmasai ambaye anasifika kwa kutanguliza emotions infront of commonsense.Trust me,kuna mengi yatakayojiri between now and 2010.EL has so far decided that he would become the next TZ President by any means neccessary.Kama wapinzani wako makini,hii ni fursa nzuri zaidi ya zote kuwaacha mafahali wakigombana na wao kujichukulia madaraka kiulaini.Unfortunately,there's a possibility that the EL's camp would solicit help from the Opposition camp to clear its (EL's) way to Ikulu.

Kufanya jitihada za pamoja kuhakikisha mmoja kati ya marafiki wawili anampa demu bomba is one thing,kuvumilia kuona rafiki anatanua na demu huyo baada ya efforts za pamoja kumpata is another.And that's exactly what we are witnessing now.

As to mapambano dhidi ya JF,any sane person would understand that kama Sokoine,Katabaro and other were eliminated simply because they fought for wananchi,then JF is an ultimate pinch in the shit hole that every fisadi would love to see it gone.Tunapojadili mada nzito tunaweza kujisahau kwamba wenzetu tulionao hapa ambao hata kama wanaunga mkono vita zetu dhidi ya ufisadi,wapo hapa kujua nani ni nani.Angalau akina mugongomugongo au tafiti then jadili walijiweka bayana kuwa wao wako upande gani.Ni vema,therefore,kuchukua tahadhari muhimu kuhakikisha kwamba upendo wetu kwa taifa letu,which is synonymous to kutia mchanga kwenye vitumbua vya mafisadi, hakuishii kuharibu maisha yetu binafsi.Ukiwa open-minded na conscious of ID fraud kwenye net,then watu wanaweza kulala kwenye net kusaka id yako without any success.Lakini la muhimu ni kwamba gharama za kumkomboa mtanzania ni kubwa sana,na zinahitaji wale tu ambao wanaamini kwenye cause hiyo (and I belive most of us do).Sudden soft tone ya DCI and his co dhidi ya "magaidi wa JF" isichukuliwe lightly.
 
jk inabidi awe very careful, sababu nadhani amesahau ambition za watu hawa.

issue kubwa ni kuwa cc composition imejadiliwa na hawa mafisadi na bila aibu wamedai kuwa lifespan iko upande wao. read btn the lines. mfumuko mkubwa uko njiani na lazima jk awe full engaged kutulinda watanzania wote maana hawa watu shida ni pesa na power, usalama earn ur keep now.
 
nikifufuka, hapana siyo huyo ndugu yangu shabiki wa "dimbwi la maini" bali ni mtu mwingine..

DsL.. ndiyo Rais wetu ana kibarua kizito na asipoweza kufanya kile kinachojulikana kama "mizengwe" hataweza kupambana na hii "nguvu kuu".

Nguvu kuu iliyoshindwa uchaguzi wa kiteto?
 
Moelex23,
Upo right kabisa mkuu, yaani JK awe makini haswa. Hapa Mkuu nipo naye JK tena bega kwa bega kwani hawa jamaa wamepania kishenzi na wakishinda ni utumwa kwetu sote. Hii vita inabidi ipate mwelekeo mpya!
Hawa Mafisadi wanaijua ari ya JK, kasi yake na nguvu zake..kiasi kwamba ukweli unatosheleza kusema lifespan ipo upande wao.
Na swala hili akiendelea kufikiria kuwa ni magazeti na maneno ya vijiweni basi tumekwisha.
Majuzi nilikuwa nikitazama Hotuba za Mama Clinton akizungumzia majukumu ya rais. Moja wapo ni kuwa tayari kufikiri na kutoa maamuzi ya msingi within few hours na hivyo kumkandya Obama. Kwa maneno hayo nikamfikiria JK wetu ambaye huchukua miezi kama sio mwaka kufikiria jambo zito la kitaifa kama hujuma za Uchumi wetu..

Ndipo nilipokubaliana na Mwalimu kuwa kweli Ikulu sii lelemama, ni maamuzi kama hayo magumu ya mazito ambayo unatakiwa kuyafanya huku ukimtazama mtu machoni...JK ameshindwa kuyafanya hayo na maadam hawa jamaa wako huru na wameisha jipanga basi amekwisha....
 
Kisa chako kirefu kinaonesha kukiri kwako kuwa JK anafanya shughuli zake ipasavyo.
 
SteveD, sijaelewa unauliza nini Dar, jibu la kauli yako hapo chini ni "hapana" kwani kama angekuwa anafanya mambo barabara, tusingefika hapa!!
 
kama kikwete kweli anataka Lowasa asirudi kwa kasi zote kwenye siasa, na amfungulie mashitaka pamoja na wenziwe kuhusiana na kesi ya Richmond, akimuonea huruma ataaibika yeye siku za usoni.
kikwete kakaa kama hajui kama ukitaka kumuua nyani usimuangalie machoni??!!
 
SteveD, sijaelewa unauliza nini Dar, jibu la kauli yako hapo chini ni "hapana" kwani kama angekuwa anafanya mambo barabara, tusingefika hapa!!

Kumbuka ana miaka miwili na anasafisha madudu ya zaidi ya miaka 40 iliopita, ina maana waliotufikisha hapa si yeye bali ni hao waliomtangulia au sio?
 
Nimefuatilia kwa makini mdahalo huu unaosisimua. Jamani kumbukeni TZ ipo Afrika. Aliyeko madarakani katika nchi zetu za Afrika anakuwa ndio kila kitu; Indeed Rais ndio taasisi yenyewe, ndio nchi. Kitakachompata LK na kundi lake kitawakatisha tamaa wengine wote wenye wazo kama lao. Kwanza kumbukeni kauli ya Pinda jana/juzi kuhusu kuwashughulikia wote waliosaini mikataba bomu. Ni ishara kwamba kuna rungu linashukia watu very soon.

Anachotakiwa kufanya JK sasa hivi sio kusubiri au kuendelea kuunda tume juu ya tume. Ni kufanya zengwe la nguvu. Ni mizengwe tu sasa ndio itakayomuokoa (quote mwanakijiji). Afanye kama Nyerere alivyowafanyia kina Jumbe, Fundikira, Kasela Bantu, ....and the list goes on.

Mwanakijiji naomba kukuuliza swali; Hivi Mkapa yuko upande gani kwenye hii sinema? Tusijekum-underestimate! kwa sababu na yeye ni fisadi anayesubiri zamu yake ifike ili naye ajibu maswali. Anaweza kuwa neutral kweli? Sidhani!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom