Agenda 21 waanza kukutwa na vizuizi...

Nadhani kimewauma kuuliza swali very simple na mnaanza kutoa shutuma zisizokuwepo, poeni moto, JF si ya kwa watu fulani tuu, usinibabaishe kwa kuwa sijui nimeingia juzi, kuingia JF si lazima uchangie. Hakuna kutishana hapa. Toa hoja ujibiwe kwa hoja majungu na chuki zenu ndizo zinazowarudisha nyuma mpaka kauchaguzi ka kiteto mmekakosa. Wapi nilipo pick a fight with mwanakijiji? show me please.

Kama JF inategemewa ni kuwa ya watu aina fulani tu, si liwekwe wazi hilo, sisi tunajua hapa kuna watu wa itikadi tofauti na kila mmoja na mtazamo wake, jee kinacho wauma ni nini?

Of course JF ni ya watu flani: WAZALENDO wanaosababisha MAFISADI wakose usingizi.Unadhani ingekuwa mouthpiece ya Mafisadi ingekumbana na matatizo yaliyotokea majuzi?
Halafu kama unafahamu kuwa kuingia JF sio lazima uchangie then hakuna dhambi kukaa kimya tunapowakoma nyani giladi mafisadi unaoelekea kuwatetea.Anyway,walijaribu wenzio wakashindwa...haya maji ya kina kirefu,sio swimming pool hii.Remember,still water runs deep.
 
Tatizo langu ni matumizi ya jina" Agenda 21" katika hii ishu. Agenda 21 inayohusika na sustainable development haipaswi kutumiwa hivi. Inaonyesha tusivyokuwa makini na masuala ya mazingira na sustainable development (kiswahili chake kimenipiga chenga). Mantiki ya ktumia jina hili hapa hata siioni. Naomba litafutwe jina lingine.
 
Tatizo langu ni matumizi ya jina" Agenda 21" katika hii ishu. Agenda 21 inayohusika na sustainable development haipaswi kutumiwa hivi. Inaonyesha tusivyokuwa makini na masuala ya mazingira na sustainable development (kiswahili chake kimenipiga chenga). Mantiki ya ktumia jina hili hapa hata siioni. Naomba litafutwe jina lingine.

Fundi bila ya wewe kujua, utakuwa umetupa jibu ambalo kwa wiki kadhaa limekuwa likitukimbia.. kwanini hawa watu wajiite hivyo? (siyo mimi niliyewapa jina hilo). Ila kutokana na maelezo yako.. naanza kuona mantiki yao...sustainable...
 
Agenda 21 is a programme run by the United Nations (UN) related to sustainable development. It is a comprehensive blueprint of action to be taken globally, nationally and locally by organisations of the UN, governments, and major groups in every area in which humans impact on the environment. The number 21 refers to the 21st century.
 
Of course JF ni ya watu flani: WAZALENDO wanaosababisha MAFISADI wakose usingizi.Unadhani ingekuwa mouthpiece ya Mafisadi ingekumbana na matatizo yaliyotokea majuzi?
Halafu kama unafahamu kuwa kuingia JF sio lazima uchangie then hakuna dhambi kukaa kimya tunapowakoma nyani giladi mafisadi unaoelekea kuwatetea.Anyway,walijaribu wenzio wakashindwa...haya maji ya kina kirefu,sio swimming pool hii.Remember,still water runs deep.

Hakuna anaekataa wala kupinga kuwa ufisadi upo na ulikuwepo lakini cha msingi ni kuwa JK anaushughulikia na hakuna awamu iliyoonyesha kwa vitendo kushughulikia ufisadi kama hii ya JK. Kwa hilo inabidi apewe sifa na kila ushirikiano iwe ni kutoka kwa kila mpenda maendeleo na mzalendo wa kweli bila kujali itikadi zake kichama.

Yaani mema yote anayofanya JK hayaonekani au ni unazi tu?
 
Wamefikia wapi katika jitihada zao?

Wamefikia pazuri sana nionavyo mimi kama vile
-Uchunguzi bado unaendelea
- Wahusika kupewa barua za onyo badala ya kuwajibishwa
- Kuto tajwa kwa namna yoyote ile kwa kwa mr 'air uchumi' kuhusu hatua
zilizo chukuliwa zaidi juu yake kuhusiana na richmondule na badala yake
kuingiza dhana kwamba aliwajibika kisiasa na si kama mtuhumiwa/mhusika
- Kubariki mapokezi ya kishujaa waliofanyiwa mafisadi wakitumia hela zetu walizotufisadi
 
Wamefikia wapi katika jitihada zao?

Mwanakijiji na Rwebaguri,


Kazi imefika pazuri kwao na pabaya kwa watanzania. Hawa jamaa baada ya kuonewa soni na JK sasa hivi wameweza kumuonyesha kuwa hatima ya urais wake iko mikononi mwao. Kupitia makuwadi wao katika sekta ya habari na vyombo vyao wanavyoanzisha kama uyoga sasa kwa kutumia mapat ya ufisadi wao wameweza kumlazimisha JK kuwa na wasiwasi sana kuhusu uwezekano wa kumpinga katika mchakato wa kuelekea uchaguzi wa 2010 ndani na nje ya CCM. Hii imefanikiwa kwa upande wao kutokana na kuweza kutumia miaka miwili ya UWAZIRI MKUU wa MLINDA MLANGO WA UFISADI kuweka ama kujidai kuwaweka vikuwadi vyao vingi katika ngazi mbalimbali za maamuzi ya chama chao. Hilo limefanikiwa wakati wa kuteua makatibu wa chama wa wilaya na mikoa, wakuu wa wilaya, wajumbe wa NEC na mkutano mkuu na sasa mpambano upo katika jumuiya za chama.

Hali hiyo inasaidiwa zaidi na kukua kwa umaarufu kwa walioshindwa katika mchakato wa 2005 kutokana hali ya mambo sasa pamoja na JK kuwaudhi wajumbe wa CCM kwa kutaka kuwashurutisha serekali ya mseto na mahasimu wao wa CUF kumefanya hali kubadilika ambapo sasa JK yuko makini zaidi na jinsi ya kuhakikisha hajilipui kabla ya kupata baraka za wanachama wake 2010 na hilo likipelekea kufanya maamuzi ambayo yanaonyesha picha ya kukubali umuhimu wa MAFISADI kwa survival ya URAIS wake.

Sasa kuna hili la ZUMA na wafuasi wake walilomfanyia MBEKI. Kwa kiasi fulani linashabihiana na style ya JK kulazimisha ushindi mwaka 2005 ndani ya CCM ingawa kwa upande wao hali imeenda kwa mwendo mkali zaidi ya walivyotaraji. JK ni lazima litamuogofya zaidi na hivyo kumfanya aendelee "kuwaonea soni" maadui wetu wa ndani yaani WADAU WAKUU wa ufisadi nchini.

Yote haya yanaonyesha kuwa jamaa wanaelekea kushinda. Ni uthubutu wa watanzania tu kumshurutisha kuchukua hatua za haraka na zinazoonekana ndio zitaiokoa hatima ya Tanzania mikononi mwa hawa manyang'au wanaoendelea kujikita katika nafasi za utawala za nchi yetu....

Kwa kifupi hali ni tete na inayohitaji hatua za haraka sana. hali hairuhusu ninyi na mimi kuendelea kujificha tulipo na kuendelea kubweka nje ya nyumba wakati MANYANG'AU wanaendelea kugongeana glasi wakati wakimalizia kubomoa misingi yote ya utanzania wetu.....

Katu JK haliwezi hili kwani amekwishachelewa sana na hana uthubutu unaohitajika kwa hili na bahati mbaya kwa sasa anaamini hivyo.....

Tanzanianjema
 
Pana huyu mhariri wa RAI na waandishi waandamizi wa kampuni inayomilikiwa na RA, hivi hawa inawezekana wakawa ni wahusika wa huu mpango, naomba ufafanuzi tafadhari.



KINYESI KILICHOKAUKA KITABAKI KUITWA KINYESI NA WALA HAKITAITWA ANDAZI
 
Pana huyu mhariri wa RAI na waandishi waandamizi wa kampuni inayomilikiwa na RA, hivi hawa inawezekana wakawa ni wahusika wa huu mpango, naomba ufafanuzi tafadhari.



KINYESI KILICHOKAUKA KITABAKI KUITWA KINYESI NA WALA HAKITAITWA ANDAZI

Hao ni sehemu tu ya mkakati mzima, na wakati tunasema watashindwa sasa wamefanikiwa kubadili mawazo na muelekeo wa watu. Wamewaweka Chadema mahali wanapoweza kuwachanganya wasiwasakame, wameviweka vyombo vya habari mahali pa kuchanganyana wasipate wa kuwaandama, wameweka watu wao hapa JF ili mada nzito zivurugwe ama zisijadiliwe, halafu sasa wanamuandaa Zuma wao ili siasa zibadilike na MAFISADI waibuke mashujaa.

Kwa wanaoona kama hayo hapo juu ni NDOTO waangalie, hayo yalisemwa februari 2008 na sasa hii ni septemba mambo yanaonekana wazi wazi hakuna siri kwamba mafisadi wamejipanga kukabiliana na wimbi la kuwavuruga.

Sasa watu wanaona ndoto kwa mafisadi kuibuka kidedea wanashindwa kuangalia alama za nyakati jinsi watu na taasisi zinazopinga ufisadi zinavyoandamwa na bado mikakati ya nguvu inaendelea.

Wanasema mazingira ya Afrika Kusini na Tanzania ni tofauti, YES ni tofauti na ndio maana yatakayotokea hapa yatakuwa tofauti lakini lengo litakuwa kuhakikisha MAFISADI wanaweka serikali yao. Hawatakubali kufanya makosa waliyofanya kwani sasa wamejiandaa kikweli kweli.

Jambo la msingi ni kutokata tamaa kuanzia ngazi ya kaya na hata humu ndani ya 'nyumba' yetu ya JF. Kinyume chake ni Taifa kuangamia mikononi mwetu.
 
Currently Active Users Viewing This Thread: 22 (9 members and 13 guests) Halisi, badonipo, fidel80, gagnija, malila, mamaparoko, Realist, Shakazulu, Tshala
 
Currently Active Users Viewing This Thread: 22 (9 members and 13 guests) Halisi, badonipo, fidel80, gagnija, malila, mamaparoko, Realist, Shakazulu, Tshala

Sasa imekuwaje mpaka unawapost hawa wanaoangalia thread?
 
Muhimu angalia siku zote ukiona wageni (guests) ni wengi kuliko wenyeji (members) ujue kuna watu wako kazini

Tena unakuta wamestuana kwa sms kuwa "hebu fungua JF kuna thread inasema kadha kadha kadha"!
 
Tena unakuta wamestuana kwa sms kuwa "hebu fungua JF kuna thread inasema kadha kadha kadha"!

Umenipata kaka Kithuku, lakini nini maana ya Agenda 21? Kuna wanaosema ni Agenda 2010 lakini wameondoa hizo sifuri kupata maana ya kisayansi kama wanavyosema kina "Sheikh Yahya" kwamba kimahesabu ya kinajibu sifuri hazihesabiwi hata kama ziko katika hesabu kwa hiyo 2010 kinajimu ni 21. Tusubiri tuone. KWa waasisi wa Agenda 21 kama wana mapenzi mema na nchi yetu (wako humu JF), watuambie maana yake na si hiyo ya kusikia vipembeni.
 
Kijarida chenu cha "Cheche" Jumatano kitaibua hatua inayofanywa na Agenda 21 kama tulivyotabiri mwezi Februari. Unaweza kusoma juu ya kuundwa kwa kikundi hiki kwenye KLHN eneo la "Headlines" nenda hadi ukurasa wa 95; jinsi tulivyoripoti miezi saba iliyopita leo hii.
 
Back
Top Bottom