Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,672
- 40,549
Baada ya kuanza kuja kwa nguvu na jitihada za kuanza kumsafisha aliyekuwa Waziri Mkuu na kulirudisha jina lake kwa nguvu kwenye siasa za Tanzania kundi la "Agenda 21" (Soma KLHN juu ya uundwaji wake) wameanza kukutana na magogo barabarani.
a. Jaribio lao la kuingilia JF na kuinyamazisha liligonga mwamba pale Rais Kikwete alipomuita Manumba Ikulu na kuulizia sakata hili. Ilipojulikana ni nani wako nyuma ya "malalamiko" oda ikatolewa "waachilieni!".
b. Jaribio la kuanza kutumia vyombo vya habari kama TVT kujenga jina la Mhe. Lowassa tena ziligonga mwamba siku ya Jumamosi baada ya matangazo yaliyokuwa hewani "kulazimishwa kukatisha mara moja. (Unaweza kuona video zote mbili kupitia KLHN). Baadhi ya watu wanasema kuwa mahojiano yalikuwa yamefikia mwisho ingawa kama ndio interview zinamalizwa hivyo basi tuna kazi mbeleni.
c. Gazeti la "Mtanzania" nao walianza makala yao moja jana ambayo ilikuwa na mwelekeo wa kuendelea leo na ikiwa na lengo hilo hilo la kumsafisha Lowassa mbele ya Watanzania. Makala hiyo nayo inaonekana "imesitishwa" kiana na sitoshangaa jina la Lowassa na utetezi wake ukaanza kupotea mara moja magazetini.
Kinachotokea sasa hivi ni kujulikana kwa mtandao huu mpya ambao una lengo moja kubwa ambalo wengine tulishalisema hapa miezi kadhaa iliyopita - Kumfanya Mhe. Kikwete kuwa Rais wa kwanza kutawala baada ya mhula mmoja. Lengo la hawa jamaa ni kurudi kwa nguvu 2010 na hawana mpango wa kusubiri 2015.
Baada ya habari za kuundwa kwa Agenda 21 kupenya kambi mbili zinaonekana kujitenga. Kambi ya EL na Kambi ya JK zimeanza kutengana wazi. Kitendo cha JK kwenda kutangaza hadharani kujiuzulu na kusababisha "msukosuko" nchini hakijasamehewa na Kikwete na Kundi lake, na hususan Spika Sitta ambaye aliona kuwa "ametegwa".
Na kilichowatubua wengine ni mtindo wa EL kwenda kwao Monduli na kupokelewa kama shujaa na hivyo kujitangaza kwa namna moja kuwa "he is a power to reckon with". Baadhi ya Wafanyabiashara wakubwa wanaomuunga mkono Lowassa wameapa kuhakikisha kuwa analipiza kisasi.
Siku si nyingi zijazo kuna dalili kuwa wajumbe kadhaa wa Kamati Teule ya Bunge ambayo ripoti yake ilisababisha Lowassa ajiuzulu watakuwa walengwa kwa namna moja na kashfa za Benki Kuu. Majina ya baadhi ya wabunge hao ambao na wenyewe walipata fedha za Import Support na nyingine yameanza kutengenezewa kashfa.
Wakati huo huo, upande wa wabunge waliokuwa Mawaziri na baadaye kujikuta nje ya Baraza jipya na wenyewe wanataka kutumia "njia za Kibunge" aidha kusababishwa uundwaji wa "Kamati Teule" itakayohusu suala la BoT ili na wao waweze kukomba wenzao.
Chanzo kimoja karibu na Kuta za majengeo ya "CCM" kinasema kuwa endapo Kamati Kuu ya chama hicho haitakaa chini haraka na kufikiria njia za kushughulikia mgogoro huo unaofukuta CCM inaweza kujikuta katika mgawanyiko usio wa lazima.
Kwa upande mwingine, jitihada za kuizima Jambo Forums na wanachama wake waandamizi bado hazijakoma na kuna habari kuwa "majina kadhaa" ya watu ambao wanahisiwa ndio vinara wa forum hii yamepelekwa kwenye Balozi za TZ US na UK ili kujaribu kuhakiki kama watu hao ndio wenye "kupiga" kelele zaidi kwenye forum hiyo.
Mojawapo wa watu waliohusika na "interrogation" ya vijana wale wawili amesema (kwa masharti ya kutotajwa jina wala cheo) kuwa mojawapo ya vitu walivyokuwa wanavihitaji kujua ni pamoja na financial information, kumjua "Invisible" ni nani na kama JF inaonesha picha za ngono "live".
Pia anasema maafisa hao wa usalama (mmoja inadaiwa alikuwa ni mwandishi wa habari na blogger anayejulikana) walitaka kujua utambulisho wa mwanachama mmoja mwandamizi. Licha ya kupewa namba yake ili wazungumze naye, maafisa hao walikataa kufanya hivyo wakiamini kuwa mwanachama huyo "ana nguvu kubwa" nyuma yake.