Agawa dozi kwa waandishi wa habari

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
JANA mganga wa tiba za asili kutoka mkoani Mwanza, Mhangwa Hela, anayedai kutibia magonjwa sugu alijitokeza mbele ya wanahabari kutangaza dawa na kisha kugawa dozi ya dawa hiyo kwa waandishi wa habari waliokuwa tayari kunywa dawa hiyo.
Hela aliitisha mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuitangaza dawa hiyo ambayo anadai kutibu maradhi sugu na kuongeza idadi ya wataalamu wanaotibu maradhi sugu nchini.

Tukio hilo la aina yake la kugawa dozi kwa waandishi lililotokea ndani ya Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) alipokwu kizungumza nao ikiwa ni sehemu ya kuitambulisha dawa hiyo.

Dawa hiyo imethibitishwa na asasi ya utafiti isiyo ya kiserikali Tanzania Medicinal-Plant Foundation (TMF) yenye namba za usajili 00NGO/0004482 (TMF) na kufika mbele ya wanahabari kuitngaza.,
Mganga huyo alisema huduma yake ya dawa inatozwa kwa gharama ya shilingi 1000
 
Na bado safari ni ndefu hadi watz tutakapojua ukweli juu ya dawa hizi zinazo ibuka kama uyoga wengi tutakuwa tumeshadhurika
 
Ndugu mashikolomageni, bado hujaumwa sawasawa na ukatelekezwa na serikali yao uliyoichagua. Wacha wanaoumwa wakajaribu bahati yao kwani serikaliimewatelekeza. Hata waziri Mkuu (Mtoto wa mkulima aliyevaa suti) -Pinda alisema acha watu wakatimize imani zao:bange::bange::israel:habari ndiyo hiyoooooo!!!!!!!!!!!!!!
 
haya :majani7: yatanipoteza maana mie nilijua dozi kwa maana ya mkong'oto/kipigo/kichapo.
 
Back
Top Bottom