Aga Khan Hospital toeni tamko, la sivyo hatuwaamini tena!

SirBonge

JF-Expert Member
Jul 18, 2010
378
435
Aga khan ni hospitali kubwa inayoaminika sana Dunia nzima kwa huduma nzuri na pia hasa ni kwa watu wenye uwezo (kwani huduma zao ni za ghali).

Ninaposhindwa kuelewa ni pale mliposhindwa ku'diagnose malaria kwa Mhe Zitto Kabwe achilia mbali hiyo chronic sinusitis. Je hili ni kweli au Muhimbili waliingiza siasa tu kuficha ukweli wa ugonjwa unaomsumbua?

Tunajua malaria ni ugonjwa rahisi sana kuugundua kwani hata dispensary za vichochoroni hazishindwi inakuwaje nyie mlio kwenye ngazi za kimataifa?

Wananchi tutafurahi sana kusikia ripoti toka kwenu la sivyo HATUWAAMINI TENA kwani hakuna mtakachoweza kama Malaria mmeshindwa!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom