AG Werema alishastaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria

werema hakuwa jaji mkuu alikuwa mwanasheria mkuu nadhan umechanganya kidogo na anatakiwa kustaafu October 2015
 
inaonekana wewe ni moja kati ya watu ambao hesabu zimewapitia mbali kabisa kwa sababu mwaka 1955 +60=2015
 
Makubwa haya. Vituko haviishi nchi hii. Eti kajiuzulu. M2 anayejiuzulu huwa anapongezwa kwa UTUMISHI WA UADILIFU NA UAMINIFU kweli?
 
Unakuwa kilaza halafu unatumia ukilaza wako kutaka kupotosha umma.
Ukiachilia mbali barua aliyomuandikia Rais ni ya kujiuzulu hata huo umri wa miaka 60 haujatimia.
Hebu karibuni kuficha upumbavu wenu.
 
Yaani bonge la changa la macho!! Anazidi kuendeleza unafiki,na tusishangae siku moja akapewa nishani ya kiongozi bora aliyeachia madaraka mwenyewe.
Elli njoo huku ushangae
hahahaa nilikua nawaza almost the same kuwa kuna siku atapewa Ubalozi tu, trust me or not tena ni kabla ya JK kutoka madarakani, kama atatoka.
 
Osaka Ndugu yangu soma taratibu na uelewe. hakuna haraka yakurukia kwenye kucomment wakati hujaelewa mada yenyewe.

Mwache huyo na majazba yake, kujua kusoma ni kitu kimoja na kuelewa kile unachokisoma ni kitu kingine tofauti. Una habari hata mwanafunzi wa chekechea anaweza kusoma ila asiweze kuelewa?

Mimi nimekuelewa.
 
mkuu naona mwaka aliozaliwa hujauhesabu

Mmmmm another Mulugo ha ha ha. Hata wanaosoma nutrition needlework wanajua kwamba 60th aniversary ya huyo Muraa ni October, 2015. Hivi hakuna uwezekano wa kufanya fact findings kabla ya kuweka mada kwenye Jukwaa jamani eee?. This is pathetic.

Lakini pia Werema ni Judge. Umri wa kustaafu wa lazima kwa majaji ni 65 years. Judge anaweza ku-retire kwa hiari at 60. Someni kabla hamjaweka hoja hapa. Hili ni jukwaa la GTs basi li-reflect ukweli huu.
 
Mkuu mambeza,unakumbuka Jaji Mkuu na hata Mwanasheria Mkuu Mwanyika alistaafu? Halafu Mkuu,Profesa unayemtaja hakuwahi kuwa mwajiri. Yawezekana nimekuzidi ufaulu na elimu. Kubali matokeo Mkuu

Nnimekuuliza kanuni za utumishi katika nafasi za uteule kama AG katika kustaafu zinasemaje .......???? Wewe kama mwanasheriaa......????!!!!!! Halafu unakimbilia ufaulu.....????? Najua profesa mbunda sio mwajiri......iii ila ukweli unaujua kuhusu Yeye na Hapo ulipo. Nijibu hio ishu ya kwanza mselewa ?????
 
Last edited by a moderator:
Jamaa wamechemka! Mfanyakazi wa Serikali anayetuhumiwa kwa jambo lolote, na kwakuwa kamati maalumu inachunguza suala lake basi hakupaswa kujiuzulu!

Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Jaji Fredrick Werema amezaliwa tarehe 10 mwezi wa Oktoba mwaka 1954. Kimahesabu na kisheria,Jaji Werema alistaafu tarehe 10 mwezi wa Oktoba mwaka 2014.

Imewezekanaje ajiuzulu jana? Kwanini sasa na si wakati wa kustaafu? Mstaafu ajiuzulu kweli!?
 
Kazi aliyokuwa anaifanya Werema ni AG siyo ujaji. Kama angekuwa mahakamani ni sawa, lakini hii ni kazi nyingine.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom