AG: Vyombo vya habari vinashabikia wanasiasa bila utafiti! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

AG: Vyombo vya habari vinashabikia wanasiasa bila utafiti!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Nov 7, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Gazeti la Majira la leo limeripoti ya kuwa Mwanasheria MKuu Bw. Werema akivisigina vyombo vya habari vya hapa nchini kwa kuwashabikia wanasiasa katika uchaguzi huu bila ya kufanya utafiti..........HIi yaamanisha wanasiasa hao walishindwa kwenye chaguzi hii!!!!!!!!!!!

  Kauli hii imekuja siku ambayo JK ameapishwa katika uchaguzi ambao wengi tunaamini Dr. Slaa wa Chadema ndiye aliyeshinda kinyang'anyiro hicho tena kwa kishindo kizito................

  Ukifuatilia kwa karibu nyendo za wateule wa JK utaona kuna jitihada za makusudi za kumbeza Dr. Slaa kuwa si kipenzi cha watanzania walio wanyonge...........wakati siyo kweli na kumwinua JK kinyume na matakwa ya wengi...........

  Kabla ya hapo Lowassa alitoa waraka mzito ambao ulilenga kumbeza Dr. Slaa kuwa bado hajazijua vyema siasa za nchi hii mbali ya ukweli kuwa Dr. Slaa amekuwa mbunge wa jimbo la Karatu kwa miaka 15.........................

  Pia mtoto wa JK - Ridhiwani akifuatiwa na Rostam Aziz vile vile walimbeza Dr. Slaa kwa kuhoji juu ya tuhuma za kuwa walishirikiana na JK katika kikao kimoja kule MWanza kupanga njama za kuchakachua matokeo ya uchaguzi huo.........Hata hivyo Ridhiwani hadi leo hajaweza kututhibitishia ya kuwa kweli alikuwa nje ya nchi kwa sababu hajaweza kuleta kielelezo hata kimoja cha ushahidi................................na Rostam Aziz ushahidi alioleta umesaidia kututhibitishia mtandao wa kifisadi kumbe uko hadi Idara ya Uhamiaji ambako aliweza kughushi mhuri wa kutoka nchini lakini hana mihuri ya Afrika kusini alikodai kuwa alienda..............au wa hapa nchini siku aliyodai kuwa amerudi nchini.......Vinginevyo ushahidi wake unamaanisha bado yuko Sauzi wakati yupo hapa nchini...kama huo siyo uchakachuaji wa ushahidi mimi sijui ni nini tena...........................


  Kwa hiyo hata huyu AG anajaribu kujenga mazingira ya kuvilaumu vyombo vya habari kwa kumjenga Dr. Slaa ingawaje hakumtaja wakati AG hayupo tayari kuzungumzia kama kweli JK alishinda uchaguzi huu kutokana na mazingira yaliyojitokeza........ya NEC kuwanyang'anya wasimamizi wa Majimbo majukumu yao ya kutangaza kura za Uraisi jambo ambalo linahisiwa na wengi ilikuwa njama ya CCM kuhakikisha NEC inampora Dr. Slaa Uraisi na JK kutangazwa kuwa Raisi isivyo halali na kinyume cha sheria...................................

  Kwa hiyo Bw. Werema wewe ndiye anayepaswa kufanya utafiti wa kama kweli NEC ni huru na kama NEC inakidhi mahitaji ya watanzania wa karne hii ya 21 na wala siyo vyombo vya habari kubezwa kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kujua ni nani kati ya JK na Dr. Slaa ni chaguo la watanzania walio wengi............
   
 2. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Kama wanasheria wakuu wa serikali za ccm kuanzia Chenge akaja Mwanyika, hawa wote wamethibitika kuwa ni mafisadi what makes you think Werema is any different ? Especially when he is an appointee of the mafisadi protector!!
   
 3. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Mwanasheria afanye kazi yake ya uanasheria na wanahabari wafanye kazi yao ya uana habari. Na watafiti wafanye kazi ya utafiti. Sina hakika kama wanahabari wote Tanzania walikuwa wajinga isipokuwa yeye Werema, hata watafiti wenyewe wanajua kuwa wananchi wanataka nini. Ndio maana tafiti zao ziliminywa ili wasichafue hewa na kuweka mazingira mazuri ya uchakachuaji. Ana haki ya kutoa maoni lakini sio kuwafanya wote wajinga.
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Nov 7, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Ndiyo maana ninahoji kauli yake kuwa haitakii nchi hii mema.........
   
 5. sensa

  sensa JF-Expert Member

  #5
  Nov 7, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi kwa nini wanatumia nguvu kubwa sana kumshambulia Dr? halafu majina hayo hayo yanarudia katika kila aina ya uhalifu nchi hii,wanafikiri wanaweza wakawadanganya watz mpaka lini?Wametunyima haki yetu wote hao mafisadi tu na siku zao zinapungua kila siku.
   
 6. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #6
  Nov 7, 2010
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,054
  Likes Received: 405
  Trophy Points: 180
  Mwanasheria uchwara. Amesoma wapi sheria?
   
Loading...