Kama mnaenda mahakamani basi jiandaeni kabisa maana gazeti huru la serikali linariport nanukuu:
"WAKATI mawaziri wapya na waliobadilishwa wizara wakitarajiwa kuapishwa leo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amesema uteuzi wa Rais Jakaya Kikwete wa wabunge watatu kuwa mawaziri kabla ya kula kiapo bungeni, ni sahihi wala hajavunja Katiba ya nchi.
Jaji Werema ametoa ufafanuzi huo siku moja baada ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe kudai kwamba Rais amevunja Katiba
kwa kuwateua wabunge hao kuwa mawaziri kabla ya kuapishwa bungeni."
Mwisho wa kunukuu
sosi:HabariLeo | Mawaziri mguu sawa
Tatizo wakubwa walishazoea kuendesha nchi kama 'absolute monarchy'