AG awaonya TUCTA kujihusisha na siasa

Ni kifungu gani cha sheria kinachokataza chama cha Wafanyakazi - as a Union, kutopendekeza mgombea wao?.
 
quote_icon.png
Originally Posted by Mutu
Lete ushahidi hapa wewe unafikiri sheria inaongozwa na hisia.
Kikwete ndio aliingiza maneno ya kutokujari kura za wafanyakazi sasa what,he started it ..........where were the AG.

AG hawezi muhuku JK kuingiza mambo ya mishahara kwenye siasa kwasababu ni bosi wake anaogopa kibarua chake kisije ota nyasi.



Go back wakina Kawawa ndio walikoanzia kupigania uhuru tokea vyama vya wafanyakazi.
Je ni vibaya Tucta kama chama cha kupigania maslahi ya wafanyakazi wakisema as maslahi yenu wafanyakazi concerned mchagueni mtu mwenye sifa hizi na hizi na mtu huyo ni...............


Hapo nakumalizia ni Dr. W.P.Slaa
 
Ushauri wangu kwa wafanyakazi, pamoja na ahadi hizo za kuongezewa mishahara, wasikubali kuipa CCM kura, kwani watakuwa wamejikaanga kwa mafuta yao wenyewe.
Kulipwa mishahara ni haki yao na si fadhila. hiyo wasirubuniwe kwa kuongezewa mishahara ili waipo CCm kura. JK alishazikataa kura za wafanyakazi, na kusababu hiyo wasibweteke wakampa kura tena.
 
TUCTA wako sahihi kabisa,wanachofanya ni kuunga mkono kauli ya Mh. Rais ya kuzikataa kura za wafanyakazi. AG aache ushabiki wake, tunajua kuwa ni kada mwaminifu wa CCM.

Kweli tupu. Na hata TUCTA wasiposimama jukwaani na kusema hilo linalopingwa , sisi tayari message tunayo. Tutaangalia nani atakayejali maslahi yetu. Mmoja kashajitoa mwenyewe kwa kudai hajui cha maslahi wala nini , na hata hataki kura zetu. HE IS OUT PERIOD.
 
nchi hii ina ombwe na uongozi. aliewateua ana kasoro, walioteuliwa wanakasoro, wanaongoza watu wenye kasoro, ambao hawajui thamani ya kura zao.
Kifupi tunahitaji kuamka.
 
I always scoth politicians....ours especially....was it not TFL that helped TANU gain power to the chargin of the colonialists...what about COSATU and ANC?.....KNUT and NARC?.....Chiluba and MMD?...TRADE UNIONS and POLITICS are known bedfellows Mr Assiatant AG...law or no law
 
Hivi kumbe maji yakifika shingoni ndivyo inavyo kuwa eeeh!! hapo JK KACHEMKA yeye kwa kauli yake mwenye alisema haiwezekani hata mfanyaje hawezi kuongeza mshahara na huyu atayegoma atakiona haya! sasa iweje ale matapishi yake mwenyewe??
MIMI NASEMA SIDANGANYIKI KURA YANGU KWA DR. SLAA
 
It is true that you may fool all of the people some of the time; you can even fool some of the people all the time; but you can't fool all of the people all the time."~Abraham Lincoln:confused2:
 
Sina uhakika na ongezeko la mshahara kwa kiasi hicho kwani sijakiona kwenye salary slip yangu ya july, ila bado nasisitiza kuwa kauli ya Kikwete ilikuwa mbaya sana na dharau kubwa kwa wafanyakazi, kuongeza mishahara ili kukidhi mahitaji ya wafanyakazi ni wajibu wa serikali ila bado JK sio chaguo la wafanyakazi, na hii itakuwa fundisho kwa viongozi wengine.
 
Hiyo mbinu waliyoitumia CCM ni ya kizamani.
Sidhani kama wananchi watadaganyika kiurahisi.
Jk akitaka arudishe maneno yake kinywani kama anaweza.
 
Huo mshahara wa kinyemela wa wapi huo? Au ni allowance za muda, au ni rushwa ?
 
Nasubiria tucta wakanushe hiyo taarifa, yawezekana yakawa majungu tu. Mie kwenye salary slipyangu hakuna ongezeko lolote! Kwa hiyo inaweza kuwa habari ya kupika
 
Sizitaki kura zenu bado itaendelea kumtafuna maisha yake yote kisiasa
 
Hahahahahah, serikali ya JK kweli imejaa watu wababaishaji sana. Kwa hiyo kama haya mambo niya kweli, pesa imetoka wapi kwa ajili ya kuongeza hicho kima cha chini kwenda 260K (55K chini ya pendekezeo la TUCTA)? Kumbe hawa jamaa wanazo pesa za kulipa hata zaidi ya 315K? Na mbona hawajapunguza kodi? Kwani madai ya TUCTA siyo mishahara tu.

Dawa yao ni kuzitia ndani hizo pesa na kuendelea kuwashindilia makonde kama mvua ya mawe!! Mwaka huu lazima mabubu wataongea!!:confused2:
 
Rushwaaaaaaaaaaaaa, mi sina imani na serikali ya CCM, JK alisema mshahara umeongezwa kutoka tsh 104,000/= hadi ths 135,000/= ina maana rais kadanganya wafanyakazi au amewajaribu aone reaction yao??????, kumbuka mwaka jana mshahara uliongezwa lakini tukaupata febuary na erreas zilikatwa kodi na fedha kurudi serikalini kama pay as you earn, sasa mimi naona naona huu ni usanii.Hii sio sababu ya kutokipigia kura CHADEMA kwani tumechoka na unyanyasaji na maonezi ya serikali ya CCM.
 
Tena nasikia kuwa walio ongezewa mishahara ni ma-askari tu! ndo serikali ina waogopa. Wengine mlie tu! Kwakuwa umeongezwa kisiri, baada ya uchaguzi mtegemee kurudi kwenye mshahara wa zamani. Hii ndiyo Serikali yenu ya tangu Uhuru ni usanii kwa kwenda mbele. Uongozi umewashinda lakini hamsalimu amri.
Aibu itawapata wengi kama hawaamini wasubiri 31/10/2010. 'MABADILIKO NI LAZIMA'
 
Hawasomi Nyakati ,Serikali ya Kikwete wamechelewa sanaaaa,wangeweza kuzuia hili vuguvugu kama wangeheshimu kidogo TUCTA uongozi na wanachama na wafanyakazi kwa ujumla,mambo yao ya kuupuuza mambo mazito kama haya ambayo yanaweza kuelekeza mustakabari wa taifa unawatokea nyongo sasa.

Ukweli wenyewe kundi lolote sasa hivi chombo chochote cha habari,taasisi,na wananchi mbalimbali,kivyake vyake wanaweza kupendekeza mtu ambaye wanamuunga mkono ndio maana Askofu Kilaini aliposema J.Kikwete ni chagua la Mungu manake alikuwa anazungumza kwa niaba ya taasisi yake kwamba walikuwa wanamuunga mkono na halikuwa tatizo la kisheria wakati huo hata sasa juzijuzi alivyosema akiwa Bukoba halijawa tatizo la kisheria,
Kwa hiyo uwanja uko wazi kwa TUCTA kuamua chama au Mgombea yeyote wanaye ona kwa dhati atashughulikia matatizo yao,wakati umefika kwa watanzania kuondoa uoga dhiti ya watawala wadhalimu wanaotumia chombo cha serikali kinachotumia kodi za wananchi kuwatisha watanzania wakiwemo TUCTA,ni vizuri wamesema mapema ili TUCTA watafute wanasheria watakao wawekea utaratibu mzuri wao kusema waziwazi kabisa na ni wanamuunga mkono,
Hongera TUCTA,mwaka huu ni wenu mwaka wa UKOMBOZI tusipotumia nafasi hii tutajuta kwa miaka hamsini ijayo mapinduzi ya kweli na ukombozi wa nchii yetu nio SASA.
 
Back
Top Bottom