AG anayetuhumiwa na Rais kuchakachua sheria iliyopitishwa na bunge ni nani? Kwanini hajakamatwa?

..AGs wazalendo ninaowakumbuka ni hawa:

..Mark Bomani.

..Joseph Warioba.

..Jaji.Damian Lubuva.

..Andrew Chenge.

..Johnson Mwanyika.

..Jaji.Frederick Werema.

..Jaji.George Masaju.

..Dr.Kilangi
Mkuu hapa unamaanisha 'Wazalendo' au 'Wazawa'?
Kama ni uzalendo naona orodha itakuwa fupi sana
 
" Kwenye Ofisi ya AG alikuwa na tabia ya kufanya amendment ya Muswada uliotoka bungeni. Yaani wabunge wanapitisha sheria, yeye anaeda kubadilisha na kuweka maneno anayoyataka yeye ndo anampa rais asaini. Ni tabia mbaya ilikuwa. " JPM

..nimenukuu kauli ya JPM kama ilivyoletwa hapa JF.

..ni madai kwamba ofisi ya Mwanasheria Mkuu wamekuwa na utaratibu wa kuchakachua sheria zinazopitishwa na bunge, na kupelekea Raisi asaine sheria tofauti na ile iliyopitishwa na bunge.

..kwanini wahusika hawajakamatwa na vyombo vya dola?

..au kwanini BUNGE halijamhoji AG kuhusu suala hili na kupendekeza hatua za kinidhamu dhidi yake?
kosa liko palepale..TATIZO LA VIONGOZI WETU NI KUDHANI WANA AKILI NA BUSARA KUZIDI WALE WANAOWAONGOZA..hili tatizo likifa hatutasikia huu upupu tena
 
Hili nalo neno, tena neno zito. Kwa kawaida(kama nipo sahihi) marekebisho (amendment)yanarudishwa bungeni

AG ni kiungo kati ya serikali na Bunge, nyaraka anazofikisha katika mamlaka za juu ni sahihi kwa mujibu
Inapotokea kukawa na 'alterations' bila Bunge au Exec branch kujua kwa utashi wa AG ni kosa

Kwa jambo hili, Bunge linakila sababu ya kuchukua hatua kwa kujua AG anaingia bungeni na kwenda kinyume na kile kilichojadiliwa ni kuliingiza bunge mkenge.

Serikali nayo inapaswa kuchukua hatua kwavile AG anaiingiza mkenge kwa utashi wake tu. Nadhani vyombo hivi viwili vinawajibu wa kuchukua hatua dhidi ya AG

Hapana mimi nadhani hapa ndipo maamuzi ya mambo mengi nchini hufanana kabisa na mfumo wetu wa utawala. Haiwezekani AG mwenyewe avalishwe lawama hii peke yake. Hatufanyi utafiti wa kufahamu sababu halisi ya tatizo au tukio. Tunafanya maamuzi ya "zima-moto" zaidi.
Kwa mfano swala linalohusu taifa zima linajadiliwa bungeni, linaandaliwa muhtasari maalum, linarudishwa kwenye kamati husika, linajadiiliwa tena halafu linapelekwa rasmi kwa AG likiwa lina sahihi za Kamati za Bunge pamoja na Speaker (nadhania hivyo). Akimaliza kulipitia na wataalmu wake, huliandaa tena kisheria zaidi na kulipasisha kwenye vipengele kadhaa, naamini zipi kamati maalum za sheria katika Ofisi za Mwanasheria Mkuu hadi Wizara husika, linarudishiwa Bungeni tena sasa likiwa pia na sahihi za wahusika kadhaa. Linapasishwa tena na Bunge baada ya kuonekana kuwa taratibu zote zimefuatwa (nasisitiza tena... nadhani hivyo) na kwamba ndicho walichoshauri wabunge na kutunga au/na kupitisha. Iweje AG avalishwe lawama peke yake?
 
Kwani aliyechakachua vifungu vya kanuni za uchaguzi TLS ni nani? Yaani TLS wamepitisha kanuni wamempelekea AG atangaze kwenye gazeti la serikali akaenda kuongeza vifungu vyake na kutangaza matokeo yake wote tunajua TLS waliamua kuzipuuza hizo kanuni na kutumia kanuni za zamani. Ofisi ya AG ni jipu inashangaza hata wasomi wanaoheshimika kama Ade Kilangi anafanya upopompo kama huo.
 
Back
Top Bottom