AG Ajiunganishe kesi ya wanaharakati kama JK ana nia kweli! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

AG Ajiunganishe kesi ya wanaharakati kama JK ana nia kweli!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Feb 7, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Feb 7, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  Sheria ya Office of Attorney General (Discharge of Duties)
  SWALI: KWA Vile Rais Kikwete amesema na yeye ni "mmoja" wa wale wasiotaka Dowans walipwe je atamuagiza Mwanasheria Mkuu ajiunganishe na kesi ya wanaharakati wanaopinga malipo haya kisheria kwa kutumia nguvu alizonazo kutokana na Ibara hiyo ya sheria iliyotajwa? Maana njia pekee ya yeye kuonesha kuwa kweli hataki kulipwa ni kwa AG kutoa msaada wa kisheria kuwapa nguvu wanaharakati.
   
 2. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mzee MwanaKijiji,

  Hilo linawezekana na nafasi hiyo anayo kisheria kama ulivyoweka.

  Tatizo ni alichosema mwanzoni ambacho ndicho anakiamini, kwamba Dowans lazima walipwe. Ameshatoa msimamo wake na sidhani kama itakuwa sahihi yeye kujiunga kwenye hiyo kesi kwa sababu ataiharibu. He is already conflicted!

  Ushauri wangu ni kwamba akae pembeni kwa sababu haki yake ya kujiunga au kutetea ameshaipoteza. Haiwezekani kuwa na imani nae kwamba atatetea vizuri bila ku-prejudice utetezi wa wenzake.

  Wanaharakati hawahitaji nguvu kutoka kwa Mwanasheria Mkuu. Pale hakuna kubeba zege kusema kwamba tukiwa wengi itakuwa nyepesi kubeba. Pale kinachohitajika ni umahiri wa sheria na uwezo wa kujenga hoja. Mwanasheria Mkuu na Wanasheria wa Tanesco wameshindwa kufanya hilo aidha kwa makusudi au kwa kutokuwa na uwezo.

  Ni heri wakajitolea wanasheria wengine ambao wana nia ya dhati na wananchi wanawaamini kusimamia. Hata kama tutashindwa basi haki ionekane imetendeka na itendeke. Sikubaliani na Mzee Mkono 'kuisaidia' serikali kwenye hiyo kesi. Sio kwamba yeye au kampuni yake haiwezi ila wananchi hawana imani naye. Pia, nia hiyo njema angeionyesha wakati wa kuvunja mkataba au wakati wa Richmond!! Alikuwa na nafasi hiyo kama Mbunge na kama Mwanasheria! Nafasi ambayo ndio anataka kuituma sasa kusaidia! Vile vile kesi za BoT bado ziko shingoni mwake, malipo makubwa aliyopokea ni shubiri kwa watanzania anaotaka kuwasaidia.

  Suala la Dowans halipo mikononi mwa serikali, lipo kwa wananchi wenyewe! Wao ndio wanaotakiwa walipe au wasilipe! Serikali ilishatoa msimamo wake. Kauli kwamba 'suala hili lipo mikononi mwa wanasheria' sio msimamo!

  Nashukuru.
   
 3. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Katika hali halisi siyo rahisi kwa mtu yeyote kujua JK amesimama wapi kuhusu malipo ya Dowans. Hii inatokana na ukweli kwamba katika hotuba yake ya juzi alielezea kuunga mkono misimamo miwili inayokinzana; mmoja ukiwa umetolewa na kamati kuu ya CCM, na mwingine na wabunge.
   
 4. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #4
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kikwete ni mtaalam wa kucheza faulo au kucheza na akili za watu, kama mtu alimsikiliza kwa sikio la ndani pale alikuwa anaunga mkono dowans kulipwa alisupot kauli ya pinda na ile ya kamati kuu ya ccm ambapo wote wanataka ilipwe!

  pili hata mtu asiye na ufahamau wa sheria haimuingii akilini Rais asiwajue wamiliki wa dowanas.................................. na kama kweli hawajui tangu limechukua uzito wa juu knye vyombo vya habari na yeye mwenyewe kuhusishwa kuwa mmiliki alipaswa kuwajua wamiliki na siyo swala la kutuambia hawajui wamiliki,,,,,,,,,,,,,,,, huyu anatufanya sisi ni watoto kiakili kama hao anaowaongoza knye tasisi yake ya ccm
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kwani kuna mwingine ameteuliwa baada ya Werema? Maana huyu sasa atapotea kabisa kwenye spotlight maana kila angle aliyojaribu kujitutumua he just got wrong! Kwa hiyo hata hili he'll be afraid to probably be wrong again........... au mkuu umesahau once bitten...
   
 6. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #6
  Feb 7, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hapo ndio tunajua ubaya wa mtu wanayelilia nafasi/ position ya kazi bila kujali ukubwa wa majukumu yake na kujipima uwezo wake. Kama mwakyembe waziri wa serikali ya JK kamtaja mmiriki wa dowans kwwenye kikao halali cha chama chao. Iweje Rais anatoka hadharani kukana kuwajua dowans wala kukutana nao?!. Hatukupaswa kuwa na rais huyu hata yeye anajua. Anapigania andalee kuitwa rais lkn anatajiwa mwizi wa mali ya nchi yake aziba masikio.
   
 7. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #7
  Feb 7, 2011
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,922
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  MKJ,
  Nimekugongea "thenk" kwa ajili hii
  HTML:
  Sipendi kuwa mjinga, sipendi kuonekana mjinga, sipendi kuchukuliwa mjinga. Ninakataa kuwa mjinga. Kama Rais Kikwete hawajui wamiliki wa Dowans basi na Papa hajui Vatican ilipo! Feb 5, 2011.
   
 8. s

  sanjo JF-Expert Member

  #8
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Watanzania tuna safari ndefu ya kupata viongozi wenye kuheshimu wapiga kura na Muumba wao.
   
 9. makandokando

  makandokando JF-Expert Member

  #9
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hivi kazi ya AG ni nini? na kwa nini wali-outsource mawakili wakutetea Dowans kwenye ICC?
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Feb 7, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  Tangu mwanzo ofisi ya AG imeonesha udhaifu mkubwa kweli!!
   
 11. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #11
  Feb 7, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,744
  Likes Received: 3,182
  Trophy Points: 280
  JK ni mtu wa ajabu sana hivi kabla ya kuongea huwa anafikiri kweli au anajiongelea tu. Juzi juzi hapa kikao chao cha majambazi kiliridhia malipo ya Dowans sasa leo anakuja anasema haitambui Dowans sasa huu ni mchezo wa kuigiza au ni nini? Sasa kama haitambui kwa nini anasema ilipwe? Kweli anashindwa kutoa tamko kwamba halipwi mtu hapa maana hii kampuni siielewi. Matokeo yake anarusha tu vijembe oh wamesema oh watasema sasa wewe na hao wanaosema nani ana akili?
   
Loading...